andate
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 2,651
- 1,024
NAWALETEA KAMA ILIVYO . . . . .
WIZI MPYA WA MITANDAONI . . . . .
Haswaaaaa kwa wale wapendao kwenda internet cafe . . .
Yaani ukiingia internet cafe halafu nyuma ya computer ukakuta kuna ka-PIN keusi kamewekwa kwenye kebo ya kuchomekea Keyboard au Mouse ya computer, basi USITHUBUTU KAMWE kutumia hiyo PC. Narudia . . . . USITHUBUTU!!
Hako kadude keusi ni kama ka-memory fulani hivi ambako kanaweza ku-save data zote utakazotumia wakati unafungua mtandao au internet, mfano passwords za emails, facebook, na hata data zote za banking utakazofanya mtandaoni.
MSIJE KUSEMA HAMKUJUA . . . .
Share kwa wenzako ili nao wajue . . . .
![]()
Hivi ni vya PS2 keyboard.
Hii hapa chini ni ya USB keyboard
Pia kuna software ambazo unainstall kwenye computer ambazo zina-record keystrokes zote huna haja ya kuchomeka chochote cha ziada.
Ili kuepuka kuibiwa data zako za siri, ni bora kutumia computer yako mwenyewe.