Tafsiri ya ugaidi Tanzania; Serikali ijifunze

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Wakati Tunasoma, Hata kwenye Maisha Tunasisitiza Sana Kujifunza kupitia Wenzetu Waliofanikiwa Wanafanya nini? Au waliowahi kupatwa na Matatizo ilikuaje?

Hii inaenda kwenye Serikali Yangu ya Tanzania Na Vyombo Vinahusika. Ni muhimu sasa Kwa Tanzania Nasi kujifunza kwenye Nchi zingine Kuhusu Matukio Ya Kile Kinachoitwa ni UGAIDI. Nina fikiri Tanzania Tuna Tafsiri Yetu Binafsi ya Neno UGAIDI ambalo ni Tofauti na Nchi Zingine. Hili Tuliona Hata Kupitia kesi Ya Mwenyekiti wa Chama Cha Maendeleo Tanzania (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe, Ambaye ana Kesi ya Ugaidi Lakini Matukio Yanayotajwa Ni Tofauti na Nchi za wenzetu ambazo Tayari Zimekumbwa na Matukio Ya Ugaidi.

Leo, Uganda Wamepata Milipuko Mikubwa Miwili, Moja Ni nje/ karibu na Eneo la Bunge, Na Jingine ni Karibu na Kituo Kikuu cha Polisi Nchi Uganda. Tanzania Hatuna Tofauti na Uganda, kwasababu Wote tupo East Africa. Kupitia Milipuko hii Miwili ni Rai yangu Kuwa Ni wakati wa Serikali Yetu ya Tanzania Kujitafakari na Tafsiri ya Neno Ugaidi. Lakini Pia Hata nchi Jirani Ya Kenya Miaka Ya Nyuma Ilishakumbwa na matukio ya kigaidi Moja ni Lile la WESTGATE SHOPPING MALL ambapo watu Takribani 71 walifariki na 200 walijeruhiwa katika Mapigano hayo, Na tukio Jingine ni Lile lilotokea kwenye Hotel Nairobi.

Matukio Haya Yote Yatufundishe Tanzania na Sasa Yatupatie maana Halisi ya Neno UGAIDI! Ukiangalia Makosa Anayo tuhumiwa nayo Mbowe na Wenzake ukilinganisha na Kile kilichotokea Uganda Leo na Kenya Mwanzoni mwa mwaka Huu na Miaka Ya Nyuma Utaelewa Kuwa Tanzania Tuna Maana na Tafsiri Tofauti ya Neno UGAIDI.

Kupanga kuuitisha Maandamano Yasiyo na Ukomo haijawahi kuwa njia Ya Kufanya Vitendo vya Ugaidi hata siku moja. Mfano mzuri ni kile kilicho tokea Uganda Leo, Watu wamejitoa Muhanga na Mlipuko Mkubwa umetokea Karibu na Majengo ya Bunge, Hivyo Mabomu ndio yalitumika katika Milipuko Hiyo. Tasfiri Yake Nini? Unaona Kweli hawa watu walikuwa wamepinga Na Sio kama Sisi hapa Kwetu hatuna Hata majina ya Vituo vya mafuta vilivyopangwa kulipuliwa, hatuna hata bomu moja Lilokamatwa. Lakini Je Ni nchi gani Tukio La kigaidi liliwahi kutokea kwa Kulipua vituo vya Mafuta? Hata yale mataifa ambayo yamekuwa na Maandamano Makubwa kwenye nchi zao hawaja wahi kulipua vituo vya Mafuta.

Kilichotokea Wastegate Shopping mall, Kenya Kilihusisha Siraha kali za Kivita na A-K47 zilitawala na hazikuwa Ofisi za Za viongozi wala Serikali, Na Wanajeshi kadhaa walifariki katika majibizano, Magaidi wale Hawakuwa na Bastola lenye Risasi 3 kutekeleza ugaidi wao. Wala hakuna kiongozi wa Serikali alikuwa mlingwa walile tukio. Tanzania Tunapata Wapi Ujasiri wa Kusema Kuwa Bastola 1 na Risasi 3 vipangwa kutumika kutekeleza Matendo Ya Kigaidi nchi katika mikoa 5? Kile kilichotokea Uganda leo karibu na kituo cha Polisi Mlengwa alikuwa ni Kituo cha Polisi, huenda Target haikwenda Sawa, Je Akina Mbowe na Wenzake walipanga Kuwadhuru polisi wowote Tanzania?

Lakini Tusiende Mbali, Kuna Kijana Alitokea Anaitwa Hamza, Je Hamza Alifanya nini? Kinaendana na Kile wanachotuhimiwa akina Mbowe?

Ni wakati sasa wa Tanzania Kutafakari maana Halisi Ya Neno UGAIDI, Ambayo hata RAIS AKITOKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI, Akasema Tanzania kuna Mtu anahukumiwa kwa kufanya Mipango ya Vitendo vya Kidai basi DUNIA imuelewe.

