Aanze kujihukumu yeye na serikali yao alipokua madarakani kwa kuacha nyufa na kudharau kuiziba sasa ukuta ndo ushamwangukia ananyooshea watu kidole
Kwa hiyo fashion ni kuingia choo cha kiume walipo mafisadi na watoa rushwa au siyo?Sumaye kajikuta anajisaidia choo cha kike
Wameshindwa kusikiliza nukuu nyingi za Nyerere ambaye wanajifanya kumuenzi itakuwa Sumaye? Kifo cha hiki chama ni dhahiri na kikinusurika kitabaki mahututi.
Maoni yaliyotolewa na Mh F Sumaye, pamoja na kushindwa kupata U-NEC, ni wake up call kwa CCM.
Sina uhakika kama Mh Sumaye angetoa maoni hayo kama angeshinda kinyang'anyiro hicho cha kugombea U-NEC.
Hata hivyo kwa wanacha waaminifu wa CCM aliyosema Mh Sumaye ni common knowledge, ufisadi utaiangamiza CCM kama chama cha siasa makini.
Nimeona maoni kama haya haya ya mtoa mada ambaye vile vile inaelekea ni mwana CCM:
Nimesoma gazeti la NIPASHE leotarehe 9 Oct. 2012, Katibu Mkuu Mukama akijibu tuhuma za Sumaye kuwa azipeleke kwenye vikao husika.Tunasahau kuwa waamuzi wa mustakabali wa chama ni wanachama wanaoona yanayoendelea hukohuko mitaani.
Tumeona jana ngumi na kurushiana viti katika kikao cha uchaguzi huko Musoma, sababu ikiwa hiyohiyo rushwa.
Mukama akisubiri kuletewa hoja ofisini, basi uhalali wa chama kwa wanachama wake utaendelea kushuka.
Wahenga walisema mwenye masikio na asikie!
Asante mkuu Uwezo Tunao kwa kuonyesha kukerwa kwako na mwenendo wa rushwa ndani ya chama chetu.KWA NINI CCM KITAFUNWE KWA KASI KUBWA AJABU NA MBINU ZAKE ZENYEWE ZA UCHAKACHUAJI ULIOTUKUKA KATIKA CHAGUZI ZAKE NDANI AU NDIO KUSEMA UNABII JUU YA HATIMA YA CHAMA HIKI NDIO SASA KUTIMIA??
Mkuu asante kwa kupenda kuona CCM kisichochakachua manbo kila wakati.
Nasema asante kwa kutamani kuona DEMOKRASIA katika uhalisia wake isiobughudhiwa hata kidogo na saratani za UDINI, UANAMTANDAO, UKANDA NA UKABILA.
Nashukuru pia ulivyoonyesha mpenzi makubwa kwa kutoa maoni yako yaliojawa uchungu mkali toka kwenye sakafu la moyo wako na kuwataka viongozi wako wwe ni wenye KUWAFUATA WANANCHI WALIPO NA KUSHUGULIKIA MALALAMIKO YAO HUKO HUKO bila kuendeleza umangimeza na kiburi cha kukaa kitako kwenye viyoyozi maofisini KUTEGEMEA KUFIKISHIWA KILA KITU HUKO HUKO.
E baba weeee, kidogo hadi hapo naona kama vile uko kwenye usingizi mzito ukidhania ya kwamba hiki CCM-Ukoloni Mamboleo ambacho hivi sasa kiko rasmi katika udhibiti wa lile kundi hatari la MAFISADI eti unakichukulia kuwa sawa na ile CCM ya Mwalimu Nyerere ya miaka ile; pole sana hadi hapo.
HULKA na tabia mbaya ya ukabila, ukand, udini pamoja n uanamtandao kuwa ni misingi rasmi ya watu KUCHAKACHUANA hakika ndio sanda na jeneza la chama hiki pachaka kutoboka jumla hivi karibuni kote nchini.
Nasema kama CCM ni kile kile kilichojaa kiburi cha kobe, UFISADI wa jogoo kujihisi kila tetea ni halali yake, nasema kama CCM ni kile kile chenye 'U-MIMI' kwa na mslahi ya umma wa Tanzania badaye, kamwe hakutosikilizwa mtu hapa; si Mhe Sumaye wala melf ya wanachama wengine kibao ambao nao wamefikwa na madhila kama haya haya.
Mkuu, hadi hivi sasa ni kwamba ombi lako limefikia patupu patupu na kamwe hiki CCM tunachokifahamu vema sana tu wala hakiwezi kubadilika hata kwa dawa kwa kuwa fitina na majungu ndio sala zao za kila siku iwe ni asubuhi, mchana au usiku.
Mwisho, nimalizie kwa kusem ya kwamba unabii wa kale juu ya chama hiki kikongwe sasa waja kwa kasi ajabu leo hii kuliko hata hapo jana.
Ajabu zaidi leo hii ni kwamba hata zile salam za wanacha wakulima na wafanyakazi wa miaka hiyo kwa kusema 'KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI' leo hii imebadilika kabisa huku matajiri wachache wakiwa ndio wamekihodhi chama humu wakijibunia salam yao mpya ya 'KIMUDU CHAMA CHA MAPINDUZI' ambapo mtokeo yake ndio kama hivyo dhuluma kwa kwenda mbele kwa kila kitu wanchoweza kukitia mikononi na kukimudu vilivyo kwa faida ya wachche.
