Tulio wengi wanaotaka mabadiliko nchini tunafurahishwa na movement zenu na tumepata tumaini jipya kuelekea mabadiliko ya kweli. Lakini tuna kila wasiwasi kutokana na uzowefu wa nchi hii pale inapofika wakati harakati za mabadiliko zinapogusa interest za watawala mara nyingi hutokea yasiyotabiriwa.( Mungu aepushie mbali ). Kwa muktadha huo basi , mimi naomba nitoe tahadhari hizi. 1.Kwanza kipindi hiki mjuwe mmeigusa system ilivyo kuanzia bunge la katiba na bunge la bajeti hasa kuhusu muungano, kwa kuwa huu muungano ndio chaka la watawala kuficha mambo yao basi kutazuka mambo mengi ya hatari ikibidi hata jaribio la kupotezwa watu maisha NAOMBA MUWE MAKINI MARA 100 kuepuka kutoa mianya ya kudhuriwa hasa katika SAFARI ZENU MIKOANI. Tafuteni washauri wenu wa KIUSALAMA ili kuwapa mikakati mizuri zaidi. 2. Kuna kila dalili umoja wenu unawatisha wahafidhina watawala kote Zanzibar na Bara na wako mafichoni kuja na mkakati wa kuvunja umoja wenu immediately, hawatoacha kutumia mianya ya tofauti zenu katika umoja wenu ili kupandikiza mgogoro na hatimae kuvunja nguvu yenu, kamwe msiwe rahisi kwa hilo na mjifunze kwa yaliyopita haiwezekani kuiondowa CCM bila kuwa wamoja, hawa jamaa wameota mizizi katika system kuanzia muhimili wa mahkama, serikali/ utendaji na bunge na hata katika vyama vingi vya upinzani wameweka nyenzo imara. Sahauni tofauti zenu, jengeni umoja imara, aminianeni, tengeneza mkakati wa kitaalamu, shambulieni kwa hoja, muwe wanganganizi wa hoja, toweni data na facts katika hoja, wapotezeni kujuwa mikakati(tunza siri), ongeza intelijensia na kuchimbua katika Banks za mikiakati yao finyu na propaganda, panga safu kali ya mashambulizi, buni njia za kupata bajeti kwa wakati, kuweni waangalifu wa hali kwa jamii na hisia zao halafu muwe tayari- nawaambia jamaa hawawezi kutoka safari hii tafadhali kuweni makini na haya inatosha.