Tafuta uzuri katika ubaya

Shemasi Jimmy

Member
Apr 23, 2021
93
104
Shemasi Jimmy 0659 611 252

Halleluja watu wa Mungu, apendaye mafundisho hupenda maarifa, karibu tupate maarifa.

Maandiko yanasema: Rum 12:21 SUV

Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Binadamu yeyote ana mazuri na mabaya, Ubaya au uzuri upo katika mtazamo wa mtu. Unayemuona adui kwako aweza kua malaika sehemu nyingine, aliyekua Rais wa Tanzania Mh Kikwete alisema ‘’usikubali kurithi adui wa mwingine’’.

Yesu hakua na dhambi lakini alikaa na wenye dhambi ili awaokoe hao wenye dhambi. Yesu hakua mwizi lakini aliongea na wezi na hata kuwaokoa (Mt 11:19). Yesu alijua Yuda kua ni mwizi(Yoh 12:6) na mwenye nia mbaya na uhai wake, lakini aliendelea kumuamini na kumkabidhi hazina ya michango iliokusanywa. Yesu alijua Petro atamsaliti lakini hakusita kumkabidhi funguo za ufalme. Wewe unaona nini kwa adui yako?

Tumeambiwa tusamehe saba mara sabini (Mt 18:22) ili tusiyakose mazuri kwa waliotukosea. Kumbuka hata saa mbovu kunawakati husema ukweli (Je, hilo sio jema?), wenye hekima wanalo la kujifunza kutoka kwa Teja, mwizi, kahaba, na wengineo wasio aminika katika jamii.

Samsoni aliona asali katikati ya mzoga wa simba aliyemuua (Waamuzi 14:9) wewe unaona nini katikati ya mabaya ya mwenzako?

**Mungu akubariki sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom