Ahsante sana. Sijasikia kutoka kwenye mamlaka zetu kusema chochote? Mpaka maafa? Dah
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe:
met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti:
Tanzania Meteorological Agency - Admin -
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 02 Januari, 2014
Taarifa kwa umma: Upepo mkali pamoja na mawimbi makubwa vinatarajiwa
katika maeneo yote ya ukanda wa pwani.
Taarifa Na. 201401-01
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 4 Asubuhi
Daraja la Taarifa: Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
03 Januari, 2014
Mpaka:
Tarehe
05 Januari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na
mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0 inatarajiwa katika ukanda
wote wa pwani.
Kiwango cha uhakika: Wastani (60%)
Maeneo yatakayoathirika
Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara
pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo
wa hewa katika Bahari ya Hindi, kusini mashariki mwa kisiwa cha
Madagascar. Mfumo huu unatarajiwa kusababisha kuvuma kwa upepo
mkali kutoka pwani ya Somalia kuelekea pwani kusini .
Angalizo:
Wakazi wa maeneo yaliyotajwa (hatarishi) wanashauriwa kuchukua
tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo pale itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.