Kama watu mlikua hamjui bado tu; CCM ya leo 'KINA WENYEWE' na wenyewe hao si MKULIMA wala MFANYAKAZI tena hivyo unapolia kilio cha mtu mzima hivi mbele ya kandamnasi wengine huku tujajiuliza eti 'kwani bado alikua hajui tu CCM ya leo hati miliki yake kuwa chini ya makucha ya MAFISADI ORIGINAL without apology???????'
Majuzi Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania, aliwaita waandishi wa habari kuwaelezea kile kilichoitwa rushwa mpya katika chaguzi za ndani za CCM. Katika kulijadili hili, tuiangalie dhamira na uadilifu wa SUMAYE, na kisha nafasi ya SUMAYE katika kuenzi au kuipiga vita rushwa.
Katika mkutano wake na waandishi, SUMAYE alitaka kuwaaminisha waandishi na watanzania kuwa yeye ni mtu safi, mtu asiyependa rushwa. Na kwa maneno yake alitamka kuwa atapigana ndani ya CCM kuondoa mfumo unaopalilia uongozi wa rushwa.
Katika kuitafakari kauli hiyo ya SUMAYE, tumjadili SUMAYE kama kweli ni mtu mwenye uwezo wa kupigana na rushwa, na pia tuangalie, na kisha tujiulize: Je, SUMAYE atapigana na rushwa za ndani ya CCM ili yeye SUMAYE asiye na uwezo wa kupata hela ya kutosha kuhonga aweze kushinda, au atapiga vita rushwa kwa sababu anaichukia rushwa?
Napenda kuwakumbusha wachambuzi kuwa ni huyu SUMAYE akiwa waziri mkuu ndiye aliyekuwa mtetezi mkuu wa ile rushwa walioianzisha CCM na kuiita TAKRIMA. Hakuna aliyekuwa mtetezi mkuu wa TAKRIMA wakati ule kumzidi SUMAYE. Ni huyu SUMAYE ndiye aliyewaambia vijana na wafanyabiashara mara kadhaa kuwa, 'ukitaka biashara yako istawi, lazima uwe ndani ya CCM'. Ni wakati wake vijana wengi ili wasisumbuliwe na polisi, askari wa jiji na TRA waliamua kuchomeka bendera za CCM ili kuepuka usumbufu. Na kwa upande mwingine, kauli yake ilidhihirika kwa wale wafanyabiashara ambao walionekana kushabikia upinzani, baadhi yao walifilisiwa kwa kuitumiaa TRA, na wengine kupitia mamlaka za miji.
Ndani ya CCM hakuna kiongozi hata mmoja ambaye hajawahi kupokea rushwa au malipo yasiyo halali. Ni CCM ndiyo walioasisi malipo ya kukaa (sitting allowance), ambao ni wizi uliopewa kanuni ya kuulinda. Ni CCM ndiyo walioasisi malipo anayopewa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Manaibu, ambayo wanaiita officiation allowance. Hii ni posho ya kukata utepe wanapofungua miradi au kuizindua. Huu nao ni wizi wa hela ya Watanzania unaolindwa na nyaraka zilizoandaliwa na wezi wenyewe, akiwemo Sumaye.
UKWELI: Sumaye hana tofauti na viongozi wengine wa CCM. Hakuwahi kuwa na tofauti na hata sasa haonekani kuwa ni tofauti. Kauli alizozitoa ni za chuki kwa wana-CCM wenzake watoa/wapokea rushwa baada ya kuona hana uwezo wa kuwashinda. Ni vema Watanzania na waandishi wa habari mngemwuliza ushiriki wake wa kuanzishwa na kupalilia rushwa kwa kuipamba kwa neno, 'TAKRIMA'. Tunamshukuru Mtikila aliyeipinga kwa nguvu zote, na kueleza wazi kuwa TAKRIMA ni rushwa, na kisha mahakama kuridhia kuwa kinachoitwa na CCM TAKRIMA, ndicho watu waadilifu hukiita RUSHWA.
Mkuu huo ndio ukweli wenyewe, sasa nimkuwa nikitafakari sana juu ya kilio ch viongozi wetu juu ya utawala bora.Mkuu unaipa tahadhari CCM dhidi ya rushwa? Unatilia maanani kauli ya Sumaye? Bado hujakubali kuwa motisha (incentive) inayowavutia wengi kugombea nafasi za uongozi katika chama hicho ni fursa kadhaa za kifisadi ikiwemo rushwa, ukwepaji kodi, dili za kila aina, n.k. bila kuguswa na sheria wala kubugudhiwa na taasisi za dola? Basi angalau mkumbushe kwanza Sumaye aikane kauli yake maarufu kwa wafanyabiashara kama "wanataka mambo yao yawanyokee ...". Ukiondoa fursa hizo za kifisadi, CCM haipo! Hakuna ndani ya CCM asiyejua madhara ya rushwa na umuhimu wa kuipiga vita kwa mustakabali mwema wa chama lakini ndio hivyo tena; anayeipiga vita rushwa kwa dhati SI MWENZAO!