Tahadhari: Umeme unaua

Tahadhari: Umeme unaua

clion dismas

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
185
Reaction score
169
JIHADHARI: UMEME UNAUA

Habari ndugu, pole na miangaiko ya hapa na pale kadhalika, mshukuru MUNGU kuzidi kukupa pumzi ya uhai hadi leo.

Bila ya kupoteza muda, twende katika mada husika moja kwa moja.

UMEME watu wengi tunaufahamu kwa kuona matokeo yake, mfano:-

· TAA KUWAKA

· KUCHAJI SIMU

· PASI KUNYOOSHA NGUO

· KUPIKA KWA JIKO LA UMEME

· REDIO, TV KUWAKA n.k

Naam, ni vyeme kabisa na huo ndio umeme ninao taka kukujuza juu ya athari zake ambapo kubwa kuliko zote ni kifo.

Kitaalamu, umeme ni mtiririko wa elektroni( si muhimu sana). Jambo la muhimu ninalotaka uelewe mwisho wa siku ni , Ufanyeje ili ujikinge na madhara ya umeme.

Nimefanya tafiti kwa miaka 5 na nimebaini ya kwamba kuna sababu nyingi ambazo husababisha vifo na madhara makubwa, jambo jema, ni kwamba, zote ni sababu zinazozuilika , lakini, ukiamua ndugu.

Umeme unaua, hii iko wazi na ni kweli kabisa, tunashuhudia vifo mara kadhaa na hakika tunapoteza muda mwingine wapendwa wetu wa karibu.

PITIA VISA HIVI

v Nakumbuka mwanzoni wa mwaka jana( 2017), rafiki yangu( nitamuhifadhi jina lake) alipokea simu kitoka mkoani, nyumbani kwao ya kwamba, mama yake mzazi kafariki.

Alihoji juu ya taarifa hiyo kwa maana muda si mrefu aliwasiliana na mama yake na alikua buheri wa afya, ndugu walimjibu na kumwambia, ni kweli, alikua mzima, lakini alfajiri ya leo alidamka kuelekea shambani kulima, siku iyo mvua ilikua imenyesha, akiwa na panga na nyenzo nyingine. Wakati akipunguza majani ya migomba, panga lake liligusa ule waya wa aluminiamu ambao uwa unaishikilia nguzo ya umeme. Ilisikika sauti ikipiga kelele ikihitaji msaada, lakini kufika pale mtu aliyekuwa karibuna shamba, alikuta tayari mama amekwisha poteza uhai wake.


v kuna kijana mmoja, alikua akijishughulisha na biashara zake chini ya njia ya umeme, umeme wa kawaida wa majumbani, yaani, umeme wa njia moja na wa volti 240, bahati mbaya, gari liligonga nguzo ya umeme na ule waya wenye umeme ulimuangukia kijana, yule kijana alikauka palepale.


v Kadhalika, Watoto 2 walikua wameenda kusenya kuni, mmoja akakweka mtini, akawa anakata mashina ya miti, akakata la kwanza kavu, alipokata shina la pili ambalo lilikua halijakauka, alijikuta kaunguzwa na umeme vibaya sana, mdogo wake akujua la kufanya, alikimbia nyumbani, akawaita nduguze, walipofika, kijana alikwisha fariki zamani. Katika mti huu, kuna nyaya za umeme zilikua zimepita.


v Pia, kuna nyumba moja ambayo iliungua na chanzo kilibainika ilikua ni shoti ya umeme, mtoto mmoja alipoteza maisha. Baada ya uchunguzi kufanyika, ilibainika ya kwamba mfumo mzima wa ethi haukuwa katika viwango stahiki.



Sababu zinazopelekea ajali za umeme nimezigawanya katika Nyanja 3:-

1. Mfumo wa umeme ulio chini ya viwango kwenye majengo, maarufu kama ( wiring)

Ili limekua tatizo la kudumu na ndilo tatizo kubwa linalopelekea kusababisha faults au shoti za mara kwa mara. Umefanikiwa kuweza kuinua jingo, fundi kajitahidi kudizaini jingo katika uzuri wake lakini fundi wa kufanya wayaring’/( wiring) yanatokea makosa.

