Naam, Bwana Zitto Sikia haya ninayoenda kuandika hapa. Siasa zetu katika nchi za kiafrika ni zaidi ya Siasa.Ujenzi wa chama si kazi ya lelemama kwanza inahitaji watu makini,pesa,mipango mkakati iliyo madhubuti na uwanja sahihi wa kufanyia siasa zenyewe.
Siasa zetu za kiafrika sio sawa na zile za nchi zilizoendelea, kwamba sera pekee zinaweza kumshawishi mtu akuunge mkono katika chama chako, hapa kwetu unajua vyama vyetu wafuasi wengi wana matarajio ya muda mfupi na wanalenga kupata jambo fulani kipindi fulanI, katika muktadha huu utakuta Migogoro mingi inaibuka kwenye vyama hivi ambavyo havina rasilimali za kutosha mwisho mgogoro ukikomaa utakuta chama kinakufa kifo cha kawaida, na hapa sina maana chama kifutwe kwa msajiri.
Hakika kuna matarajio uliyonayo moyoni mwako lakini hayataweza kutokea katika siasa za ACT maana sasa wale waliokupokea wanahitaji muda ili waanze kupishana na wewe na hapo ndio utajikuta unakuwa Easy target.Chama kikiyumba utakuwa unajiona unalo jukumu la kurekebisha mambo na hapo Zitto utakuwa hauna amani tena moyoni utakuwa unajutia yale yaliyotokea na yanayobeba historia ya maisha yako kisiasa.
Sasa jukumu unalo tena zito,kipindi hiki unapoangalia mbele kwenye uchaguzi mkuu ujao,hakika itakuwa ni kazi ngumu mno wewe kurudi bungeni katika kipindi hicho ijapokuwa unaweza ukadhani ni rahisi lakini nataka nikwambie kwamba si rahisi maana kazi uliyonayo itakuwa kukijenga chama na si kujenga himaya yako ndani ya ACT,Akina Mwigamba naweza kusema hakuna chemistry kati yako na Mwigamba na hilo litakuwa tatizo la msingi.
Mwigamba anaamini katika mawazo yake na wewe pia, kamwe hamtaweza ku compromise pindi mkitofautiana katika harakati zenu mlizo anza.
Safari hii uliyoianza ni tofauti kabisa na ile uliyoianza pale ulipokua na umri wa miaka 16. kipindi hicho ulipata mafanikio mengi ndani ya siasa na nje ya siasa, ulipewa nafasi na chama chako kutenda majukumu makubwa,lkn safari hii ukiwa na umri wa 39 umeanza safari mpya yenye mashaka mengi.