TAHADHARI: Utapeli mpya waingia makanisani/misikitini

wang'ambo

Senior Member
Nov 29, 2015
113
27
Habari za leo wanaJF, napenda kuwajuza ulimwengu ulipofika wadau,

Na hii ni baada ya ajira kuwa mziki, kuna aina ya utapeli unaoendelea sasa hivi katika makundi/taasisi za kidini na ngo's flani flani, jana baada ya kutoka ibadani niliandikiwa msg toka namba flani akidai yeye ni mtangazaji toka kituo flani maarufu hapa nchini na kwamba wanataka kuandaa kongamano hivyo nimtumie namba za viongozi na wakuu wa idara hapa kanisani kwetu,

Kabla sijamjibu jamaa huyo aliandika msg nyingine akidai yeye ni mchungaji wangu yupo kikaoni simu yake ni mbovu nimjibu kwa sms, baada ya kuona mkanganyiko huo nilish2ka nikajua hapa naingizwa mjini, nikawa mpole nikawa sijamjibu keshoyake akairudia msg ile lakini kwa namba tofauti

Aliendelea kusisitiza kwamba yeye ni mtangazaji wa kituo flani cha redio kinachohusu maswala ya kuandaa kongamano, baada ya kuona mkanganyiko huo nilimwambia mbona unajichanganya leo unasema hivi kesho unasema vile inakuwaje [HASHTAG]#Hajajibu[/HASHTAG] msg mpaka leo,

Kwa hiyo ndugu zangu kuweni makini kutoatoa namba za watu hovyo na hasa mnaosali pamoja au kwenye kundi moja, binafsi naamini huyo ndg alihitaji namba za watu ili kuwaandikia msg kwa jina la kiongozi wetu hapa kanisani aliemtaja akiomba pesa kwamba amekwama yupo nje ya eneo flani.

Chanzo mimi mwenyewe
 
Back
Top Bottom