Muda mwingi, mmiliki wa nyumba aelewi umeme, ajui abc’s za wiring, fundi anakuja anafanya aliyoyafanya kumbe kafunga bomu linaloweza kulipuka muda wowote. Nyaya za umeme gharama ya chini sana/mbovu/feki zinafungwa majumbani, nyaya zisizoweza kustahimili jotoridi la mkondo wa umeme, nyaya zinayeyuka, umeme unavuja, waya wa moto/live na nyutro zinagusana, kinachotokea hapo,ni moto mkubwa sana.

Unakuta mfumo wa ethi ni ovyo, umeme Zaidi ya volti 50 unakuwako kati ya waya wa ethi na moto, jambo ambalo, pale shoti inapotokea, upelekea mtumiaji kifaa kuwa njia ya umeme kuelekea ardhini. Ethi rodi zisizokidhi vigezo na mabo mengine mengi. Haya yote yanafanya mtumiaji wa mwisho, ambaye ni mimi na wewe kuwa katika hatari kubwa sana ya umeme ambao ukiwa unaleta madhara hauchagui, sura, rika wala dini.

Nimeangalia main switch za nyumba kadhaa, jambo nililo baini ni kwamba, baadhi ya nyumba, boxi hili unakuta hali ya hatari sana, yaani, fundi anaunga njia ya umeme wa taa, umeme wa swichi za kuwashia tv na majiko ya umeme njia moja au kwenye fuse moja. Kadhalika, unakuta waya wa moto umeungwa katika eneo husika lakini waya wa nyutro/neutral haujaungwa eneo husika, unakuta uko karibu sana na waya wa moto, kitu kinachopelekea, ukifungua mlango wa main switch, nyaya mbili hizi ugusana. Na main switch nyingine, nyaya ya ethi haijaungwa.

SERIKALI imejitahidi kuweka mfumo mbadala wa kuhakikisha wanaofanya wiring ni mainjinia waliosajiliwa na kiasi fulani tatizo limepungua lakini bado. Kwani, baadhi ya mainjinia wanatumia leseni zao ndivyo sivyo kwa kuwapa vishoka na vishoka wanaharibu majumba ya watu. Nadhani serikali umefika muda sasa, hata kama ni kiasi fulani cha pesa kiwekwe, wataalamu wa umeme kutoka shirika la umma waweze kukagua mfumo wote wa umeme wa jengo kabla ya kuwasha umeme katika jingo husika. Mara zote, shirika la umeme uishia kwenye mita ya mteja.

Na wewe mwananchi, jaribu kufuata mfumo uliowekwa na serikali wa kufunga njia za umeme kwenye jingo lako kuepuka hatari, maana, muathirika mar azote ni wewe mlaji wa mwisho. Epukana na vishoka.



2. Shirika la umeme( KUTOKUWA MAKINI)

Hiki ni chombo kilichopewa dhamana ya kusambaza umeme katika nchi. Changamoto wanakutana nazo nyingi sana katika kutekeleza utaalamu wao. Kwa mfano, msukumo wa kisiasa. Wataalamu hawawi huru kifikra katika kutimiza majukumu yao na wengi wao wanajikuta kuacha ethics au maadili yao ya kazi ili wawafurahishe watu wachache wakati baada ya muda mfupi, tatizo kubwa linaenda kutokea.

Jambo hili uhafifisha taaluma za wataalamu wetu na jamii uwachukulia kama wachumia tumbo na watu wasio na ufanisi katika kutimiza majukumu yao. Wahandisi wa Nyanja hizi, naamini katika kusoma kwenu taaluma hiyo mmesoma WORLD CASES mbalimbali kama ile ya chenobyl na kule fukushima na mkaelewa shida kubwa ilikua ni nini. NAOMBA MKUMBUKE JAMBO LILE, NAOMBA MUISHI MAADILI MLIYOYAPATA, MUWE TAYARI KUACHA MUDA MWINGINE KAZI, AIJALISHI ITAKUEJE, ILI MSIUE WATU. “USALAMA KWANZA”, NAAMINI HIKI NDICHO MLICHO FUNDISHWA.

