COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,622
- 3,696
Wadau;Hizi power bank tunazo tumia kuchajia simu zetu hizi kwa kweli ni MAJANGA.Juzi kati hapa Morogoro rafiki yangu alinusurika kuunguliwa gari lake aina ya HARRIER baada ya Powerbank kulipuka na kuanza kuunguza kiti cha gari, begi la laptop na vitu vingine vilivyokuwepo jirani.Jamaa tulikuwa naye kwenye kikao, alikuwa ameacha hiyo powerbank ndani ya gari lake kwenye begi la laptop. Laptop alikuwa nayo kwenye mkutano. Shukrani za pekee zimuendee mjumbe mmoja aliyekuwa amechelewa kuingia mkutanoni maana yeye ndiyo aliyeona moshi mkubwa ukitoka ndani ya hiyo HARRIER. Jamaa akaja mbio na kusema jamani gari ya fulani kuna moshi mkubwa unatokea ndani yake. Tukatoka nduki nje, duuh kufika pale haraka kufungua milango na kuanza kuzima moto kwa fire extinguisher, michanga n.k n.kBaada ya hapo tukaona powerbank ilikuwa imelipuka kabisa, begi la laptop na documents zilizokuwemo zote zimeungua na sehemu ya kiti cha gari ilikuwa ndiyo imeanza kuungua.
USHAURI: Hizi power bank siyo salama sana. Tuone namna ya kuwa tunazibeba na mahali pa kuziacha.
USHAURI: Hizi power bank siyo salama sana. Tuone namna ya kuwa tunazibeba na mahali pa kuziacha.