Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
...Ya Rasimu ya Katiba ya Muundo wa Serikali Tatu?!.
Wanabodi, naomba nianze na Preamble ya sarufi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili kuhusu semantiki ya neno "kinyume cha maumbile" kwa maana safi iliyomaanishwa ndani ya uzi huu, ili kuepuka matumizi mabaya ya neno hilo yanayohusishwa na mambo mabaya!.
"Umbile" ni linatokana na neno "umbo", yaani muundo halisi wa jinsi kitu fulani kilivyoumbwa!.
"Kinyume cha Maumbile" ni kufanya kitendo tofauti na njia rasmi iliyoainishwa ya jinsi ya kufanya jambo fulani!"
Kwa msingi huo sasa twendeni kwenye mada halisi ya jinsi CCM inavyotaka kutufanya kinyume cha maumbile katika mchakato wa Katiba ndani ya Bunge Maalum la Katiba.
Hivyo tukirejea Umbo la Rasimu ya Katika katika Mfumo wa uundaji wa serikali, rasimu hiyo imeumbwa kwa umbo la mfumo wa serikali tatu. Hivyo maumbile halisi ya rasimu ya katiba ni umbile la serikali tatu!. Ni kufuatia maumbile yake halisia nia ya Bunge la Katiba ni kuijadili rasimu hiyo kwenye umbo lake la asili la jinsi ya kuunda katiba mpya yenye mfumo wa serikali tatu, na rasimu hiyo haikuweka option ya kuibadili maumbile ya rasimu hiyo kutoka maumbile ya serikali tatu, kwenda maumbile ya serikali mbili au maumbile ya serikali moja.
Hivyo kitendo cha CCM kuendelea kushikilia msimamo wa kuibadili rasimu ile kutoka muundo wake halisi wa serikali tatu na kwenda muundo wa serikali mbili, huku ni kwenda kinyume cha maumbile! hivyo inachokifanya CCM ni kutaka kutufanya kinyume cha maumbile!.
Nimefuatilia mjadala katika kipindi cha Tuongee Asubuhi na Star TV kilichokuwa live leo asubuhi, ambapo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mjumbe wa Bunge la Katiba, Alhaj Abdalah Bulembo, amesisitiza msimamo wa CCM itashikilia serikali mbili na utautetea msimamo huo kwa hoja, na kuwataka UKAWA warudi ndani ya Bunge la Katiba, walete mezaji hoja zao za kutetea muundo wa serikali tatu, washindane kwa hoja, hoja itakayoshinda kati ya serikali mbili na serikali tatu, ndipo ipelekwe kwa wananchi wapige kura kuipitisha hiyo katiba au kuikataa!.
Naomba kuuliza, hivi Rasimu ya Katiba iliweka options au za serikali mbili au za serikali tatu?, au CCM inataka kutupeleka kinyume cha maunbile halisi ya Rasimu ya Warioba yenye maoni ya wananchi ambao wengi wametaka serikali tatu?!.
Jee kwenye mchakato wa katiba mpya, jee tuiache CCM ikitupeleka kinyume cha maumbile rasmi ya ile rasimu ya Warioba, au tuungane kuikemea CCM ikubali kurudi kwenye mstari wa kuijadili rasimu ya Warioba katika umbile lake la asili ambalo ndio maoni ya wananchi?!.
NB. Disclaimer: Leo ni Jumapili, ni siku ya ibada kwa baadhi yetu, hivyo naomba michango kuhusu hili la CCM kutaka kuwafanya watanzania kinyume cha maumbile, tulijadili kwa mawazo safi kuhusu matumizi ya neno "kinyume cha maumbile" lijadiliwe maana safi niliyoimaanisha hapa ambayo ni ya umbile la Rasimu ya Katiba na sio kinyume cha maumbile ya tendo jingine lolote nje ya mjadala wa katiba!.
Pasco