Tahadhari: Kuweni makini sana leo na barabara zote kutoka uwanja wa Taifa baada ya mpira kuisha

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,217
Nimekuja mapema asubuhi kuwajuza tu dada zangu,kaka zangu,ila hapa hasa wanawake.

Leo watani wa jadi wapo uwanja wa Taifa,mpira hujaza watu wengi wa kila aina,watumiaji wa barabara ya Chang'ombe .Muwe makini na uporaji utaokao fanyika jioni baada ya mpira kuisha.

Kwani kuna makundi ya vijana kutoka Keko, Magomen na Temeke hufanya uporaji barabarani kana kwamba wanashangilia ushindi wa Timu zao.

Mnaotumia bajaji, Mandela road, Chang'ombe road na Kilwa road leo mpumzike wakati wa jioni hasa nyie dada zangu.

Kama una misimu mikubwa acha kwenu leo sio siku nzuri kabisa kutakua na uporaji mkubwa mno.

Dada zangu mnaotembeaga na masimu yenu jioni mkiwa hamna wasiwasi leo acheni simu zenu nyumbani.Ukipata ujumbe huu msambazie na mwenzako.

ukiwa kwenye gari au unatembea kwa miguu gafla ukaona kundi kubwa linashangilia kaa mbali kabisa na umati huo,kama ni gari basi funga vioo vyako,hao wanaitwa safisha safisha.

Ni mimi zubedayo_mchuzi mzee wa kutembea umbali mrefu.
 
Na hata wenye magari kuhakikisha umeweka lock milango yote...Hwa jamaa ukiwa kwenye foleni akikuchek umekaa kizembe zembe anafungua mlango anaingia kwenye gari ghafla unashangaa umewekwa chini ya ulinzi huku umeshikiwa bonge la kisu...Wanachukua zao wanashuka ukiwa kwenye line hap hapo...Hiyo wanaiita kimya kimya..
 
2006 niliporwa simu yangu hapo aina ya nokia (enzi hizo) na mateja wakati wa kusubiri kuingia uwanja wa taifa wa zamani kushuhudia mechi ya aina hiyo. Tangu hapo simu nilikua naacha chuo. Ile kukaa foleni huku tumejazana jamaa wakaniotea.
 
yule kamanda polisi wa dar juzi kasema atamwaga askari wengi na wakutosha na ole wao wafanye vurugu, ana akasema mpira ukiisha muende nyumbani akuna kukaa makundi makundi sasa sijui ataweza? ......... asante kwa ushauri lakini
 
Kwa hiyo tukae tukijua kabisa nchi haina ulinzi.......?....
Cc @kitwanga......
mkuu preta, tmk na vitongoji vyake serikali isipokuja na njia mbadala ni aibu kwa siku za usoni hawa watoto wanaopora ni wanafunzi wa sekondari na shule ya msingi wadogo sana,na wanakua wengi mno, kama hawa wanaoiba keko na tmk yote wanafahamika mpk majumbani kwao,ila kulindana tu.
 
yule kamanda polisi wa dar juzi .... kasema mpira ukiisha muende nyumbani akuna kukaa makundi makundi
Mpira ukiisha na timu yako imefungwa, lazima ujiliwaze kwa kubaki kundini na wenzako. Yaani nikimbilie kuondoka halafu kwenye madaladala nikutane na mashabiki wa Simba waanze kunitania!
 
Sasa tutapigaje selfie tukienda na Nokia torch
ukimaliza kutwanga photo na kurusha fb,wenyewe nayo wanaichukua,uporaji unaofanyika ni ule wa barabarani watu wanapita wanaimba kama wanashangilia sasa wakikuweka kati maana yake utasachiwa mpk kyupi,ila kama una usafiri wako ukitoka ndani ya gari funga vioo,hakuna atakae kushambulia,ila kama mtajazana kwenye bajaji mnazungukwa kama nanyi ni wachovu mnapigwa makofi na watoto hao then wanachukua simu hizo.
 
Mpira ukiisha na timu yako imefungwa, lazima ujiliwaze kwa kubaki kundini na wenzako. Yaani nikimbilie kuondoka halafu kwenye madaladala nikutane na mashabiki wa Simba waanze kunitania!
mimi sijui mtafanyaje aisee? ila kasema ulinzi utakuwa nadhani sasa yale magari ya machozi yale yaliyoletwa kwa ajili ya uchaguzi watayafanyia mazoezi kwenu
 
mimi sijui mtafanyaje aisee? ila kasema ulinzi utakuwa nadhani sasa yale magari ya machozi yale yaliyoletwa kwa ajili ya uchaguzi watayafanyia mazoezi kwenu
nitatoa ulinzi special kwako,ukiwa taifa nijulishe niwe bodi gadi kama jet lii......
 
ukimaliza kutwanga photo na kurusha fb,wenyewe nayo wanaichukua,uporaji unaofanyika ni ule wa barabarani watu wanapita wanaimba kama wanashangilia sasa wakikuweka kati maana yake utasachiwa mpk kyupi,ila kama una usafiri wako ukitoka ndani ya gari funga vioo,hakuna atakae kushambulia,ila kama mtajazana kwenye bajaji mnazungukwa kama nanyi ni wachovu mnapigwa makofi na watoto hao then wanachukua simu hizo.
Umesomeka mkuu
 
Back
Top Bottom