Mambo yanayo wakumba au niliyo baini ni kama ifuatavyo:-

· Kushindwa kufanya ukaguzi na ukarabati wa mara kwa mara katika njia za kusafirishia umeme

Katika mashamba ya watu, nyaya zimepita na muda mwingine, miti inakua na kufikia nyaya za kusafirisha umeme, kitu kipelekeacho mti kuwa na umeme pia.

· Kutokuwa makini katika ufungaji wa nyaya za umeme, kitu kinachopelekea umeme kuwako hadi kwenye maeneo ya chini nguzo iliposimikwa.

Jambo hili upelekea stay wires, au nyaya za aluminiamu zishikazo nguzo kuwa na umeme, muda mwingi majira ya mvua. Na upelekea athari kwa wapitaji na watoto kiujumla.

Aidha ni vyema pia wananchi tukafahamu jitihada za shirika la umeme, mara nyingi tunahabarishwa katika vipeperushi, vyombo vya habari juu ya athari za umeme kama vile, “ TUSISHIKE NA KUSOGELEA NYAYA ZILIZO KATIKA AU KUANGUKA”, “ KUTOA TAARIFA JUU YA TATIZO LOLOTE LA UMEME ” na mengine mengi.

3. Uhujumu miundombinu

Kuna watu sio waaminifu, sio wazalendo na hawana huruma yoyote juu ya maisha ya wenzao. Sasa unaiba kifaa kinacholinda usalama wa mfumo wa umeme, haujui ya kwamba mbali na kuhatarisha maisha yako, unahatarisha pia maisha ya rafiki yako, ndugu , mkeo au mtoto wako?

Unakuta ni mwananchi wa kawaida au mtaalamu unaiba kifaa kama relay( kwa aina zake) katika mfumo wa umeme, kifaa chenye gharama kubwa tene kinachoweza KUBAINI TATIZO AU SHOTI KABLA HAIJATOKEA NA KUZIMA MFUMO WA UMEME ILI MWANANCHI NA MTEJA AWE SALAMA. Tambua fika ya kwamba huu ni uuwaji kama uuwaji mwingine, unamchukiza MUNGU na huna budi kuacha na kuungama hizi laaana. Karibu kila mwaka, kifo Zaidi ya kimoja juu ya shida ya umeme uripotiwa, je, unafurahi kuona watu wanafariki?

Tutambue bayana, shirika peke yake haliwezi kulinda usalama wa mali na maisha yako juu ya shida ya umeme, kadhalika, hakuna mwanadamu hata mmoja aliyekamilika , haijalishi uelewa wako ukoje, taaluma yako wala nini, TUSHIRIKIANE WOTE, TULINDE MAISHA NA MALI ZETU. Hakikisha pia miundombinu ya shirika haiujumiwi, maana, kuna watu wanakata nyaya za shirika, wanaiba na kwenda kuuza, mara nyingine tunawaona na hatutoi taarifa mamlaka husika na unakuta nyaya iliyokatwa ilikua inalinda usalama wa watu na maisha yao Zaidi ya 1000, na mwanao anapopoteza maisha juu ya shida ya umeme unahuzunika sana. TUBADILIKE.

KIIMANI, KAMA UMEONA HUJUMA YOYOTE ILE AU MITI IMEKUA HADI IMEGUSA NYAYA NA MENGINE MENGI NA TAARIFA HUKUTOA MAMLAKA HUSIKA, HII NI DHAMBI, KWANI JAMBO UNAPOLIJUA NA USILITENDE, MOJA KWA MOJA NI KOSA KWA MUNGU. Umefika muda sasa, penda kuona mwenzako anaishi, penda kuona umeme unatusaidia bila ya athari katika jamii, penda taifa lako, kuwa mzalendo, linda mfumo wa umeme. LINDA MAISHA YA JIRANI YAKO.

NI KUELIMISHANA TUU…

Lengo langu sio kumlaumu mtu yeyote wala kumshitaki.

Lengo langu NI WEWE UTAMBUE MCHANGO ULIO NAO KATIKA USALAMA WA MAISHA YA MWENZIO.

Kwani umeme ni moto, ukiwaka nyumba moja, nyumba ya pili iko katika hatari pia.

