Tahadhari na Taxi Dar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari na Taxi Dar!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bob K, Jun 23, 2009.

 1. B

  Bob K Member

  #1
  Jun 23, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kama wiki tu limepita rafiki yangu kaka angu mmoja kwa jina namhifadhi alipopatwa na mkasa huu.

  siku ambayo kulikuwa kuna mvua mvua akiwa kapungia teksi njiani akiwa ana mpango wa kwenda maeneo ya nyerere road teksi ikasimama na kwa kuwa kulikuwa na mvua haraka akatumbukia,canasema dereva alikuwa ni mtu mzima wakati wanakwenda akamweleza kuwa kwa kuwa alikesha na kwa kazi na asubuhi ikambidi adamkie kwa mgonjwa wake muhimbili hivyo basi akaomba ampigie kijana wake ili atakapomfikisha yeye abiria yeye aweze kurudishwa nyumbani akapumzike na yule shunta wake aendelee na kazi,kwa kuwa alikuwa ni mtu wa makamo my friend akumtilia shaka loo kumbe!! anamwita jambazi mwenzakle kilichofanyika ni gari kuelekea majani ya chai kue kwenye ofisi za mobitel wakati huo yule jamaa kesha panda na yuko kwenye uskani na yule mzee karudi nyuma anapekua mfuko wa abria jamaa akashutuka kumuuliza vipi mzee akaambiwa tulia kama ulivyokaa bisu lime toka na jama wa mbele nae kwenye jaketi katoa bisu jamaa kwa kuwa alijua mfuko unanguo tu za kupeleka kwa dobi akutaka kuuleta vurugu hivyo ikabidi atulie walichoambulia ni walleti yenye pesa kidogo miwani yake ya macho fuko la nguo chafu wakamwachi.

  jamani kuweni macho na taksi za juu kwa juuu pia usidhani huyu dereva mzee ndio wa maana wengine ni afadhali ukutane na chui angalia stahili aliyotumia mi nimechoka ooh kijana wangu kumbe naye ni jambazi. this is dar es salaam wazee nao ni majambazi.

  ushauri tuu kwa kamanda kova taksi zote rangi moja zipigwe na manamba ya ubavuni makumbwa lakini kama kuna mwenye mchango mwingine naomba achangie katika hili kudhibiti maana matukio hay si mageni.
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Wazo zuri sana.
   
 3. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,076
  Likes Received: 15,730
  Trophy Points: 280
  jamani kuweni macho na taksi za juu kwa juuu pia usidhani huyu dereva mzee ndio wa maana wengine ni afadhali ukutane na chui


  Mwenzangu "ume click" penyewe ni kweli hawa madreva wazee sio watu. Mie mwenyewe yamenikuta 13/6/2009 ingawaje sio ujambazi lakini nimelinganisha kama ujambazi. Nilichukua teksi tena dreva ni babu kabisa wa kiislaamu hapo Barabara ya Bibi titi karibu na geti la CBE, yule babu nikamwambia anipeleke Magomeni Mikumi, akasema 4,000/= lakini cha ajabu tulivyofika pale nilipokuwa nakwenda nikampa 10,000/= yule babu akakata 5,000/= nikamwambia si tumepatana 4,000/= .eeee bwana alinotolea maneno ya kiswahili ya ajabu ya matusi ambayo siwezi kuyaandika hapa.

  Kwa hayo yaliyonikuta na mie nakazia kwamba madreva wazee tusiwashobokee kabisa hawana nidhamu
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Unataka sema nini hapo! Pole kwa kutapeliwa!
   
 5. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,076
  Likes Received: 15,730
  Trophy Points: 280
  Nataka kusema kwamba alionekana ni muumini mzuri wa dini yake na ana heshima zake
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Reminds me of mtu mzima ovyooooo
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  In general,safety percentage in dar is dropping rapidly,dont trust anybody easily.
   
 8. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,076
  Likes Received: 15,730
  Trophy Points: 280
  Kweli ndugu yangu
   
 9. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yeah Taxi drivers Bongo hawaaminiki. Kuna dada mmoja yeye alikubwa na umauti kabisa kwani dereva alimpa kitu kama mwanasesere na akamlazimisha amunyonyeshe na inaonekana mwanasesere alinyonya damu yote na dada yule kafa. Ni washirikina pia. Ushauri wangu: Jitahidi kuwa na Tax driver wako unayemfahamu mpigie simu aje akuchukue huko uliko ni salama zaidi.
   
 10. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,076
  Likes Received: 15,730
  Trophy Points: 280
  Yesu na Maria!!!!
   
 11. R

  REOLASTON Member

  #11
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu kwa yaliyokukuta.

  Kuna kisa kingine kaka yangu siku moja anatoka kwenye mihangaiko akafika pale tangi bovu ilikuwa saa 2 usiku mvua inanyesha akasikia watu wanamwita tena kwajina kabisa wakamwambia tunaomba utusongeze jirani. akasimama akawachukua ila yeye akajaribu kuwakumbuka hakupata jibu akafikiri ni majirani tuu walipofika pale kunduchi kona wakamwambia tunashuru tumefika wakashuka na laptop yake. anafika nyumbani ndio anahamaki hamna bag.

  siku hizi hakuna uaminifu kabisa
   
Loading...