Wana jf wenzangu..,kuweni makini sana pale mnapotaka kufanya maamuzi ya kutaka kupanga au kununua kitu
Wengi wa madalali hasa hapa bongo wanatumia nguvu za giza kuwalaghai watu katika kufanikisha azma yao ya either kupangisha au kumuuzia mtu kitu, mfano labda unataka kununua nyumba au kiwanja...,dalali atakupeleka kwenye nyumba au viwanja mbalimbali labda wewe hujaridhika navyo yeye anachokifanya anakupumbaza unajikuta unanunua bila hata kujitambua ili mradi yeye chake cha udalali akipate,
Nina ushuhuda wa hili yamemkuta rafiki yangu kauziwa nyumba hata yeye mwenyewe binafsi anashangaa ilikuwaje akakubali kununua sehem hatarishi kama hyo
Nilipokuja kuhoji baadhi ya madalali wakakiri kabisa kuwa uchawi ndo mtindo wao wa maisha ili kufanikisha mipango yao hasa kwa wateja wao wasumbufu
Think twice before hujafanya maamuzi ya kufanya biashara na madalali
Nawasilisha