Taharuki: Wananchi waua simba tisa Serengeti

Taharuki: Wananchi waua simba tisa Serengeti

Kwahiyo unataka Simba waachwe waendelee kutafuna mifugo ya watu na mwisho wa siku wawatafune watu kabisa.

Kwanini waishi kwenye hifadhi? Ni ulimbukeni tu. Aliyewapa sumu anatakiwa akatwe kichwa chake ili iwe fundisho kwa wengine..pumbaffu kabisa
 
Hivi wanyamapori wakiharibu mali ya mwananchi mwananchi anapata fidia?
Achaa tu jombaaa, sisi kwetu ni waathirika wakubwa karibu kila mwaka wa uharibifu wa wanyama pori hasa tembo, na hapo sisi tupo mbali sana na hifadhi ila wanatufuata.
Shamba litateketezwa na tembo hadi ukiliangalia hivi unalia tu.
Tukifuatilia fidia, utafatilia hadi ukate tamaa halafu fidia yenyewe wanasema sheria inaelekeza tulipwe shilingi elfu ishirini sijui kwa hekari.
Ila bado siyo sahihi hata kidogo kwa wananchi kuua wanyama pori, siyo wa serikali, ni wa kwetu sote.
 
ngoja nizuie madole yangu ku type ninachowaza juu ya huyu waziri nimetoka ban juz tu
 
Inamaana huko porini simba kuua nyati anaruhusiwa ila nyati akijilinda na kumjeruhi simba mpaka kusababisha kifo inatakiwa hiyo nguvu kazi imsakame nyati kwa kumua simba, pia angewalaumu hao nguvu kazi kwanini waliruhusu simba waingie kwenye makazi ya watu.
 
Waafrika sijui tuna matatizo gani..unamwekea sumu SIMBA MMOJA unategemea atakufa unaemtaka!! Si utakuwa umesababisha mauwaji ya wanyama wengi wakiwemo lion's family, akina fisi, mbwa mwiru n.k.... Kuna mijitu mingine haiogopi dhambi kwa Mungu au pengine ni mipagani tu.
Tuna safari ndefu sana ya kupambana na huyu adui "Ujinga".
 
View attachment 795681
Simba hao waliuawa kwa sumu baada ya kuvamia katika makazi ya wananchi na kuua ng’ombe ndipo ikatokea hatua ya kulipiza kisasi kwa kutia sumu hivyo kusababisha vifo vya simba.

Mbali na kulishwa sumu, mmoja alikatwa miguu, mkia, ngozi ya juu ya mgongo na kuchukuliwa baadhi ya viungo vyake.

Kutokana na vifo hivyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ameagiza Kikosi Kazi Dhidi ya Ujangili cha Taifa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Serengeti kuwasaka watu waliohusika na mauaji hayo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kigwangalla alisema mauaji hayo hayavumiliki kwa kuwa yana athari kubwa kiikolojia, kiutalii na uchumi wa taifa kwa ujumla.

"Bahati mbaya sana ni kuwa anapouawa simba kwa sumu hafi peke yake, inakufa familia nzima ya simba na mara nyingi wanakufa pia wanyamapori wengine wanaodowea nyama na wanaokula mizoga. Walipouawa simba wa Ruaha hivi karibuni walikufa zaidi ya fisi 70 na zaidi ya ndege mbeshi 100, achilia mbali wadudu," alisema.

Alisema pamoja na faida kubwa za simba kwa taifa kiuchumi, Kijiji cha Nyichoka pekee walikouawa simba hao ni sehemu iliyofaidika na miradi ya ujirani mwema kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

"Wanyama hawa jamii ya paka wakubwa ni muhimu sana kwa kuweka mizani ya ikolojia sawa maana wanadhibiti idadi ya wanyama wala nyasi kwa kuwala, bila hivyo hifadhi zote zinaweza kugeuka kuwa jangwa.

"Hakuna mtalii atakayekuja hifadhini asitamani kumwangalia simba, mfalme wa pori. Wanapouawa maana yake tunashusha hadhi ya hifadhi zetu kiutalii, hivyo kutishia kupoteza mapato yanayotokana na utalii," alisisitiza.

Alisema tukio hilo la kuuawa kwa simba wa ikolojia ya Serengeti si la kwanza kutokea nchini kwa kuwa mwishoni mwa mwaka jana, simba wengine watano waliuawa pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.


IPP
kumbe mnyama kwa nnji hii ni anathaminiwa zaid kuliko binadam[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Utalii unawanufaisha nyinyi ...Ng'ombe ndio maisha yetu manufaa yake tunayaona moja kwa moja ....kill those shits
Aiseee!! "Soo sad.

..kweli wananchi wamekwishajikatia zao tamaa siku nyingi kuhusiana na suala zima la National cake.
 
Waafrika sijui tuna matatizo gani..unamwekea sumu SIMBA MMOJA unategemea atakufa unaemtaka!! Si utakuwa umesababisha mauwaji ya wanyama wengi wakiwemo lion's family, akina fisi, mbwa mwiru n.k.... Kuna mijitu mingine haiogopi dhambi kwa Mungu au pengine ni mipagani tu.
walitumwa kuja kijijini kwetu[emoji196] [emoji201] [emoji83]
 
Uhasama hauwezi kuisha hadi pale Serikali itakapokuwa inatoa fidia kwa Wananchi wanaopata hasara kwa sababu ya hivyo viumbe pori! Akili tu inatakiwa na sio ubabe
 
Waafrika sijui tuna matatizo gani..unamwekea sumu SIMBA MMOJA unategemea atakufa unaemtaka!! Si utakuwa umesababisha mauwaji ya wanyama wengi wakiwemo lion's family, akina fisi, mbwa mwiru n.k.... Kuna mijitu mingine haiogopi dhambi kwa Mungu au pengine ni mipagani tu.
Imenisikitisha sana hii!
Mola atusaidie tuthamini mali zetu walahi
 
Waafrika sijui tuna matatizo gani..unamwekea sumu SIMBA MMOJA unategemea atakufa unaemtaka!! Si utakuwa umesababisha mauwaji ya wanyama wengi wakiwemo lion's family, akina fisi, mbwa mwiru n.k.... Kuna mijitu mingine haiogopi dhambi kwa Mungu au pengine ni mipagani tu.
WANGEKULA NGOMBE WAKO NA KUUA MTU KIJIJINI KWAKO UNGEFANYAJE? HAWA WANAOWALINDA HAWAELEWI. NI SHAURI JEMA KAMA HAWA WANYAMA KAMA SIMBA NA TEMBO AMBAO HUPENDA KUINGIA VIJIJINI PESA IWEPO STANDBY WAKIHAIBU MAZAO AU KUUUWA NGOMBE WALIPWE MARA MOJA. HAPI ITAONESHA UMUHIMU WA WANYAMA HAO KWA WANAKIJIJI. BINADAMU AKIULIWA NI SWALA NGUMU ZAIDI ILA FAMILIA IWEKWE KWENYE KUFAMU KUWA WANYAMA HAWANA UTASHI KAMA SISI.WATAELEWA TU.
 
Uhasama hauwezi kuisha hadi pale Serikali itakapokuwa inatoa fidia kwa Wananchi wanaopata hasara kwa sababu ya hivyo viumbe pori! Akili tu inatakiwa na sio ubabe
Umeongea jambo la maana sana.
 
Hao simba wangeua watu mwisho wa siku nao pia wangeuawa so hakuna namna hapo .......

Hongera sana kwa kuwaondoa simba wala nyama za ng'ombe...
 
Back
Top Bottom