Tahadhari - Wikipedia inatumika kubadilisha historia ya Tz na viongozi wake !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Wana JF nimekuwa nikifuatilia historia ya Tanzania na hasa ya viongozi wake na nimegundua njama za makusudi zikifanyika kuipotosha.

Kwa faida ya vizazi vijavyo ni jukumu letu popote pale tulipo kuhakikisha kuwa historia ya nchi yetu haipindishwi na mtu yeyote kwa malengo yoyote yale. Naomba mlio na muda mjaribu kupitia maelezo yanayotolewa kuhusu viongozi wetu wa sasa na wa zamani kama yako sawa katika mitandao mbali mbali.

Nasema hivi kwa sababu kuna tetesi kuwa kuna mkakati maalum unaodaiwa eti unaandaliwa na kikundi cha watu kuibadalisha historia ya taifa letu kwa njia mbali mbali. Mojawapo ya njia hizo ni kupitia vitabu vinavyoandaliwa na hawa watu na lingine ni kufanya wanachodai ni masahihisho kupitia mtandao wa internet.

Nina imani kubwa kuwa wananchi waadilifu hawatakubali hizi njama chafu zionazosukumwa na watu weye visasi na wapenda sifa zifanikiwe.

Wikipedia ni mojawapo kati ya vyombo wanavyovitumia katika kufanikisha malengo yao - nawakilisha.
 
hueleweki.....
unasema hawa watu,watu gani?
viongozi,viongozi gani?
historia,historia ipi?
ya kwao binafsi viongozi au
ya taifa????
 
mkakati maalumu wa kundi lipi?
kwa lengo gani?

ibadilishwe iweje????

bado hueleweki......
 
Mag3
Usiwe na wasiwasi. Tunao akina Companero watatusaidia kuwasuta na kuweka mambo sawa.
 
Back
Top Bottom