Tahadhari kwa wazazi wa watoto wa Panya Road, nina bastola

Hawezi mtu anamkaribia baba/mama yangu kumpiga panga la kichwa mimi nimpige risasi ya mguu.. ujinga huo siwezi mkuu
Ukiua uanze kwenda lumande, ukimvunja mguu ushaidi na watatajana, hii ya wafungwa kupigwa risasi miguu nilimuulizaga swali anko wangu wanawafanyaje wafungwa wakiona wanakimbia.
 
Habari zenu wakuu,

Nina hofu kubwa sana juu ya wazazi wangu na hawa vijana wavamizi mimi naishi Masaki na wazazi wangu wanaishi Mbezi kwa hizi habari za uvamizi nineona nyumba yangu nimuachie mlinzi na mimi na familia yangu tuende Mbezi kwa ajili ya kuwaimarishia wazazi wangu wapendwa ulinzi.

Sasa tahadhari kwa hawa vijana wavamizi bila shaka wao wamejitolea kufa sasa naomba nitoe onyo kwa wazazi wao sitarudisha moyo wangu nyuma nitakapogundua wametuvamia wallah nitawapiga bastola yaani nitaua nawahakikishia sito hofia kesi wala kupanda mahakamani.

Nawapenda sana wazazi wangu na nadhani hakuna asiyewapenda wazazi wake na kwa hilo sitahofia kumwaga damu ya atayejaribu kuruka katika fance ya wazee wangu kwa kuja kujaribu kukaba kuwakata mapanga na kuwapora au kuwaibia nawahaidi nitaua mtoto wa mtu.

Baada ya tukio ndio mtakuja kunilaumu wasifieni tu ila mtu atakayejaribu kuja kuichezea familia yangu ntammwaga ubongo ninyi endeleeni kuwachekea tu.
Broo, kwa kuweka hii jinai kwenye maandishi ni ushahidi tosha dhidi. Hatuombi ufike huko,lakini yakitokea ya kutokea,
Hapo utakuwa umeua kwa kudhamiria na sio kwa kujihami. Hivyo Adhabu ya kunyongwa hadi ufe itakuwa ni halali yako
 
Panya hawana smart phone we wafate vijiweni mwao, au wape taarifa wazazi wao
 
Mkuu yaani ikifika usiku watu wote wanalala hapa kwa mzee nabaki macho mpaka hasubuhi kwa hofu kuwa watapita ila nakuhakikishia ukisikia mahala wamekatiza na wamepigwa bastola rudi tena hapa kuniulizia nikuadithie movie lilivyokuwa mkuu .. nakuhakikishia watajijutia kuingia chaka
Mwizi ni shetani,wizi ni Roho ukikesha unawasubiri awaji, uthibisho chukua bastola fully loaded tembea mida ya wezi Katu huwezi kutana nao hata utembee mwezi mzima huwezi kukutana na mwizi au kibaka.Wale ni kama upepo uzuka kama upepo kwa kuongozwa na roho ya wizi au pepo la wizi ndio uwaongoza kufanikisha uhalifu.
Pia waganga Wana mchango Mkubwa Sana na uwepo wa wezi, Hakuna mwizi asiye na mganga,Ili kutokomeza wezi ilifaa Jamii iwashughulikie waganga hawa ndio uwapa wezi nguvu.
 
Ukiua uanze kwenda lumande, ukimvunja mguu ushaidi na watatajana, hii ya wafungwa kupigwa risasi miguu nilimuulizaga swali anko wangu wanawafanyaje wafungwa wakiona wanakimbia.
Kuua kwa self defense sio kosa,hasa kama amekuja kwenye site yako. Pia damu ya mwizi, mchawi hazina laana sababu wale ni agent wa kuzimu.
 
Kitu kama hiyo
Screenshot_20220503-185828_Samsung%20Internet.jpg
 
ungewaeleleza ni nyumba gani ili wasije fanya mistake wakaja au weka announcement nje ili wasije kukulaumu
Tangazo tangazo nyumba hii inalindwa kwa bastola, panya rodi ukijichanganya nakufumua ubongo... Sitaniii...
 
Kwann mnawaza kuua innocent kids ?
Hebu waulize Broo!!!
Hao si ndio watoto wa wale wanaoitwa wanyonge, waliokosa elimu bora na malezi na mlo wa siku.
Ingependeza pia kama tungepiga sana kelele humu kutaka damu za wale majambazi/wanasiasa waliotuibia zile trillioni 6 alizoainisha CAG.
Sitetei uhalifu ila nachukia double standards zetu. Watoto watukutu wanaopora watu machungwa na simu mitaani baada ya kuibiwa future yao na wanasiasa na mafisadi wengine wa mali za umma, tunataka wahukumiwe kifo au wakafundishwe ujambazi wa hali ya juu zaidi huko magerezani, badala ya kuwapeleka kwenye "Vyuo vya Mafunzo" mbali na vishawishi vya mijini na nyumbani, wafundishwe tabia nzuri, maadili na stadi za maisha zitakazowasaidia kujikimu na kuwa raia na wapiga kura wazuri.
 
Ila watu wa dsm kuna mahali mnafeli sana. Yaani Leo mnavamiwa mnasubiri kutangazwa kwenye TV tu na mapicha mengi. Nina uhakika hao vijana wangefanya hayo huku mikoani hakika hata kwenye TV msingewaona. Kuna watu majasiri huku sio mchezo. Ingepigwa mbiu tu halafu mngeona ushirikiano wa wanajamii. Tatizo lenu huko hata kusalimiana tu issue. Mnajifanya mpo busy na mbele saaana kumbe hamna kitu.
Mkuu Kuna kipindi nilikuwa mikoa ya ziwa magharibi Kigoma hukoo... Wafugaji wakawa wamevamia misitu ya hifadhi na mifugo yao kibao... Yaani Kuwatoa huko msituni lazima watu wa maliasili wajipange na bunduki vinginevyo ni balaa. Sijaona watu watu courageous kama hao jamaa yaani ili uwakamate lazima ujipange haswa maana na magobole wanayo
 
Ila watu wa dsm kuna mahali mnafeli sana. Yaani Leo mnavamiwa mnasubiri kutangazwa kwenye TV tu na mapicha mengi. Nina uhakika hao vijana wangefanya hayo huku mikoani hakika hata kwenye TV msingewaona. Kuna watu majasiri huku sio mchezo. Ingepigwa mbiu tu halafu mngeona ushirikiano wa wanajamii. Tatizo lenu huko hata kusalimiana tu issue. Mnajifanya mpo busy na mbele saaana kumbe hamna kitu.
Hivi wale vijana wa taleza, walikua wanakula mnapokula, tena hata bila kunawa mliwafanya nini.
 
Back
Top Bottom