masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,608
- 14,552
Chama kikongwe cha siasa nchi Tanzania CCM kinazidi kupoteza demokrasia ndani ya chama chake,ama kwa makusudi au kujisahau.Namaanisha kutokana na staili yake inayofanyika katika chaguzi zake za ndani ya chama.Tumeona rushwa,udini na ukabila umeendelea kushika kasi na kukitesa chama hiki kikongwe nchini.
Yaliyotokea huko Shinyanga ni mfano mzuri wa CCM kujimaliza ama kujikaanga kwa mafuta yake yenyewe.Kampeni za ujumbe wa NEC kupitia wilaya kwa wilaya ya Shinyanga mjini imekitia doa chama hiki kwa kampeni chafu za ukabila na rushwa huku wagombea wakijinadi wataimaliza CHADEMA kwa kutumia nguvu yao ya kifedha na kiutawala kuelekea uchaguzi wa 2015.
Uchaguzi umezidisha makundi yanayo hasimiana ndani ya chama.Pia chaguzi hizi zimeibua chuki miongoni mwa wanachama hususani wale wanao kikosoa chama, kwa majina yao kufyekwa na sekretarieti ya chama,huku majina mengine yaliyofyekwa huko wilayani yakirudishwa mfano jina la Mary Nagu.
Hali hii imesababisha sintofahamu ndani ya CCM kutokana na staili yao ya kujilimbikizia madaraka kitendo kinachooneka mtu mmoja kuwa viongozi ndani ya jamii kama vile hakuna watu wenye sifa za kushika nyadhifa ambazo mtu mmoja anatunukiwa.
Janga lingine ni kuondoa kundi ambalo limekuwa wasemaji wasio ogopa kukisema chama chao kwa kufuata misingi ya kiongozi akubali kukosoa na kukosolewa.Hali hii imesababisha baadhi ya wabunge majina yao kukatwa kwa vile tu walionyesha msimamo wao wakati wa kumpinga Waziri mkuu kwa kusaini kwenye fomu ya kutafuta saini 70 za Zitto Kabwe za kutaka kumng'oa mtoto wa mkulima.
Pia chama hiki kimekuwa kokoro katika uchaguzi zake kwa kuzoa hata wale waliopoteza sifa ndani ya jamii husika ama kwa vitendo vya rushwa ,ukatili na hata uharamia kitendo kinachosababisha chama hiki kushindwa kujitenga na kauli ya wapinzani kwa kukiita Chama Cha Majambazi.
Mwisho ,kauli ya Sumaye aliyekuwa wazir mkuu kwa kipindi chote cha serikali ya awamu ya tatu kuutangazia umma kuwa CCM ina nuka rushwa ni pigo kubwa kwa mustakabali wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu,kauli ya Sumaye si ngeni masikioni mwa Watanzania kwani hata Mh. Makongoro Nyerere aliwahi kulalamika katika harakati zake za kuusaka ubunge wa EAC.Ni wakati sasa wa kujitazama na kuangalia wapi wanacheza karata zao vibaya na kutafuta karata turufu na kucheza kadi vizuri.
Maoni yaliyotolewa na Mh F Sumaye, pamoja na kushindwa kupata U-NEC, ni wake up call kwa CCM.
Sina uhakika kama Mh Sumaye angetoa maoni hayo kama angeshinda kinyang'anyiro hicho cha kugombea U-NEC.
Hata hivyo kwa wanacha waaminifu wa CCM aliyosema Mh Sumaye ni common knowledge, ufisadi utaiangamiza CCM kama chama cha siasa makini.
Nimeona maoni kama haya haya ya mtoa mada ambaye vile vile inaelekea ni mwana CCM:
Nimesoma gazeti la NIPASHE leotarehe 9 Oct. 2012, Katibu Mkuu Mukama akijibu tuhuma za Sumaye kuwa azipeleke kwenye vikao husika.Tunasahau kuwa waamuzi wa mustakabali wa chama ni wanachama wanaoona yanayoendelea hukohuko mitaani.
Tumeona jana ngumi na kurushiana viti katika kikao cha uchaguzi huko Musoma, sababu ikiwa hiyohiyo rushwa.
Mukama akisubiri kuletewa hoja ofisini, basi uhalali wa chama kwa wanachama wake utaendelea kushuka.
Wahenga walisema mwenye masikio na asikie!
Kwa hiyo unakubali kuwa rushwa katika chaguzi za CCM ni msingi sahihi wa kupata viongozi!Sidhani kama kulikuwa na haja ya kuwa na utaratibu ndani ya chama kama maamuzi yangekuwa yanafanyika mitaani. Sumaye anatapatapa tu, Fisadi mkubwa yule. mara hiyo tu ameshasahau soko la machinjio kule kibaigwa na Mashamba aliyojitwalia huko kibaha? Kupigana na viti ni kawaida tu kwa vyama vyetu hivi kwani siyo siku nyingi haya tumeyashuhudia ndani ya CDM kule Ilemela.
angetoka ccm tusingejua haya aliyotueleza, muda muafaka ukifika atatoka tu, kila jambo na wakati wake.sumaye hana jipya,kama ye mjanja atoke ccm ili tumwelewe vizuri! Sio kulalama tu.....!
Maoni yaliyotolewa na Mh F Sumaye, pamoja na kushindwa kupata U-NEC, ni wake up call kwa CCM.
Sina uhakika kama Mh Sumaye angetoa maoni hayo kama angeshinda kinyang'anyiro hicho cha kugombea U-NEC.
Hata hivyo kwa wanacha waaminifu wa CCM aliyosema Mh Sumaye ni common knowledge, ufisadi utaiangamiza CCM kama chama cha siasa makini.
Nimeona maoni kama haya haya ya mtoa mada ambaye vile vile inaelekea ni mwana CCM:
Nimesoma gazeti la NIPASHE leotarehe 9 Oct. 2012, Katibu Mkuu Mukama akijibu tuhuma za Sumaye kuwa azipeleke kwenye vikao husika.Tunasahau kuwa waamuzi wa mustakabali wa chama ni wanachama wanaoona yanayoendelea hukohuko mitaani.
Tumeona jana ngumi na kurushiana viti katika kikao cha uchaguzi huko Musoma, sababu ikiwa hiyohiyo rushwa.
Mukama akisubiri kuletewa hoja ofisini, basi uhalali wa chama kwa wanachama wake utaendelea kushuka.
Wahenga walisema mwenye masikio na asikie!
Mkuu usiifurahishe nafsi yako kwa kufikiri mtu unaweza kumshabikia mtu badala ya principle.Naona sasa mzee wa hanang anaanza kumzidi mzee mamvi umaarufu humu JF, au kawanunua watu wa kumpandisha chat?
Msishabikie sana kifo cha CCM maana hakitakuja bila a price tag ya machafuko ndani na nje ya CCM.Kufa kufaana, wao wanakufa sisi tunachukua nchi
kama fisadi anaweza kuona ufisadi wa kutisha zaidi ya kuushangaa basi ni wazi hali si shwari.Hii ni ishara kwamba alichoona Sumaye hakuwahi hata fikiri ndio maana anashangaa.Hii ndio kazi waliyoiasisi kupitia Takrima.