mama klareee
Member
- Jul 19, 2017
- 26
- 138
Mara nyingi nilikuwa napita hapo nimewahama.
.....Hapo Arusha vituo navyoweka mafuta ni kwenye vituo vya Total, Oryx na Puma.
Hiyo nayo juzi imemkuta rafiki yangu Dodoma hajaniambia ni sheli gani lakini inaonekana kuna mchezo unaoendelea kwa wauza mafuta wa sheli.Ahsante sana mkuu kwa tahadhari.
Juzikati niliweka mafuta ya shs 20,000 baada ya kutoka Tripple A, break ya kwanza ilikuwa Babylon Club, ila kabla ya kupark nikaona kama kuna dalili za mafuta kuisha, ikabidi nifanye kucheck upya ikiwa ni pamoja na kwenda pale Mount Meru Petroleum Meru Posta.
Sikufanikiwa kufika kwani niliishiwa mafuta pale Benson & Company. Later niligundua kuwa hakukuwa na mafuta kwenye gari (hapo dumu la mafuta na toyo ya kuyafuata mafuta petrol station viliokoa jahazi).
Baada ya kuweka upya mafuta (na kutoa upepo kwenye fuel system) nikarudi tena kule tTriple A na kuwapigia kelele pale nilipokuwa nimeweka mafuta earlier (Triple A) ndipo nilipofuatwa na madereva taxi na toyo wakanituliza kuwa ndio tabia ya pale ila nisiwataje.
Tabia kama hizi ni mbaya sana na ni vema vyombo vinavyohusika vikafuatilia kwa siri na wakigundua kuwa tunaibiwa wakifungie kituo hicho na vituo vyenye tabia hizo kwani ndio uwajibikaji wa jumla kwani waajiri ndio wanaowapa wafanyakazi/mfanyakazi nafasi za kutekeleza majukumu ya kazi zake.
Kwa kifupi, mwajiri ndiye nayebeba dhamana ya mfanyakazi wake.
Hii tabia ikomeshwe nchi nzima kwa waathirika kuifichuliwa pindi wafanyavyo tukio kama hili.