Tahadhari kali kwa nyote mlio na magari binafsi; chunga sana na waambie wengine!

Kweli uendeshaji gari ktk highway una changamoto nyingi sana. Madereva lazima tuzitii sheria za barabarani,ila tusiwe ving'ang'anizi kwa kutochukua tahadhari kwa wavunjifu wa sheria barabarani kwa sababu tu eti sheria ipo upande wako kwa wakati huo. Lazima ujari usalama wako kwanza,mpishe uokoe roho yako na za wengine pia.
 
Hii habari si mara yangu ya kwanza kuisikia.
Sidhani kwamba speedometer hutengenezwa bila kuzingatia ukubwa/udogo wa gurudumu.

Hio habari sio ya ukweli kabisa

Speedometer inasoma speed ya gari...Ikiwa ni 80 ni 80 kwenye magari ya aina zote......ila ukiniambia kwa sababu ya uzito wa basi 80 ni spidi ya kawaida hapo ntakuelewa
 
Kwenye kuzoe spidi ndo umenikamata kabisa, na hii si kwa gari tu na hata kwa waendesha pikipiki. Niliwahi kuendesha pikipiki kutoka Morogoro Mjini kwenda Dumila kwa dakika 30. Mimi nilikuwa naona natembea mwendo wa kawaida. Nilibahatika kutambua hili kwa kurekodi muda nilioanza safari. Wakati wa kurudi pikipiki niliipakia kwenye roli... Sikutaka kuendesha tena kurudi Morogoro Mjini na usafiri huo baada ya kukokotoa speed niliyotembea nayo kwenda Dumila.

Hakika wewe ulipanga kukimbia hizo speed za kufa!!! kama ulirecord hadi muda unaoanza ili ujue umetumia muda gani!!! Kwa sababu kama ni safari yenye lengo la kufika tu hakukua na sababu ya yote hayo. La msingi ulijitambua kwamba ulichokifanya kilikua si kizuri ukabadilika.
 
Hakika wewe ulipanga kukimbia hizo speed za kufa!!! kama ulirecord hadi muda unaoanza ili ujue umetumia muda gani!!! Kwa sababu kama ni safari yenye lengo la kufika tu hakukua na sababu ya yote hayo. La msingi ulijitambua kwamba ulichokifanya kilikua si kizuri ukabadilika.
Mkuu ilikuwa mara yangu ya kwanza kuendesha pikipiki kutoka Morogoro kwenda Dumila...ndiyo hasa lengo la kurekodi muda ili siku nyingine niweze kupanga muda wa safari kwa uhakika zaidi.
 
Uliyetoa hii thread wewe ni mtu wa muhimu sana unafaa kuwa mshauri kwa mambo haya ya uendeshaji wa vyombo vya moto, ni moja kati ya thread zenye akili hapa kwenye jamvi, big up......saluteeeeeeeeeeeee!!!
 
Uliyetoa hii thread wewe ni mtu wa muhimu sana unafaa kuwa mshauri kwa mambo haya ya uendeshaji wa vyombo vya moto, ni moja kati ya thread zenye akili hapa kwenye jamvi, big up......saluteeeeeeeeeeeee!!!

Nimefuatilia uzi huu kwa makani sana. Hongera sana mkuu mwasisi.
 
Mzee hii ni shule nzuri sana umetoa ila naongezea kwamba kama unajua utaendesha gari kwa zaidi ya saa tano au sita jaribu kulala usingizi wa kutosha maana wengine hulala saa sita au saba usiku tena wakinywa pombe na asubuhi anachukua gari kwenda mwendo mrefu matokeo yake anaanza kusinzia barabarani na matokeo yake anafanya ajali mbaya.
 
Uliyetoa hii thread wewe ni mtu wa muhimu sana unafaa kuwa mshauri kwa mambo haya ya uendeshaji wa vyombo vya moto, ni moja kati ya thread zenye akili hapa kwenye jamvi, big up......saluteeeeeeeeeeeee!!!

Ahsante sana Mkuu. Sikujua kama nitapata appreciation kiasi hiki. Nimekuwa humbled, sana.
 
Poa sana ila naomba kuelewa overdrive inavyotumika na ikawa inawaka ktk dashboard yako ndo iko on au of


Mkuu, nilishajibu swali la overdrive hapo nyuma, hebu angalia hapa chini;

Overdrive inatumika ili kuifanya gari ikupe namna fulani ya gia za juu na kama vile gia fulani ya ziada unapokuwa kwenye spidi za juu. Tuseme gari yako ya Automatic ikiwa na gia 6, Overdrive ni kama inakupeleka gia za 5,6 na namna fulani kama vile gia ya 7. Sasa mara nyingi, wengi huwa tunaendesha gari likiwa tayari kwenye Overdrive toka tunapoondoka (taa ya OD inakuwa haiwaki pale kwenye dashboard), yaani hatuweki Overdrive off. Hilo sio tatizo. Ina maana kwamba, unakuwa umeipa gari uamuzi wa kukuweka kwenye gia za chini ukiwa mwendo mdogo na zile za juu na ya ziada kila ikifikia spidi ya juu, hasa kuanzia 70km/hr. Hilo ni nzuri, kwa sababu gari itakapoingia kwenye Overdrive ina maana inapunguza mzunguko wa injini inapofikia spidi ya juu, na hii inafanya gari itumie mafuta kidogo, na hata muungurumo unakuwa wa chini.

Lakini sasa, ukiondoa Overdrive kwa kui-switch off (yaani taa ya OD inakuwa ON), ni sawa na kuiambia gari nataka usinipeleke kwenye zile gia za ziada za juu (kama ya tano, sita na saba) kwa sababu nataka injini inipe nguvu zaidi, na hasa pale ninapotaka ku-accelerate haraka, kama ku-overtake.

