Tahadhari huyu anaejiita ndupa ni tapeli

Tahadhari huyu anaejiita ndupa ni tapeli

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,595
Reaction score
1,863
Habari waungwana,

Kuna huyu jamaa anajiita ndupa ambaye ame post hapa tangazo lakutafutia watu wasichana wa kazi, nitapeli na hatari.

Niliamua kuanza nae mpaka nione mwisho wake; anakudanganya ameshapata msichana wakazi huku akikwambia tafuta njia ili akufikie, hakwambii utume pesa ili usimuone tapeli anatafuta mwenzie huko anadanganya ni kondakta wa gari fulani anakwambia mtumie konda then ukimpokea ndio mtumie hela yake ya kukutafutia, ukituma tuu umeumia.

Anadanganya anamuandikisha kwa serekali za mitaa kumbe uongo.

Nilianza nae kwa maswali mengi saana, kuanzia ki vp wazazi wakuamini wakupe mtoto wao, kwanza hawakujui pili anapo kwenda wao hawajui.

Kabaki anababaika tuu, nikamwambia sasa we mtume kwenye gari akifika stand ndio nilipe nauli, pia nipe mawasaliano na wazazi wake, kasema ngoja afanye maarifa, akaa kimya hakujibu lolote.

Nikampigia nikamwambie nishapata kondakta namfamu mpigie mkabidhi, kuhusu nauli nishamalizana nae, jamaa kasema powa, kuanzia hapo hakupokea simu tena mpaka leo.
 
nani akulipe wewe ndupa kuweka tangazo jamiiforum? Ingekua jf ni mtaani ungeshatiwa kiberit. Wizi siyo kitu kizuri. Dunia itakufunza in a hard way. Mark my words
yupo agent sinza wa kazi hizo siyo mimi
 
Mkuu weka hapa no yake ya simu anayoitumia kutapeli
 
ndupa usicheze na JF siku zako zinahesabika na tutaleta mrejesho hapa
 
Last edited by a moderator:
labda timu moja na yule jamaa wa kipindi kileeeeee MCHUMIPESA teteteteheeee
 
mambo mengine mnajitakia tu, bora tuwaseme.
Mtu mzima utaanzaje kutuma tu pesa kirahisi wala humjui unayemtumia? hivi mpaka muambiwe nini ili muelewe..? kwa nini hamtaki kujifunza kwa wengine.
hizi kesi zipo tangu kitambo sasa kwanini mtu mwingine leo urudie makosa yaleyale.
Achaneni na mahousegirl wa mitandaoni.

samahani kama nimekukwaza ila siku hizi mtu kutapeliwa kizembe inakera sana.

narudia tena samahani kama nimekukwaza kwa maneno niliyotumia.
 
Naona Mr Ndupa alikuja kupima upepo alipoona mambo mazito kakimbia kweupe... naona kuanzia sasa no zake za magumashi hatatumia tena.
 
Back
Top Bottom