Tahadhari kwa Zitto Kabwe

Tahadhari kwa Zitto Kabwe

Nani anamfuatilia mwenzake kama siyo wafuasi wa zzk na act kuendelea kuiandama cdm utadhani cdm ndio chama tawala?Hii inajionyesha kuwa act haina lengo la kuing'oa ccm madarakani bali ni kudhoofisha upinzani ili ccm iendelee kutawala milele kwa kuhujumu matumaini ya watanzania
kwa taarifa yako hakuna mwenye muda na nyie mijusi. au mnajipa promo tu humu? mbona thread zenu juu ya zitto haziishi humu? mara mjifanye mnamshauri na upuuzi mwengine kuhusu zitto. nawashauri fanyeni yenu muacheni na zitto afanye yake.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Kumbe adui wa ACT ni CHADEMA si CCM!
 
mtajifanya wenyewe kuwa washauri wa zitto. lakini tunajua inawauma sana ndo maana zitto hawaishi kwenye hizo nazi zenu juu ya shingo. mnaonaje sasa mkaendelea kumsifia godless lema-mbowe-slaa-tobo-mbuga? maana zitto sio saizi yenu. au mnafikiri zitto ni lema au sugu?

Kama unajua hivyo kinachokuuma ni nini sasa mkuu au kwa kuwa unajijua kuwa wewe si ACT ila ni mpiga kelele wa CCM !! Sisi ngoma tunaipiga kimyakimya . Kama huyo jamaa yako angekuwa ni mashuhuri sana kuliko CHADEMA ndo angesindikizwa na wafuasi 12 wapya na tena usiku!!? ha ha ha kazi mnayo, baada ya wiki moja ACT itakuwa ndo imezikwa jumla mpaka atakapokuja mgombea urais wenu mtarajiwa.
 
Kaka Zitto alishinda kata 9 kati ya 11 Kigoma Kaskazini jee kuna ushindi landslide zaidi ya huo? Kusema kwamba Kigoma Kaskazini inaweza kwenda CCM hilo kaka nadhani utakuwa umekosea, UKAWA hawezi kusimamisha mgombea Kigoma Kaskazini sababu hiyo ni wastage ya resources.

Kigoma yoyote Zito akigombea anashinda, sababu that is facts huko kwao yeye ni shujaa wao. Pili, katika majimbo ambayo ama CUF au CDM walikuwa na wagomebea wenye nguvu sawa na UKAWA wakigawa jimbo kwenda kwa moja ama CUF au CDM basi jua mwingine atajiunga ACT. Zitto is not stupid, yeye sherehe yake ni UKAWA kwani anakuja na mbadala au alternative.

Anachotakiwa ni kushinda wabunge 5-10 ili apate pesa ya Ruzuku, baada ya hapo miaka 5 ijayo akafanya national politics. Kitila anajua fika kabisa kwamba wao kushinda national politics ni ndoto za mfalme njozi, lakini wanaweza kushinda Kigoma, Tabora na wakatoa upinzani mkali sana baadhi ya sehemu kama Arusha. Ninavyoona Msando atagombea Arusha, he have money and mvuto maana yake atagawana Kura na Lema, means CCM will win.

Kwa mara ya kwanza tunaweza kuona analytical and calculated political campaign, sababu ya scarcity of resources nadhani ACT watajikita sehemu ambazo wana chance.

Nimependa uchambuzi wako,ila asikudanganye mtu ZITTO hapendwi kiasi hicho kigoma,na kwa taarifa tu angekuwa na uhakika wa kushinda kaskazini asingeenda kuaga.ACT wakifanya siasa za kushindana na chadema watapotezwa mazima.bora wazingatie ushauri wako
 
Sioni kama kuna namna ya kukifanya chama cha ACT kutokua na mzuto kwa jamii ya Tanzania hasa ukozingatia watu wa nchi hii tulivo na siasa za kufuatafuata...ni wangapi watamfuata ZZK even if amekuwa akikatishwa tamaa pamoja na kutukanwa na wafuasi wa CHADEMA wengine bila kujua wala kufahamu chanzo husika cha yeye kufikia kufanywa hivo
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Kuwa tishio kwa Chadema! sio chama tawala CCM?, This is fuc...ing cheap POLITICS, i thought our main enemy,we oppositions, is CCM,definately i thought wrong!

THIS is totaly poor bloody fuc...ing bongo politics,
 
Yaani hapa ndipo akili zetu zinapooneka zina hitilafu,ACT ni chama cha upinzani au tawi la CCM???? unapima ubavu na CDM au CCM hebu fikiria mara mbili kabla hujaleta mada hapa JF
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...
 
