Ngoja waje watetezi wa marijali bandia hapa uone povu la kutosha!!hili jambo la nguvu za kiume kila kukicha ni mtihani,tatizo ni ulaji wa ovyo na kila mtu sasa hivi amekuwa doctor wa nguvu za kiume.Hebu wenye hii taaluma tunaomba mtoe darasa la kutosha.
Pweza wanasifika kwa kuongeza nguvu za kiume, lakini kwa upikaji huu ninaouona ni wazi kuwa nguvu zetu ziko mashakani. Wakati wa kuwaandaa, vijana hawa huwafunika kwa nailoni wakiwa jikoni hadi waive. Kuna usalama hapo? Kazi kwenu walaji wa pweza mnaosaka nguvu za ziada
Kwenye freezer anakaa muda gani akiwa mbichi bila kuharibika s.crony
mfafanulie vizuri kuhusu aliyepigwa, sio kupikwaKm freezer yako ni nzuri anakaa muda mrefu tu...mi naweka wa2/3 natumia mwezi mzima,lkn kwa Tanesco yetu hii na kwa vyakula vya baharini unashauriwa kutumia haraka mara baada tu ya kununua kuepuka food poisoning nk.Jaribu kutayarisha hii kitu utakuja niambia hapa hapa.hakikisha unanunua aliyepigwa tayari jaribu kuuliza kabla hujanunua....
Pweza wa vipande barabarani hana faida yoyote zaidi ya kukuletea maradhi.....hakuna nguvu yoyote utakayoipata hapo.Unataka msaada wa mawazo,nenda feri nunua pweza wako 1kg ni km buku 4-5 hivi.....fika nae nyumbani muoshe vizuri kwanza kwa maji ya kawaida,pili maji ya moto huwa anakuwa na michanga sana mikiani.weka jikoni usiweke maji kwanza mpaka akaushe maji yake mwenyewe,kisha weka maji kwa supu yako,tupia kitunguu kiasi kuongeza hamu na km una kitunguu saum kiasi ni bora chemsha km dk30.Hii ni zaidi ya "mkuyati" hutotumia Viagra tena!