Safi sana mtambuzi. Endelea kupona haraka ili tuzidi kufaidi hii mambo. Sasa binam yako anaendeleaje baada ya kuibiwa mme na beki tatu?
Kipipi chondechonde wanaume hatuko kama unavyofikiria!
Kutokana na ukweli kua maisha yamebadilika sana in every level hivyo kupanda kwa gharama kila sehemu ugusayo hasa ukitaka kitu quality ili kupata huduma ya uhakika iwe education, malazi/makazi, matibabu, chakula, - facts zinazofanya wenza wote wawili mujishulishe hivyo kama mna watoto mnamtafuta binti wa kuwasaidia… Tatizo ndo linakuja hapo.. NDIO akina dada tuko busy saaana lakini jamani are we so busy to the extent huwezi nyanyua kidole hata kidogo??? – Nauliza/nasema hivi in the sense kua NDIO Msichana wako anakupa support katika kuendesha/kuangalia nyumba lakini je kuna haja ya kumpa full access kwa mumeo… kwa mtazamo wangu wadada/mama wengine huyataka mambo kama haya ya kwenye thread hii kuwatokea tokana na the way anendesha mambo yao katika ndoa yake….
Kwanini umpe msichana wako FULL ACCESS kwa mumeo???? Ladies if you love your man and proud of him at all cost minimize vitu/mambo yawezao kumshawishi (akina mama tuna njia tofauti hii ni kwa wale wataoona I am right) … Kama Speaker alivyosema katika moja ya post.. "Never let your man's mind wander .... " Hivyo akina dada/mama tujiulize je wewe personaly umempa msichana wako (maarufu kwa house girl) Full Acces OR No Access kwa mumeo???
FULL ACCESS
Anaingia chumbani kwenu (eti kufanya usafi…lol!) na worse enough yeye ndo anatandika kitanda ambacho wewe na hubby mnajimwaya; Anapika mwenyewe (si mbaya sana) but worse enough yeye ndo anaandaa chakula na kumkaribisha hubby mezani..; Anampokea mizigo akifika – in other words mumeo anatangulia kufika kabla yako kila siku (bad news - kwa wale ambao iko nje ya uwezo …😉; Ndio afue nguo (for maybe you have no time) but ziwahi hakuna haja ya hubby kuulizia soksi ikowapi which at the end of the day atamfuata binti kumuuliza mana anajua wazi hufui wewe…. Etc.
NO ACCESS
Huna nafasi ya kupika, but unahakikisha umekagua chakula, umeandaa mwenyewe na umemkaribisha mwenyewe mezani, Ndio nguo hafui but at least anahakiki zimetakata zimenyoshwa vizuri na zinarudishwa room kabla hubby hajazimiss..; Ana hakikisha kila mumewe anpokuwepo nyumbani yupo tayari home' labda in rare cases plus kujitahidi kurudi kabla ya the hubby… etc. Kwa ufupi kutojenga mazingira ya wao kuwa karibu…. House girl awe karibu na watoto…. BUT not the husband
Note; Wanaume hawalindiki hasa akiwa na nia but at least ikitokea utasema "I tried my best but he is just a Ba****"
Ni kweli kabisa nyie wanaume hamna jema jamani......ndio maana mwanzo sikutaka kusema kitu maana najionea tabu tu. Hata mkeo akufanyie nini kama haujastaaribika ndio basi tena hata mdogo wa mkeo kutembea nae huoni shida licha ya HG!!!!!
Kwakweli kilichobaki ni kila mwanamke apige goti kumuombea mumewe maana mmmhhhh.....kama ni mtihani tunao.
Mara nyingi wanawake tunajisahau saana na kuona kana kwamba mumeo aweza vutiwa tu na mwanamke huko nje.... IMO house gal ni binti wa kumuogopa saana na kua nae makini ni kiasi gani awe karibu na mumeo.... Nimewahi zungumzia hili kwenye thread ya First Lady, the below ni copy and paste from that thread.
Source: Thread ya First Lady - LINK
House girl hufanya kazi nyingi kuliko muolewaji……….. najua mtadai kuwa huo ni wajibu wao kwa sababu ya kijimshahara cha elfu thelathini mnachowalipa……lol…….. amkeni nyie acheni ujinga wajibikeni ili mlinde ndoa zenu. Mwanaume hutazama nani anawajibika ndani ya nyumba kuliko mwingine………. Yaani hata chai ya jioni ya mumeo atayarishe house girl? Mwanaume hupenda mtu anaye m-handle na kum-care kwa kila jambo, na hata kama wewe hufanyi, basi fuatilia kuhakikisha linafanyika kwa usahihi.
Ni kweli kabisa nyie wanaume hamna jema jamani......ndio maana mwanzo sikutaka kusema kitu maana najionea tabu tu. Hata mkeo akufanyie nini kama haujastaaribika ndio basi tena hata mdogo wa mkeo kutembea nae huoni shida licha ya HG!!!!!
Kwakweli kilichobaki ni kila mwanamke apige goti kumuombea mumewe maana mmmhhhh.....kama ni mtihani tunao.
Dah Mtambuzi Baba karibu tena. Naona umepona Baba tunamshukuru MUNGU kwa hilo.
Hii mada yako ya leo ....................Dah!
Hapo kwenye red: Unataka kunambia mwanaume anaoa kwa kuwa anataka mtu wa kuwajibika? Kumpikia, kumfulia n'k? Kama ni hivyo am sorry naombeni niprolong likizo yangu tafadhalini!!
Mtambuzi eti tuwajibike kwa kufanya kazi kwa kuwa mwanaume anaangalia nani anayefanya kazi kuliko mwingine ndani ya nyumba????!! Oh Puleeeez Mtambuzi Give me a break eh!!
Hapo kwenye Blue hebu nifafanulie Mdada wa Kazi anam-care na kum-handle vipi Mbu wangu??
kumbe ulishawahi kutoa darasa zuri namna hii hapo nyuma...............ushanirahsishia kazi ya kumshauri binamu yangu, haa ni ku-copy na ku-pesti tu, kazi kwisha..................
Si ndo hapo; kwa hiyo nkitoka job nianze kuwajibika mpaka saa tano usiku ili nishindane na hosegirl kuchapa kazi asije nizidi kete; kwa mtaji huo atembee nae tu mradi nisiwashike.