Tahadhali: Wizi wa Mb Halotel

Tahadhali: Wizi wa Mb Halotel

Hawa jamaa walianza vizuri sana,speed kali na bei nafuu mpaka nikawa addicted nao

Majuzi wamepandisha bei ya vifurushi na speed imeshuka bado nipo loyal ila this week nimegundua kitu cha ajabu sana,mb zinakatika kwa speed ya ajabu nikasema jana usiku nifanye jaribio fulani

Nimelala saa nne nikiwa na MB 1000 nikazima data na simu kabisa,naamka saa 12 nina MB 200 jesus christ nikasema ni peruse jamii forums,in 30 minutes nina MB 0,nikiwapigia wananiambia eti niende kwenye office zao

Leo naweka mb kwa mara ya mwisho nione tena wizi wao unaendaje,jamani HALOTEL VAS kuweni na huruma jamani,uchumi wenyewe wa kibashite tunaumizana hivi? mimi mwenyewe ni mteje loyal kila siku naunguza karibu 4,000 kwa mb zenu mnanifanyia hivi jamani??

UPADATE: saa 8.30 asubuhi niliweka tena 1500 mb sasa hivi saa 12.52 mchana nina 411 mb,hapo nipo jf na facebook tu toka asubuhi,sijadownload kitu wala sija stream video....ENOUGH IS ENOUGH HALOTEL VAS narudi airtel hata kama speed ndogo lakini kufanywa bashite kwa kuibiwa mb siwezi tena...byebye,itabaki line ya kupokelea simu tu.
pitia huku Vifurushi vya internet visivyo rasmi kwa makampuni ya simu
 
Hili ni tatizo kubwa..


Mimi nilinunua ile Wifi yao baada ya kuona huu ushenzi wa Halotel nikatupilia mbali kile kimodem chao...japo nimekula hasara
Usinge tupa kuna jamaa humu jf wangekuelekeza ungeiunlock ingekuwa inatumia mitandao yote.
 
Halo mkuu hawa jamaa ni shida TCRA inabidi wafuatilie.Asubuhi SAA tatu Leo nilikua na MB 200,nimeperuzi JF tu ata dakika 20 hazijafika nikazima data sasa hivi SAA 19:05 kuna MB 116!kweli hawa jamaa ni kiboko.
 
mkuu angalia simu yakonkama hauna auto backup zozote unazofanya pale unapiwasha data. natumja halotel lain ya chuo jana saa tatu usiku nimeweka 1100mb nimestream youtube mpaka nimechoka na now naendelea kuperud insta na jf bado bundle lipo la kuzid

Sometimes simu zetu zinafanya autoretrieve bila kujijua unakuta mb zinaenda tu
Auto backup ndo mini?ebu tujuze mkuu.
 
Halo mkuu hawa jamaa ni shida TCRA inabidi wafuatilie.Asubuhi SAA tatu Leo nilikua na MB 200,nimeperuzi JF tu ata dakika 20 hazijafika nikazima data sasa hivi SAA 19:05 kuna MB 116!kweli hawa jamaa ni kiboko.
jaribu kuangalia labda kuna baadhi ya application zinarun background nenda kwenye setting kisha cheki data usage
sometimes mb zinaisha bila hata ya kufungua application yoyote ile
au tafuta app ya internet speed meter hiyo app inayoonyesha matumizi yako ya internet. hapo utaona kama unaibiwa au vipi?
Screenshot_2017-08-26-11-10-26.png

hapa chini utaona matumizi ya internet yanavyoenda
Screenshot_2017-08-26-11-09-32.png

sema baadhi ya laini zina majanga yake.
 
Back
Top Bottom