Narudia Tanzania Sisi Hatujawa Kisiwa, Tujifunze kwa Uganda na Kenya Namna Matukio Yalivyotokea. Then Tutajua ni wapi kwa kuimarisha. Wananchi Wakija Kuchoka Na Matukio yeyote yule anaweza kuwa Tayari kufanya Lolote.
 
Unafikiri hawajui tafsiri ya neno GAIDI, wameamua tu kwa vile wanaamini nguvu walizonazo wanaweza kufanya chochote na wasifanywe chochote, wanachotakiwa kufanya ni kutafakari, je haya wanayofanya yanalijenga hili Taifa ama yanalibomoa, MAONI YANGU.
 
Gaidi unamwambia nyosha mikono juu.

Huku muuza mbege anafagia uwanja. Halafu huo mtaa wanaitwa wenyeji kushuhudia magaidi.Wakati watu wangefichama hata kwenye mapipa ya mbege.

Sabaya ni mtu mhimu sana kutoa ushahidi utetezi ukianza.aweza toa siri zote
 
Kwa mujibu wa kesi, kikosi kamili walikuwa magaidi 4,bastola 1 na bajeti ya laki 6. Walipanga kufanya nchi isitawalike kwa maandamano kila mahali na wakati huohuo wakilipua vituo mbalimbali vya mafuta, wakiangusha magogo kuanzia Moro hadi Mbeya na kuyatandika barabarani kuzuia magari yasipite, na wakati huohuo wakiwadhuru kina Sabaya kwa kuwapulizia sumu kwenye pua zao ili wafe.

Upelelezi ulofanywa na vyombo mahiri vya Tz, uliwakuta na bastola 1 na risasi 3 (sio mabomu na vilipuzi). Na hao wapelelezi wa vyombo vyetu vya usalama wakagundua kuwa magaidi hao wangeweza kulipua vituo mbalimbali vya mafuta na kuua viongozi wa serikali. Haya yote yangefanyika katika majiji makuu mbalimbali kama Dar, Moro, Iringa, Mbeya, Ars, Mz.

Wakati mipango yote hiyo ikiendelea, kati ya 2020/2021, ofisi zetu za usalama zikawa na huruma, magaidi wakaachiwa kuendelea na shughuli na mipango yao ya kila siku - kiongozi mkuu akaachiwa kusafiri ndani na nje ya nchi, kuruhusiwa kuomba na kugombea nafasi za kisiasa ...nk. kwa mwaka mzima.

Tumesikia (mwenye uhakika athibitishe), upelelezi (polisi) una mashahidi 20 kati ya 22, mmoja kati ya hao 2 wasio mapolisi ni yule mama muuza mbege.

Hii kesi ni kali, 90%+ ya timu nzima ya mashahidi inatoka ukoo 1, wa mapolisi. Kizibiti pekee kilichopo ni bastola 1 na risasi 1.
Namwonea huruma Hakimu. Mungu amjalie ahukumu kwa hekima za Mfalme Selemani mwanae Mfalme Daudi ktk Biblia
 
Nimecheka sana mkuu:D:D:D yaani huo muda wa kukata miti gaidi ataupata wapi?
Yaani bado nacheka nikuvuta picha na kuona jinsi gaidi anavyokata miti mikoa ya Arusha, Dar, Morogoro, Mbeya, Mwanza nk:D:D:D:D
 
Yaani bado nacheka nikuvuta picha na kuona jinsi gaidi anavyokata miti mikoa ya Arusha, Dar, Morogoro, Mbeya, Mwanza nk:D:D:D:D
Ni kwamba, kwa kuwa hawana misumeno ya aina yoyote (ingekuwepo wangeifikisha kama kizibiti), wangeazima kwa majirani ambao wasingekataa kwani Mbowe ni mtu mashuhuri.

Baadae angewarudishia misumeno yao na kuwaomba wasimwambie mtu, iwe siri yao hohooo! Halafu wangesaidiana kusukumia barabarani kuzuia magari yasipite, kuanzia Moro hadi Mbeya - hao 3, wakimaliza mkoa 1 wanahamia mwingine hadi miti yooote iishe.

Wakati huohuo wakikabiliwa na maandamano pamoja na kuwapulizia sumu kina Sabaya bila kusahau vituo vya mafuta...duh.
Kaaazi kwelikweli
 
uliwakuta na bastola 1 na risasi 3
Na kamfuko kama haka
1637110926102.png
 
Ugaidi wa kwetu ni kuonyeshs dalili za kwenda kinyume na hicho chama cha majambazi. Kudai haki wewe dai jambo lolote kinyume nao. Utasikia si jeshi polisi mpk raia wajinga wa mtaani kwako wanakusema. Utapigwa na utauawa na kuchekwa mpk hata na maskini wenzio
 
Back
Top Bottom