Jaribu kufuata haya nawe utawabariki wengi.

mbarikiwe. UKO HURU KUKOSOA KWA LENGO LA KUJENGA, KWA MAONI NA USHAURI PIA.
 
Ni nyaya gani n vifaa gani vinavyomudu umeme vizuri?
 
Ni nyaya gani n vifaa gani vinavyomudu umeme vizuri?


NYAYA YOYOTE AMBAYO INATUMIKA KWA KULINGANA NA UKUBWA WA MKONDO WA UMEME STAHIKI INAFAA. MFANO, MKONDO WA 63A, WAYA WA SAIZI YA MITA ZA MRABA 16 UNAFAA. KADHALIKA, KIFAA CHOCHOTE KILE KINA UWEZO WA KUDUMU UMEME VIZURI ENDAPO KIKIPEWA UMEME ULIOTONGENEZWA KWA AJILI YA UWEZO WAKE. YAANI, KUKIPA POWER KULINGANA NA RATINGS.NATAMBUA KUWAPO KWA VIFAA FEKI NA ORIGINAL ILA NITAOMBA SAMAHANI, SITOWEZA KUTAJA MAJINA YA MAKAMPUNI AU MASHIRIKA YANAYOUZA VIFAA HIVYO KWANI NI KINYUME NA MAADILI. LAKINI NIKUSAIDIE, KABLA YA KUNUNUA KIFAA CHOCHOTE KILE OMBA USHAURI KWA WATAALAMU WA UMEME WALIOSAJILIWA NA SERIKALI, KWA MAANA, WAKIKUSHAURI KINYUME, UNAWEZA KUWAPELEKA MAHAKAMANI. PIA, WAWEZA LIENDEA SHIRIKA LA UMEME LIKAKUSAIDIA KWA USHAURI.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
NYAYA YOYOTE AMBAYO INATUMIKA KWA KULINGANA NA UKUBWA WA MKONDO WA UMEME STAHIKI INAFAA. MFANO, MKONDO WA 63A, WAYA WA SAIZI YA MITA ZA MRABA 16 UNAFAA. KADHALIKA, KIFAA CHOCHOTE KILE KINA UWEZO WA KUDUMU UMEME VIZURI ENDAPO KIKIPEWA UMEME ULIOTONGENEZWA KWA AJILI YA UWEZO WAKE. YAANI, KUKIPA POWER KULINGANA NA RATINGS.NATAMBUA KUWAPO KWA VIFAA FEKI NA ORIGINAL ILA NITAOMBA SAMAHANI, SITOWEZA KUTAJA MAJINA YA MAKAMPUNI AU MASHIRIKA YANAYOUZA VIFAA HIVYO KWANI NI KINYUME NA MAADILI. LAKINI NIKUSAIDIE, KABLA YA KUNUNUA KIFAA CHOCHOTE KILE OMBA USHAURI KWA WATAALAMU WA UMEME WALIOSAJILIWA NA SERIKALI, KWA MAANA, WAKIKUSHAURI KINYUME, UNAWEZA KUWAPELEKA MAHAKAMANI. PIA, WAWEZA LIENDEA SHIRIKA LA UMEME LIKAKUSAIDIA KWA USHAURI.
Kuna jamaa alishauri nyaya nzuri za wiring ni hizi single. Sio zile unakuta ndan zipo 3(LNE) unakuta waya upo mmoja tu ili uweze kudhibiti joto vizuri.
Wewe unazungumziaje?
 
Kuna jamaa alishauri nyaya nzuri za wiring ni hizi single. Sio zile unakuta ndan zipo 3(LNE) unakuta waya upo mmoja tu ili uweze kudhibiti joto vizuri.
Wewe unazungumziaje?

YAWEZEKANA YUKO SAHIHI AU HAYUKO SAHIHI( LABDA NINGEPATA KUMSIKILIZA YEYE MWENYEWE, NINGEELEWA JIBU LA LULUPA).

LAKINI KITAALAMU IKO HIVI,

KINACHOSABABISHA JOTO MARA NYINGI NI MKONDO WA UMEME( CURRENT), PALE UMEME UNAPOPITA KWENYE KIPITISHI CHA UMEME CHOCHOTE KILE, UWA KUNA JOTORIDI AMBALO UZALISHWA( NAOMBA NIELEWEKE NAMNA IO, SITOTAKA KUELEKEA HADI KWENYE MAHESABU YAKE).( YUMKINI, NDUGU YAKO ALIJENGA HOJA KUPITIA HILI, KWAMBA NYAYA ZIKIWA NYINGI, JOTO LAWA JINGI NA IVYO, KUCHEMKA KUWA JUU.)

NJIA YA NDEGE HALIWEZI KUPITA GARI MOSHI. UKIFUNGA UMEME WA NJIA TATU KWENYE NYUMBA YA UMEME WA NJIA MOJA, UTAKUWA UNATAFUTA MATATIZO MAKUBWA SANA.

LAKINI PIA, JOTORIDI LAWEZA SABABISHWA NA LOOSE CONNECTION. UNAKUTA UNACHOMEKA PLUG YA KIFAA KWENYE MATUNDU YA SWITCH SOCKET NA ALIFIKI HADI MWISHO. HAPA KUTAKUWA NA USUMAKU, KUVUTANA AMBAKO UPELEKEA UMEME KUZALISHWA KWENYE ILO GEPU NA MWISHOWE, JOTO KUWA KUBWA KWENYE WAYA NA KIFAA HUSIKA.

PIA TAMBUA, JOTO NA UMEME HUWEZI KUVITENGANISHA, BALI WAWEZA VIWEKA KATIKA HALI ISIYO NA MADHARA.

JOTORIDI HILI MARA NYINGI KILA WAYA UNA KIWANGO CHAKE STAHIKI CHA KULIVUMILIA, NA ITAKUA IVYO ENDAPO TU, WAYA WENYE KIASI SAWIA UKITUMIA KATIKA UMEME SAWIA. LAKINI WAYA MDOGO, UTUMIKE KUPITISHA UMEME MKUBWA, WAYA UTACHEMKA, PLASTIKI YA JUU ITAUNGUA, NYAYA ZITAGUANA, NA BOMU LA MOTO LITATOKEA.

SWITCH SOCKET ZOTE, ZILE AMBAZO UNACHOMEKA SIMU KUCHAJI NA UNAUNGA KUANGALIA TV, ZINATUMIA NYAYA 3, LIVE, NEUTRAL NA EARTH(LNE), NA ZINA KIPENYO STAHIKI KULINGANA NA UMEME WA MAJUMBANI, KAMA NI WA NJIA MOJA( SINGLE PHASE) AU NI WA NJIA TATU.

UNAPOTUMIA STRANDED WIRES KUNA FAIDA NYINGI( KITAALAMU), YAANI RUNDO LA WAYA NDOGONDOGO KWENYE WAYA MMOJA, LAKINI, KILA KITU HUTUMIKA KULINGANA NA KAZI HUSIKA.

MOJA YA FAIDA NI KUPUNGUZA KELELE, YAANI, ELECTRICAL NOISE KWENYE MAWASILIANO.
NAZIDI KUKUSISITIZIA, USHAURI WOWOTE WA KIUFUNDI, UPATE KWA MTU MWENYE TAALUMA YA UFUNDI NA ANAYETAMBULIKA NA SERIKALI. WENGI WETU MTAANI, TUNAJALI MATUMBO YETU.
 
Nafuatilia kwa makini hii mada, hivi punde nimetoka kufanya wiring kupitia mafundi wa mtaani na sasa nafuatilia tanesco waniunganishie umeme. Nimeshtuka kidogo, hii thread kama imeniamsha, nimekosa uhakika na alichokifanya fundi kama atakauwa kafanya kwa usahihi ama lah.

Pia kuhusu vifaa vya wiring kama ni sahihi au feki. Vipi pia kuhusu gharama za kuingiza umeme baada ya wiring, nimepeleleza ni kama laki 3 na 21 elfu, ndo bei zake ama inategemea na mahali? nawezaje kujua kama wiring imefanyika vizuri?
 