Kwa lugha nyepesi, ikiwa gari iko kwenye Overdrive, inaweza kukupeleka kwenye gia za juu wakati wewe bado unataka injini ikupe nguvu au acceleration ya haraka, ambapo unaweza kukuta gari haichanganyi vizuri wakati unataka ku-overtake haraka. Ni sawa na ukiwa na gari la manual, urudi gia namba tatu wakati wa ku-overtake, lakini wakati uko katikati ya ku-overtake ubadili gia toka gia ya tatu kwenda ya tano. Sasa ukiweka Overdrive off, ni sawa na unaiambia gari isije ikaingiza gia toka ya tatu kwenda ya tano kwa sabau tu imehisi tayari umefikia spidi ya juu kwa hiyo ikakuchagulia gia za Overdrive hata wakati bado unahitaji injini ikupe power ya ku-overtake.
Ila ni vizuri ukisha overtake urudishe gari kwenye Overdrive.

Sasa, kuna wakati ni vizuri tu kui-switch Overdrive off muda wote. Kwa mfano gari ni automatic na limebeba mzigo mkubwa. Au kwa mfano unaendesha gari katika barabara mbaya ambapo hata kufika spidi ya 80km/hr ni shida, basi ni vema ku-switch overdrive off. Na pia ukiwa na mzigo mkubwa au hata bila mzigo unateremka mteremko mkali au mteremko kwenye barabara mbaya, au ya matope, ni vema kutoa Overdrive, na hata kuirudisha gia toka D kwenda 2. Ukiacha gari kwenye Overdrive inaweza ikafikia mahali ikawa kama unashuka mteremko mkali na gari ya manual wakati uko gia ya tano au sita, hata kama mwendo wako sio mkali. Gari inakuwa nyepesi sana, na inakuwa haina breki ya injini.

Kwa mfano, basi au lori ambalo lina gia automatic, dereva kushuka Kitonga wakati yuko kwenye Overdrive ni kutafuta ajali mbaya. Ina maana gari itakuwa inashuka mteremko na wewe unaipunguza mwendo kwa kutumia breki peke yake, bila injini kusaidia kupunguza spidi ya gari. Matokeo ni kwamba breki zitaanza kupata moto sana na kuungua (utasikia harufu mbaya sana kama vile clutch inaungua) na inaweza hata kutokea breki zikafeli. Ukigusa rim ya tairi utakuta ina mto vibaya sana na tairi inaweza kupasuka kwa kuyeyuka!

Kuna sehemu fulani kule Mbeya kwenda Tukuyu mteremko unaitwa Uwanja wa Ndege, ukiwa na lori au basi automatic ukashusha nalo ule mteremko ukiwa kwenye Overdrive, unaweza ukakuta inafikia breki hazishiki tena, zimeungua! Kushuka mteremoko kama ule na lori au basi liko kwenye Overdrive ni sawa na kushuka mteremko ukiwa na lori au basi la gia manual wakati uko gia ya sita, huku unapunguza spidi kwa breki!!!

Kwa loli au basi la automatic, unaposhuka milima ya Lushoto au Kitonga au Uwanja wa Ndege (kwenda kule Tukuyu) lazima u-switch off Overdrive, na hata zaidi uitoe gari kwenye D na kwenda kwenye 2.

Nadhani nimekusaidia kukuelewesha suala la Overdrive mkuu.

Katika hali ya kawaida ni sawa kuacha gari kwenye OD wakati wote (taa ya O/D iwe off, haiwaki). Unaweza kuiondoa kwa sababu nilizotaja hapo juu.

Kumbuka:

Overdrive off - taa ya OD inawaka kwenye dashboard (ni vema katika mazingira yaliyotajwa hapo juu, lakini si vizuri ukiwa kwenye spidi za juu)
Overdrive on - taa ya OD haiwaki kwenye dashboard (ni vema katika spidi za juu)
 
Endesha gari ukichoka paki pembeni osha USO kwa maji,endesha gari ukifuangua vioo inapunguza kusinzia.
Na si kila mtu anauwezo wa ku endesha barabarani kuu tafadhali tafuta dereva mzoefu wa njia hizo!
 
hizo akili lzm utakua ni chadema.

Ha ha ha! Mkuu Yugo, acha kunichonganisha. Angalia signature yangu utaona niko wapi - sina upande wowote. Mie bwana Chama changu ni Tanzania, na wote nyie wengine, muwe Chadema, CCM, TLP, CUF, NCCR, Mzalendo sijui, nk, wote ndugu zangu. Wazo lolote au kichwa chochote kizuri juu ya maendeleo ya Tanzania nalikumbatia kwa moyo wote - bila kujali linatolewa na nani. Nasikiliza mawazo yote, japo si kila wazo nitakubaliana nalo. Nimesikia mambo mengi mazuri sana na mabaya sana toka kila Chama, nikakumbushwa kuwa kumbe wanachama wote wa hivi vyama ni binadamu tu kama mimi, wenye mazuri na mabaya, busara na ujinga, ushupavu na uoga, uzalendo na ubinafsi. Nikakata shauri kwamba rangi ya uanachama haipaswi kuniamulia nani kwangu ni rafiki au adui, anayekubalika au asiyekubalika, kwa kuwa mwisho wa mambo yote, sisi sote ni Watanzania, jambo ambalo wengi wa wale wanaojiona wanasiasa wenye hekima wanalisahau kirahisi sana.
 
Back
Top Bottom