Mashaka yangu Act ni hiyo nyota mliyoweka kwenye kadi zenu na kwenye bendera!hiyo ni nembo na utambulisho wa dini ya kiislamu.Nashauri mbadili hyo nyota ondoeni mtapata wengi

Mkuu ndo maana wanajipa moyo wa eti wanaenda kuanzia mkoa wa pwani.
 
Kama unajua hivyo kinachokuuma ni nini sasa mkuu au kwa kuwa unajijua kuwa wewe si ACT ila ni mpiga kelele wa CCM !! Sisi ngoma tunaipiga kimyakimya . Kama huyo jamaa yako angekuwa ni mashuhuri sana kuliko CHADEMA ndo angesindikizwa na wafuasi 12 wapya na tena usiku!!? ha ha ha kazi mnayo, baada ya wiki moja ACT itakuwa ndo imezikwa jumla mpaka atakapokuja mgombea urais wenu mtarajiwa.
mtasubiri sana. halafu nani kakuambia kuwa mimi ni ccm? nitake radhi tafadhali.
 
naam, bwana zitto sikia haya ninayoenda kuandika hapa. Siasa zetu katika nchi za kiafrika ni zaidi ya siasa.ujenzi wa chama si kazi ya lelemama kwanza inahitaji watu makini,pesa,mipango mkakati iliyo madhubuti na uwanja sahihi wa kufanyia siasa zenyewe.

Siasa zetu za kiafrika sio sawa na zile za nchi zilizoendelea, kwamba sera pekee zinaweza kumshawishi mtu akuunge mkono katika chama chako, hapa kwetu unajua vyama vyetu wafuasi wengi wana matarajio ya muda mfupi na wanalenga kupata jambo fulani kipindi fulani, katika muktadha huu utakuta migogoro mingi inaibuka kwenye vyama hivi ambavyo havina rasilimali za kutosha mwisho mgogoro ukikomaa utakuta chama kinakufa kifo cha kawaida, na hapa sina maana chama kifutwe kwa msajiri.

Hakika kuna matarajio uliyonayo moyoni mwako lakini hayataweza kutokea katika siasa za act maana sasa wale waliokupokea wanahitaji muda ili waanze kupishana na wewe na hapo ndio utajikuta unakuwa easy target.chama kikiyumba utakuwa unajiona unalo jukumu la kurekebisha mambo na hapo zitto utakuwa hauna amani tena moyoni utakuwa unajutia yale yaliyotokea na yanayobeba historia ya maisha yako kisiasa.

Sasa jukumu unalo tena zito,kipindi hiki unapoangalia mbele kwenye uchaguzi mkuu ujao,hakika itakuwa ni kazi ngumu mno wewe kurudi bungeni katika kipindi hicho ijapokuwa unaweza ukadhani ni rahisi lakini nataka nikwambie kwamba si rahisi maana kazi uliyonayo itakuwa kukijenga chama na si kujenga himaya yako ndani ya act,akina mwigamba naweza kusema hakuna chemistry kati yako na mwigamba na hilo litakuwa tatizo la msingi.

Mwigamba anaamini katika mawazo yake na wewe pia, kamwe hamtaweza ku compromise pindi mkitofautiana katika harakati zenu mlizo anza.

Safari hii uliyoianza ni tofauti kabisa na ile uliyoianza pale ulipokua na umri wa miaka 16. Kipindi hicho ulipata mafanikio mengi ndani ya siasa na nje ya siasa, ulipewa nafasi na chama chako kutenda majukumu makubwa,lkn safari hii ukiwa na umri wa 39 umeanza safari mpya yenye mashaka mengi.
act itakuwa kimbilio la wengi
jambo kama hili ndilo lililoiangusha kanu
kwa siasa za kiswahili mpaka sasa hakuna aijuae kesho
ngumu sana kutabiri
pengine nchi itaangukia mikononi
kwa watu tusiowafahamu.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Unaanzisha chama kwa kutegemea wafadhili? Akili mufilisi kama za jk anayeamini Tz itaendelea kwa kutembeza bakuli.
 
Inaonekana unatumiwa na CCM, Kwa nini useme ACT itakuwa tishio kwa CHADEMA? Unatakiwa kujenga hoja. Kwani kuna mashindano ya vyama?
Ipo hivi mkuu, ACT itakuja kuwa tishio kwa CDM kama chama kikuu cha upinzani kwa Tanzania Bara, na vivo hivyo kwa chama tawala CCM
 
Back
Top Bottom