Hakuna haja ya kuchukua tahadhari ya umeme mkuu, maana huku kwetu tulisha ng'olewa hadi nguzo za umeme kwasababu ya madeni (vyuma kukaza
 
Nafuatilia kwa makini hii mada, hivi punde nimetoka kufanya wiring kupitia mafundi wa mtaani na sasa nafuatilia tanesco waniunganishie umeme. Nimeshtuka kidogo, hii thread kama imeniamsha, nimekosa uhakika na alichokifanya fundi kama atakauwa kafanya kwa usahihi ama lah.

Pia kuhusu vifaa vya wiring kama ni sahihi au feki. Vipi pia kuhusu gharama za kuingiza umeme baada ya wiring, nimepeleleza ni kama laki 3 na 21 elfu, ndo bei zake ama inategemea na mahali? nawezaje kujua kama wiring imefanyika vizuri?
Aisee hawa jamaa wa mtaani wanajifanya fundi lakini wengi hawajasajiriwa kama mainjinia wa kufanya hiyo kazi.
Wanatumia ujanja, ukijaza zile fomu za Tanesco na kuwapa wao wanaandaa michoro na kufanya wiring kwenye nyumba yako halafu wanaenda kwa mkandarasi aliyesajiriwa na wanamlipa pesa anagonga mihuri zile fomu na kisha zinarudishwa Tanesco.

Kwahiyo Tanesco watajua nyumba yako imefanyiwa wiring na mkandarasi mwenye utaalam mkubwa maana amesajiriwa, kumbe ni uongo.
Kwahiyo kama wamefanya kazi iliyochini ya kiwango, au kutumia vifaa feki hasara ni yako mwenye nyumba.
Wanapenda vifaa vya bei rahisi ili usione gharama kubwa, earth rod nyingi ni feki yaani ni chuma kilichopakwa rangi ya shaba baada ya muda kinaoza kwa kutu huko ardhini na mtu unakuwa hujui kama kishaoza maana kimefukiwa chini.
 
Nafuatilia kwa makini hii mada, hivi punde nimetoka kufanya wiring kupitia mafundi wa mtaani na sasa nafuatilia tanesco waniunganishie umeme. Nimeshtuka kidogo, hii thread kama imeniamsha, nimekosa uhakika na alichokifanya fundi kama atakauwa kafanya kwa usahihi ama lah.

Pia kuhusu vifaa vya wiring kama ni sahihi au feki. Vipi pia kuhusu gharama za kuingiza umeme baada ya wiring, nimepeleleza ni kama laki 3 na 21 elfu, ndo bei zake ama inategemea na mahali? nawezaje kujua kama wiring imefanyika vizuri?


SAMAHANI KWA KUCHELEWA KUCHANGIA JUU YA HILI, LAKINI NAONA NDUGU WAMEELEZEA VYEMA.
VIPEPERUSHI VINGI VYA SHIRIKA LA UMEME VIKO WAZI NA VINAPATIKANA VIKINYUMBUA GHARAMA ZOTE ZA UMEME PAMOJA NA UFUNGAJI WAKE, TEMBELEA OFISI ZAO UCHUKUE VIPEPERUSHI HIVI. KWANI ILE NI OFISI KWA AJILI YA KUKUHUDUMIA WEWE MWANANCHI NA VYATOLEWA BURE KABISA.

KUHUSU KUJUA KAMA WIRING NI SAHIHI, NIKUSIHI NDUGU, NENDA HAPOHAPO SHIRIKA LA UMEME, KUTANA NA MHANDISI MWANDAMIZI( SENIOR REGIONAL ENGUNER), MUELEZE, NAAMINI ATAKUPA USHAURI MKUU NA MZURI KWA AJILI YA KUONDOA WASIWASI ULIONAO. NAAMINI, WATAALAMU WATAFANYA UPEMBUZI YAKINIFU KABLA YA WEWE KUWASHIWA UMEME.

ILA NIWASII, TUMIENI WAHANDISI AMBAO WANA LESENI NA WAMESAJILIWA NA SERIKALI KUEPUKANA NA SINTOFAHAMU BAADAYE.

YUMKINI LIKAJA TOKEA JANGA LA UMEME, KAMA ULIPITA NJIA YA PANYA, HUWEZI LIPWA FIDIA NA SHIRIKA, NASISITIZA, HUWEZI KULIPWA.
 
Back
Top Bottom