Tahadhari kwa walaji wa Pweza

Jamani mada mbona imehama? Hivi mnajua wanakoandaliwa hawa samaki hadi wakufikie hapo njiani? Tunalishwa maradhi wandugu
 

Huwa sinunui pweza wa Barafu nanunua fresh na najua yupi fresh na yupi sio fresh na nafahamu hata aina ya pweza na mwambao aliovuliwa!!..pale feri huwa wanakuja wa leo leo na nawajua vizuri na ndio maana huwa sihangaiki sana kuwapiga nabeba naenda kuwaosha vizuri nawaweka kwenye friza then baada ya siku mbili unakata tuu vipande. Kumbuka mimi sio mwenyeji tu wa maeneo yenye pweza wengi ila pia mimi ni mvuvi mstaafu wa pweza!..inaonekana wewe una idea kubwa na pweza ila hapa kwangu unaweza jifunza kitu kuhusu pweza usinibeze fanya hivyo nilivyokuambia lazima unikubali!
 

Ha ha ha.....ntafanyia kazi hili.....hapana mimi si tu kuwa nna idea....ni mvuvi pia...lkn km wasemavyo bahari pana kuna la huku halijulikani kule,thanks!
 
Kula vzr fanya mapenz kwa afya(mara mbili kwa wiki),fanya mazoez ya kutosha uone kama utapungukiwa nguvu ....kula pweza kwa hamu na kwa afya otherwise hvyo vpande vya mitaan na supu za mitaan ni maradh tu nothing else
 
mfafanulie vizuri kuhusu aliyepigwa, sio kupikwa
Mkuu moja ya matayarisho ya pweza ni kumchezesha judo,kumpa kichapo kikali akiwa amekufa la sivyo haliki atagangamaa na akipikwa itakuwa afadhali utafune soli ya kiatu chako badala ya pweza!
 

Uko sawA mkuu mi nakumbuka kipindi niko mtwara nilikua nikimtengeza pweza wakati namchemsha nilikua naweka ma sukari kidogo sana ili alainike.
 

Aisee!!!!Noted with thanks
 
Mkuu moja ya matayarisho ya pweza ni kumchezesha judo,kumpa kichapo kikali akiwa amekufa la sivyo haliki atagangamaa na akipikwa itakuwa afadhali utafune soli ya kiatu chako badala ya pweza!
hahahaaa... Duh! Watu wavumbuzi kweli. Aliyevumbua hiyo staili ya kupiga sijui alikuwa anawaza nini
 
Ukimuona Pweza akiwa hai sijui hata kama utatamani kumla, kumbe Pweza anaongeza nguvu za kiume? Hii ni kweli au Iman tu?
 
Wakifunikwa kwa nailoni ndo saafi, ndulele husimama kama nguzo ya Tanesco siku mbili mfululizo!
 

Shida si wakati wa kuwapika tabu ni wakati wa kuserv maana hapo ndo mnapishana na nzi,, ila kama wako jikoni hata kama wako wazi si shida maana hilo joto lake hakuna bacteria ata suvive
 
mimi ni mlaji mzuri wa pweza kila jioni, ila si kweli kuwa wanaongeza nguvu, uwezo wa uwanja wa seremala ni saikolojia yako, mfumo wa vyakula, mazoezi. ila hizo theory zingine za pweza, nyagi, zanzi mhhhhh. imani.
 
akina dada wakishaona mume au boyfriend wake yuko busy na pweza, wanahaha mno, sijui wanaogopa gwaride
 

Duuuuh Kwel noma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…