Tafasiri mseto kwa kusanyiko la viongozi wakuu.

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,950
1,039
Habari ya wikienda nyoote.
Leo kumbe ni siku ya tafakari ya madawa ya kulevya Duniani na kitaifa imeadhimishwa Arusha katika uwanja wa Shekhe A.Karume, mgeni rasmi akiwa Mkuu wa nchi.

Nilikuwa na miaadi yakukutana na mdau mmoja siku ya leo so namcheck akanijuza kamba yupo kwa uwanja na wamezuiwa kutoka kabisa hadi Mkuu wa Nchi amalize tukio hilo.

Amenijuza mengi kwamba gari zimetumika somba watu na kuwapeleka uwanjani na watumishi sharti kuorodheshwa majina kuthibitisha ushiriki wao.

Najaribu jiuliza hayo je ni maagizo ya nani?! Je ni viongozi kutaka thibitisha uwingi wa watu ni ishara ya kupendwa Mkuu?! Au hao wanatetea nafasi zao?

Je ni kuendelea mdanganya Mh rais kwamba watu wanakupenda ndio maana wamejaa tungu asubuhi ili hali wamesombwa na kwa vitisho haswa kwa hao watumishi na katazo la watu kutokutola nje ya uwanja?!

Mseto wa mawazo najaribu kuwaza haya mambo, au ni desturi ya wananchi kupelekeshwa hivyo kwa faida ya nani?! Na je ni haya hujitokeza katika makusanyiko yote ya viongozi wa kitaifa au ni leo tu?!!
 
Back
Top Bottom