chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,359
- 27,739
Simu ya mkononi iliyokuwa imeibwa ilituma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo kuonyesha ndiye mmiliki wake.
Polisi katika eneo la Essex nchini Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo aina ya HTC iliyoibiwa kutoka kwa koti la mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea nyumbani.
Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye simu hiyo ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza nambari ya siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.
Msemaji wa Polisi alisema simu hiyo ilimpiga picha mwanaume huyo alipojaribu kuingiza nambari hiyo bila kufanikiwa.
Barua Pepe ya mwanafunzi huyo ilituma ujumbe kwa polisi kuwaarifu kuhusu wizi huo.
Mshirikishe na mwenzio habari hii.
Source; BBC Swahili.