Tahadhari na waendesha bodaboda!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari na waendesha bodaboda!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwalimu, Dec 13, 2011.

 1. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Leo asubuhi maeneo ya mbezi karibu na shule ya HOPAC nimeona gari moja ikiwa imeteketea kwa moto...nilipouliza kulikoni nikaambiwa gari ile imechomwa moto na waendesha bodaboda baada ya gari hilo kumgonga mmoja wao na baada ya mabishano kati yao ndipo walipoamua kulichoma moto gari hilo! Na kama mnavyofahamu hawa jamaa jinsi wanavyojikusanya kwa wingi pindi mwenzao anapopata ajali....

  Madereva wa magari kuweni waangalifu sana mnapokumbana na hawa jamaa ukigongana nao manake wanakuja jeshi kama nyuki na kama uko peke yako inakuwa noma zaidi!

  Nawasilisha...
   
 2. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa wakianza kuja ni kuwachapa bastola tu, kuna jamaa yangu aliwachapa bastola baada ya mwenzao kujiingiza barabarani akagongwa sasa wakati anataka kumsaidia kumpeleka hospitali wakaja mmoja akampiga mkewe jamaa kuona hivyo akamchapa risasi pale pale akafa, na yule aliyemgonga hakumpeleka hospital mpaka polisi walipokuja naye akavuta. Wale wengine woote wakalala mbele. Ushauri ukimgonga karibu na kijiwe chao tafuta eneo lisilo na foleni lala mbele wakikufukuzia wakanyage na gari maana ni vita hiyo.
   
 3. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani wahusika waliangalie hili kwa makini kwani haya matukio ya huu umoja haramu wa hawa bodaboda unaanza kuvuka mipaka
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Waendesha "boda boda" wengi ni ex-criminals!

  Ukigonga "bodaboda" usisimame au kama una silaha "shoot & kill" yeyote yule atakaye kuletea ujuaji!
   
 5. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  duh hii ni hatari sana maana wafanyacho si sahihi , ajali mara nyingi inatokana na uzembe wa dereva wa boda boda .. kamaa ikikutokea hakikisha unachukua namba ya pikipiki husika na kamata yeye na wenzake weka ndani
   
 6. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nasikia kuna Hiace nyingine ilichomwa moto last week kwa ajili ya hawa hawa jamaa wa boda boda!
   
 7. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,632
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  hao jamaa ni NYUKI! Wana mbinu chafu sana,hebu ona hii hapa ambayo wanaitumia sana hapa mwanza: mmoja wao akigonga mtu wenzake wanajifanya ni wananchi wenye hasira na kuificha pikipiki iliyogonga,polisi wakifika hakuna pikipiki na hivyo ushahidi hakuna! Baadae pikipiki urejeshewa mwenyewe kimya kimya!
   
 8. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  mama mmoja arusha alichomewa land cruser prado baada ya kumgonga mtu wa boda boda
   
 9. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mkuu, nakubaliana na wewe, hii sector isiyo rasmi imetoa cover na ajira kwa criminals and ex criminals.

  Ikigonga bodaboda, tambaa tu, au mparamie tena umalizie na ulale mbele.
  Washenzi hawa walichoma prado ya mama mmoja arusha, kwasababu tu amemsukuma kidogo bodaboda.
   
 10. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Madereva wengi hamko makini barabarani mnazarau na ivyo vigari vyenu vya mkopo hiyo ndo dawa yenu
   
Loading...