Tafiti: Wanaopiga selfie wana matatizo ya upweke!

Tafiti: Wanaopiga selfie wana matatizo ya upweke!

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Watafiti wabaini wapendao sana kujipiga selfie wana tatizo makubwa!

Wanasayansi wameonya kuwa wale ambao hupenda kujipiga selfie mara kwa mara, wana hatari ya kuwa wapweke.

Wanadai inaweza kuwa ni ishara ya kuwa na matatizo kwenye mahusiano yao au tatizo la afya ya akili.

Wanaojipiga sana selfie wanaweza kuwa watu wenye kasoro au wanaotafuta kuangaliwa, utafiti umesema. Watafiti nchini Thailand, walifanyia tathmini wanafunzi 300 na kuangalia mara ngapi huangalia picha walizojipiga wenyewe.

Washiriki hao ambao wengi walikuwa wanawake, walikuwa na umri kuanzia miaka 21 hadi 24, walihojiwa kuangaliwa kama walikuwa ni watu wa kujiamini, kutaka kuonekana, tabia ya kuwa wenyewe au upweke.

Wengi wao walionekana kutumia asimia 50 ya muda wao wa ziada katika simu zao au kwenye internet.

Wataalam wanaamini kuwa wanaume na wanawake wenye upweke hupenda kuchukua zaidi selfie kutafuta kukubalika na watu wengine.
Chanzo: Bongo5

plastic-surgery-selfies.jpg
 
Duh Wana matatizo? labda
Ila nadhani wangefanya utafiti kuhusu hawa wanatumia Instagram Tanzania, sijui wana matatizo gani, maana niejaribu kutumia Instagram nimeshindwa mara nyingi
Nasikitika IQ yangu hainifanyi nipende kutumia Instagram
Hehehehe dah kama ulikua kichwa ni kwangu
Bora instagram umejiuliza kuhusu Snapchat??
 
tafiti nyingine bhana......,, upweke

hasa tukipiga self watu wengi hapo inakuwaje?, upweke wa wengi??
 
Sasa si wanapiga ili waonwe na wapendwa wao? Kumbuka wengi wanaotumua social media kama Istagram ni vijana....na vijana kutafuta kupendwa, kuonekana zaidi, kupata likes nyingi zaidi [emoji4]....yote haya ndio wanayotaka vijana wengj....ni hali ya kawaida tu. Maisha yamebadilika sasa hivi watu hawana marafiki mitaani kwao, kila mtu anakuwa busy zaidi na hapa automatically unaanza kuishi mwenyewe mwenyewe, labda kuwasiliana na marafiki wachache tu na si watu wengi. Hii haimaanishi watu wamekuwa wapweke.....hii inamanisha watu wanafurahia maisha yao, kuwasiliana na wapendwa wao mitandaoni...

Ukichunguza zaidi unagundua....jinsi familia nyingi zinavyozidi kuimarika kipato (kwenda middle income level) basi watoto wao nao wanaingia mtindo mpya wa maisha...na mtindo huu wa maisha unawaweka karibu na technology....ni mabadiliko tusiogope.....tu-supoort vijana
 
Kuna dada mmoja nafanya nae kazi ofisi moja,

huyu dada ni shida,
Kila akija mgeni maarufu,atamganda na mwishoe atakukabidhi simu yake umpige picha na mgeni yule.

Mbaya zaidi,kuna wageni wengine unaona kabisa usoni kuwa hawapendi kupigwa picha ila wanalazimika kukubari tu kiroho upande.

Imefika wakati, anapofika tu mgeni ofisini,kila mtu anamkwepa dada yule.maana ukizubaa karibu yake,atakukabidhi simu yake na kukuegeuza mpiga picha wake wa dharula.inakera sana kwa kweli.
 
Kuna dada mmoja nafanya nae kazi ofisi moja,

huyu dada ni shida,
Kila akija mgeni maarufu,atamganda na mwishoe atakukabidhi simu yake umpige picha na mgeni yule.

Mbaya zaidi,kuna wageni wengine unaona kabisa usoni kuwa hawapendi kupigwa picha ila wanalazimika kukubari tu kiroho upande.

Imefika wakati, anapofika tu mgeni ofisini,kila mtu anamkwepa dada yule.maana ukizubaa karibu yake,atakukabidhi simu yake na kukuegeuza mpiga picha wake wa dharula.inakera sana kwa kweli.
hajiamini huyo Dada!
 
[HASHTAG]#MAJIRA[/HASHTAG] Watafiti Thailand wadai kuwa watu wanaopenda sana kujipiga picha za selfie wana matatizo ya kiafya au matatizo kwenye mahusiano yao https://t.co/HzhZm7ncmu
 
WEWE NI JINSIA GANI MBONA PROFILE YAKO IMEANDIKWA NEVER TRUST A WOMEN
 
Ha ha ha ha dah bas wadada wengi as kitanzania watakua wana matatzo maana kwa Selfie hatar sana na kile kimdomo kinavyovutwa
 
Nadhani itakuwa kweli,**** mtu aliewahi kuchukua muda kumtathmini Mange?
 
Back
Top Bottom