Tahadhari: Mshauri wa familia kampa mimba mke wangu

mwl. mziray

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
597
397
Ndugu zangu napenda kuwashirikisha kisa hiki cha jirani yangu ili muwe makini na hawa washauri wa familia zenu.

Jirani yangu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya (Pumu) kwa muda mrefu hali iliyopelekea kushindwa kumtendea haki mkewe katika maswala mazima ya vuta nikuvute wawapo ulingoni.

Hali hii ilileta migogoro ya mara kwa mara katika familia na kupelekea kuibuka kwa mshauri wa familia ambae ni jirani aliyeokoka na kumpa Yesu maisha yake.

Kila mgogoro ulipoibuka mshauri huyu alijitokeza na kuwapatanisha ila baadae mambo yalienda kombo na ndoa kuvunjwa na padri kutokana na malalamiko ya mwanamke kukosa utamu ipasavyo.

Kama tujuavyo dunia haina siri, yalisikika mengi kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi kati ya mshauri na mke wa jirani ambao wote ni majirani zangu na hatimae mimba ikabebwa na baadae kuzaliwa mtoto afananae na mshauri kama vile katolewa copy.

Hali hiyo imesababisha msongo wa mawazo kwa jirani yangu kwani katika ndoa yao walishapata watoto watatu.

Ushauri wangu kwenu ndugu zangu kuweni makini sana na hawa washauri mnaowashirikisha mambo ya kifamilia.
 
Ndugu zangu napenda kuwashirikisha kisa hiki cha jirani yangu ili muwe makini na hawa washauri wa familia zenu.

Jirani yangu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya (Pumu) kwa muda mrefu hali iliyopelekea kushindwa kumtendea haki mkewe ktk maswala mazima ya vuta nikuvute wawapo ulingoni.

Hali hii ilileta migogoro ya mara kwa mara ktk familia na kupelekea kuibuka kwa mshauri wa familia ambae ni jirani aliyeokoka na kumpa Yesu maisha yake.

Kila mgogoro ulipoibuka mshauri huyu alijitokeza na kuwapatanisha ila baadae mambo yalienda kombo na ndoa kuvunjwa na padri kutokana na malalamiko ya mwanamke kukosa utamu ipasavyo.

Kama tujuavyo dunia haina siri, yalisikika mengi kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi kati ya mshauri na mke wa jirani ambao wote ni majirani zangu na hatimae mimba ikabebwa na baadae kuzaliwa mtoto afananae na mshauri kama vile katolewa copy.

Hali hiyo imesababisha msongo wa mawazo kwa jirani yangu kwani ktk ndoa yao walishapata watoto watatu.

Ushauri wangu kwenu ndg zangu kuweni makini sana na hawa washauri mnaowashirikisha mambo ya kifamilia.
Sasa wewe mwalimu Mziray kwani ungesema kweli kuwa wewe ndio ulioumizwa na sio jirani,je ingekudhuru nini?aaah Mziray bhaana.,.,..
 
Na ndiyo maana nilishamwambia wife marafiki zangu wanaume aache wawe marafiki zangu tu na yeye asijilegeze kwa kigezo cha huyu na Shemeji yangu hawezi nifanya kitu..Hapana kuna watu hawana cha ushemeji wife akimchekea mara 1,2 jamaa keshahisi waife anampenda na ataanza ujinga na shetani sometyms ana nguvu.....Na marafiki za wife huwa sitaki mazoea nao kabisa tena wakati wife hayuko nao kabisa...
 
Walokole bana ndio zao...kujiweka karb na matatizo ya watu as if wao hawana matatizo...kumbe wanatafutaga tunda la mti walile bila kushawishiwa na nyoka
Hahaha,kujiweka karibu na matatizo ya watu,.... mi si muamini binadanamu now zamani hawa washika dini tuliambiwa tufutate maneno yao na si vitendo, lakini now akili za kuambiwa tuchanganye na zetu hayo maandiko hawachelewi kuyapindua.
 
Sasa wewe mwalimu Mziray kwani ungesema kweli kuwa wewe ndio ulioumizwa na sio jirani,je ingekudhuru nini?aaah Mziray bhaana.,.,..
Hahaha sio mimi ndg yangu, huyu ni jirani yangu tangu mwaka 1999 nikihamia huu mtaa nnaoishi nlimkuta kashajenga tayari na ana familia yake.
 
Masahibu ya mke wangu na mimi na yabeba kichwani. Nayatatua mimi mwenyewe. yakinizidi nakaa pembeni nayaangalia matatizo yangu kwa kumuachia Mungu ayatatue.
Ni jambo jema kwakweli maana ikiwakaribisha watu wayafahamu matatizo yako ndo wanatumia njia hiyohiyo kukupindua.
 
Walokole bana ndio zao...kujiweka karb na matatizo ya watu as if wao hawana matatizo...kumbe wanatafutaga tunda la mti walile bila kushawishiwa na nyoka
Mbaya zaidi jamaa anaachiwaga aongoze ibada kanisani. Mchungaji kapewa taarifa ili amsimamishe kuhudumu ila hana ubavu wa kumzuia kutokana na uwezo wake kifedha.
 
Na ndiyo maana nilishamwambia wife marafiki zangu wanaume aache wawe marafiki zangu tu na yeye asijilegeze kwa kigezo cha huyu na Shemeji yangu hawezi nifanya kitu..Hapana kuna watu hawana cha ushemeji wife akimchekea mara 1,2 jamaa keshahisi waife anampenda na ataanza ujinga na shetani sometyms ana nguvu.....Na marafiki za wife huwa sitaki mazoea nao kabisa tena wakati wife hayuko nao kabisa...
Hapo umejenga msingi imara. Siku hizi shemeji-shemeji kumbe kuna kinachoendelea nyuma ya pazia...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom