Tafuta njia ya kukabiliana na matatizo

Tafuta njia ya kukabiliana na matatizo

Protein

Member
Joined
Apr 18, 2019
Posts
53
Reaction score
194
Maisha ni kama wimbi la maji mtoni na baharini. Yanakuja na takataka nyingi sana. Unapata habari ya msiba wa mpendwa wako mzazi, mume, mtoto, rafiki nk. Unapata habari za ugonjwa usiotibika cancer, HIV,nk.

Kukosa pesa wakati una majukumu, undaiwa madeni mtaani, ada za watoto, kodi ya nyumba na mengineyo.

Kupata habari mke/mume wako ana mahusiano ya kimapenzi na boss wake, rafiki yako wa karibu au mtumishi wenu wa ndani.

Wengi hatuna coping mechanism za kukabiliana na majanga. Wengine huamua kunywa pombe, kuvuta bangi, kula kwa kujiliwaza. Haya yote huleta matatizo mbadala.

Njia nzuri wengi huitumia ni kutegemea kitu chenye nguvu kuliko wewe. Unaweza kumtegemea Mungu, mizimu ya kwenu au kuwa na imani.

Bila ya kuwa na imani kwa kitu chenye nguvu kuliko wewe, unaweza kujiua.

Tuelezane coping mechanism zetu .

Bujibuji
 
Bible verses nd prayers , Tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu
 
Back
Top Bottom