Tafakuri za Mwisho wa Mwezi kuelekea Tanzania Tunayoitaka.

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
mahatma-gandhi-gandhiji.jpg

Sio kwamba hakuwa na hela ya kula hapana; aligoma kula kama sehemu ya jitihada ya kupigania haki kwa watu wa india. Pamoja na afya yake hiyo iliyotokana na harakati zake za kuwapigania watu, mmoja wa watu aliokuwa akiwapigania aliamua kumuua kwa kumpiga risasi tatu kifuani. Kosa lililomuudhi Bwana Nathuram hata akachagua kumuua mzee wa watu ; Ni jitihada za Mahatma kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya Wahindu na Waislam ambapo muaji aliona kuwa Mahatma kakupaswa kutafuta suluhu na waislam hasa ukizingatia kuwa yeye mwenyewe (mahatma) hakuwa muislam.Kwake Mahtma haki, usawa na utu vilikuwa ni vitu muhimu kuliko kitu chochote, bila kujali anamtetea nani na ujasiri aliokuwa nao katika kutetea mambo hayo ulikuwa ni mkubwa kuliko woga aliokuwa nao dhidi ya kifo.

Kila kiongozi ni mwanasiasa katika level Fulani ila si kila mwanasiasa ni kiongozi na katika mambo ya hatari sana duniani ni kuwa na wanasiasa ambao si viongozi kwa kuwa wanajikuta wakiwa na nguvu nyingi bila mitizamo sahihi. Hata hivyo jambo la kutia moyo na kufurahisha ni kwamba; mtu yoyoye anaweza kujifunza misingi ya uongozi, akaishika, akaifanyia kazi na kuleta matokeo mazuri.

Katika maisha ya mwanadamu, threat kubwa kupita zote ni kifo. Hivyo watu wengi wasio fikiri sawa sawa hupambana kutafuta positions na tittles wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wanapunguza threats zinazowakabili ikiwemo njaa, umaskini, uwezekano wa kufa n.k. Lakini wale wajuao maana na umuhimu wa uongozi; hutumia kila walicho nacho kuhakikisha kuwa wanasimamia vitu vya msingi wanavyo amini kuwa vinaweza kusaidia vizazi na vizazi kuishi kwa furaha na mafanikio. Hawa wao ishu si kupata fedha nyingi au kufa bali wanaishi je, wanachopata wanapataje na wanatumiaje, wanatumiaje mamlaka waliyo nayo na wanakufa wakifanya nini.

Hawa wanaona kitu muhimu zaidi kilichoko mbele yao ambacho kinawapa nguvu ya kukifikia kuliko woga wanaoupata juu ya kifo, achilia mbali vitu vingine kama maslahi. Ndio maana wakati Fulani Mahatma aliwahi kusema “ Uongozi si kutafuta kitu cha kukufanya uishi au kuishi nacho bali kutafuta kitu ambacho utakufa nacho”.

Kwa bahati mbaya; wengi wetu tunaruhusu tamaa ndio zituongoze. Tunashindwa kufikiri kama toka mwanzo kila mtu angeamua kuongozwa na tamaa badala ya fikra na nia njema kwa wengine; dunia leo ingekuwaje? Hatujui kwamba kuna watu ambao wangeweza wakaamua kutowasaidia wengine na wakaishi maisha ya raha mustarehe, lakini wakaamua kujitoa ili kuhakikisha kuwa jamii na vizazi vijavyo vinakuwa na maisha mazuri!? Hatujui kuwa, kuna watu ambao (kwa mfano) walikuwa na kila kitu ila wakaamua kuishi maabara kutafiti chanjo ambazo zilinusuru jamii na magonjwa ambayo yangeweza kuiteketeza dunia huku wakiwa wanasahau hata kula? Hatujui kuwa hata sasa kuna watu au nchi zinaweza kutawala nchi nyingine kulingana na teknolojia na nguvu walizo nazo, lakini hawafanyi hivyo kwa kuwa wanadhibiti tamaa zao kwa kufikiri na kutanguliza ustaarabu?

Ndugu zangu; wale tunaotamani kupata mamlaka, vyeo au wenye ndoto za kuwa viongozi kwenye nchi hii, ni vyema kutambua yafuatayo;-

1. Hata uwe na fedha au mali kiasi gani, hauwezi kula zaidi ya kilo mbili kwa wakati mmoja, na hata ule kiasi gani baada ya masaa machache utasikia tena njaa na hali hiyo itaendelea hivyo hadi utakavyokufa. Kwa hiyo tusiwe impressed na fedha na mali kwenye vitu vya msingi bali tuwe impressed na matokeo ya yale tunayoyafanya.

2. Hata uwe na cheo kikubwa kiasi gani, bado utakula, utalala, na mwishowe utakufa. Pigania mambo yamsingi yatakayosaidia watu wapate vitu vizuri kwenye maisha yao na usipigane kutafuta sifa kwa kuumiza wengine . tumia vipaji na mamlaka yako au kile ulichonacho kwa tahadhari na tafakari matokeo ya kila unachokifaanya.

3. Usiogope sana changamoto unaposimamia mambo ya msingi ambayo yatasaidia ustawi wa watanzania wenzako na jamii ya mwanadamu kwa ujumla. Kumbuka kuwa kifo ndio changamoto kubwa kupita zote inayomkabili mwanadamu lakini hakuna mtu ambaye ashawahi kunusurika kwa kukiogopa na kukikwepa. Kwa namna ya ajabu sana; kadiri unavyokimbia kifo ndivyo unavyoki attract kukukabili. Hivyo usihofie sana kufa bali hofia kufa ukiwa unadhulumu watu wengine au kufanya matendo ambayo hayana maana yoyote.

4. Ishi duniani kwa unyenyekevu kwani sisi binadamu ni viumbe dhaifu sana hata kama tumepata nguvu au mamlaka fulani duniani. Kulikuwa na watu waliokuwa na nguvu sana duniani wengine wakazitumia vizuri wengine wakazitumia vibaya ila leo wote wamelala chini.

5. Jitahidi kwa kadiri uwezavyo kushawishi “Inspire” watu kwenye vitu unavyoviamini na kuwasaidia watu kupata vitu vizuri ambavyo wanavitamani kwenye maisha yao kulingana na uwezo na nafasi yako. Ni kwa msingi huo watu watakufuata kwa hiari na kukuheshimu sana, ukiwa hai au umekufa.

Tukiyatafakari haya na kuyafanyia kazi, tutaweza kufikia Tanzania tuitakayo mapema.
 
Last edited:
mawazo kama haya tunapaswa kuyalipia kodi kila mwaka maana ni mazuri sana. Mkuu samahani naomba kujua mtazamo wako kuhusu uongozi wa Rais John?
 
Mkuu, kuna changamoto nyingi. Lakini kwa bahati mbaya ulimwengu haujawahi kuwa free from challenges; sembuse Tanzanzania. Aidha, haitegemewi kuwa itafika siku tukaishi bila kubabiliwa na changamoto za kimaumbile na za kibinadamu.

Maoni yangu ni kuwa, badala ya kuumiza vichwa kukariri changamoto tulizonazo au zile zinazojitokeza au kukariri kile kinachotokea na hali kishatokea, tuwekeze kwenye Ku boost ustaarabu wetu kila mtu kwa nafasi yake kwa ajili ya mambo mawili.

1. Tuweze kuchukuwa hatua bora zaidi Ku manage challenges zilizopo na na

2. Kuweza kuchangia kufanya wakati ujao uwe bora kuliko uliopita.
 
Mkuu Sir Khan enzi za uhai wake, Dr. Monroe aliwahi kusema kitu kimoja muhimu sana.

Alisema, what we can do is not wishing for less challenges since it will not work, rather we have to struggle to acquire more wisdom!

Ni kwa namna hiyo tunaweza kufanikiwa.
 
mkuu kwa point zako ninaamini hata kama hauna elimu kubwa ila umeelimika sana kuliko maprofesa wetu baadhi wanywa gongo
 
Mkuu, shukuran sana kwa kunipa moyo, tuungane kuisaidia jamii yetu kuwa na mtizamo bora juu ya maisha na mafanikio kwa ujumla ili siku moja Tanzania iwe moja ya nchi bora zaidi duniani. Inawezekana na ipo siku tutafika tu ndugu yangu.
 
Mkuu nimekuelewa sana tena sana hongera kwa fikra yakinifu

Tatizo watu kama nyie wenye mawazo na hoja zenye kujenga mustawa na mustakabili wa taifa letu ukubwa na kichaa cha madaraka mnabadilika na kuwa mazezeta na magoigoi akili zenu hushikwa na watu wengine

Mifano iko mingi ya aina ya watu wenye kichaa cha madaraka

Azizi Mussa natumaini wewe sio miongoni mwa wenye kichaa cha madaraka Allah akulipe katika yaliyo ya kheri
 
Allahuma' amin Wa anta kadhalika!

By the way usiamini sana mtu, amini na simamia mambo ya msingi. Hiyo ndio pamanent, universal & eternal Shida yetu binadamu tuna udhaifu mwingi na sisi waafrika tuna udhaifu zaidi kwenye namna tunavyojitizama na kuutizama ulimwengu.

Kwa hiyo ukaweka matumaini sana kwa mtu ni hatari maana anaweza kukugeuka.Jiaminishe kuwa wewe ndio unayewajibika na utakaye leta mabadiliko na Kisha anza utekelezaji kwa lile lililo ndani ya uwezo wako
 
Pamoja na sifa zake zote huyu mzee mahatma Gandhi alikuwa mbaguzi dhidi ya watu Weusi.. Alikuwa anaamini toka moyoni kuwa huko Afrika Kusini kwanza ni wazungu kisha wahindi na “washenzi” Waafrika wako chini kabisa… waweza tafuta mtandaoni taarifa zake lakini pia waweza soma hapa:

- The Washington Post
 
Inategemea tu kwamba mtu anaangalia kutokea kwenye angle gani. Hata Nelson Mandela, kuna baadhi ya watu humtizama na kumtaja kama gaidi. Huwa mambo ni mengi lakini bado hoja za msingi zinabaki pale pale.
 
mahatma-gandhi-gandhiji.jpg

Sio kwamba hakuwa na hela ya kula hapana; aligoma kula kama sehemu ya jitihada ya kupigania haki kwa watu wa india. Pamoja na afya yake hiyo iliyotokana na harakati zake za kuwapigania watu, mmoja wa watu aliokuwa akiwapigania aliamua kumuua kwa kumpiga risasi tatu kifuani. Kosa lililomuudhi Bwana Nathuram hata akachagua kumuua mzee wa watu ; Ni jitihada za Mahatma kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya Wahindu na Waislam ambapo muaji aliona kuwa Mahatma kakupaswa kutafuta suluhu na waislam hasa ukizingatia kuwa yeye mwenyewe (mahatma) hakuwa muislam.Kwake Mahtma haki, usawa na utu vilikuwa ni vitu muhimu kuliko kitu chochote, bila kujali anamtetea nani na ujasiri aliokuwa nao katika kutetea mambo hayo ulikuwa ni mkubwa kuliko woga aliokuwa nao dhidi ya kifo.

Kila kiongozi ni mwanasiasa katika level Fulani ila si kila mwanasiasa ni kiongozi na katika mambo ya hatari sana duniani ni kuwa na wanasiasa ambao si viongozi kwa kuwa wanajikuta wakiwa na nguvu nyingi bila mitizamo sahihi. Hata hivyo jambo la kutia moyo na kufurahisha ni kwamba; mtu yoyoye anaweza kujifunza misingi ya uongozi, akaishika, akaifanyia kazi na kuleta matokeo mazuri.

Katika maisha ya mwanadamu, threat kubwa kupita zote ni kifo. Hivyo watu wengi wasio fikiri sawa sawa hupambana kutafuta positions na tittles wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wanapunguza threats zinazowakabili ikiwemo njaa, umaskini, uwezekano wa kufa n.k. Lakini wale wajuao maana na umuhimu wa uongozi; hutumia kila walicho nacho kuhakikisha kuwa wanasimamia vitu vya msingi wanavyo amini kuwa vinaweza kusaidia vizazi na vizazi kuishi kwa furaha na mafanikio. Hawa wao ishu si kupata fedha nyingi au kufa bali wanaishi je, wanachopata wanapataje na wanatumiaje, wanatumiaje mamlaka waliyo nayo na wanakufa wakifanya nini.

Hawa wanaona kitu muhimu zaidi kilichoko mbele yao ambacho kinawapa nguvu ya kukifikia kuliko woga wanaoupata juu ya kifo, achilia mbali vitu vingine kama maslahi. Ndio maana wakati Fulani Mahatma aliwahi kusema “ Uongozi si kutafuta kitu cha kukufanya uishi au kuishi nacho bali kutafuta kitu ambacho utakufa nacho”.

Kwa bahati mbaya; wengi wetu tunaruhusu tamaa ndio zituongoze. Tunashindwa kufikiri kama toka mwanzo kila mtu angeamua kuongozwa na tamaa badala ya fikra na nia njema kwa wengine; dunia leo ingekuwaje? Hatujui kwamba kuna watu ambao wangeweza wakaamua kutowasaidia wengine na wakaishi maisha ya raha mustarehe, lakini wakaamua kujitoa ili kuhakikisha kuwa jamii na vizazi vijavyo vinakuwa na maisha mazuri!? Hatujui kuwa, kuna watu ambao (kwa mfano) walikuwa na kila kitu ila wakaamua kuishi maabara kutafiti chanjo ambazo zilinusuru jamii na magonjwa ambayo yangeweza kuiteketeza dunia huku wakiwa wanasahau hata kula? Hatujui kuwa hata sasa kuna watu au nchi zinaweza kutawala nchi nyingine kulingana na teknolojia na nguvu walizo nazo, lakini hawafanyi hivyo kwa kuwa wanadhibiti tamaa zao kwa kufikiri na kutanguliza ustaarabu?

Ndugu zangu; wale tunaotamani kupata mamlaka, vyeo au wenye ndoto za kuwa viongozi kwenye nchi hii, ni vyema kutambua yafuatayo;-

1. Hata uwe na fedha au mali kiasi gani, hauwezi kula zaidi ya kilo mbili kwa wakati mmoja, na hata ule kiasi gani baada ya masaa machache utasikia tena njaa na hali hiyo itaendelea hivyo hadi utakavyokufa. Kwa hiyo tusiwe impressed na fedha na mali kwenye vitu vya msingi bali tuwe impressed na matokeo ya yale tunayoyafanya.

2. Hata uwe na cheo kikubwa kiasi gani, bado utakula, utalala, na mwishowe utakufa. Pigania mambo yamsingi yatakayosaidia watu wapate vitu vizuri kwenye maisha yao na usipigane kutafuta sifa kwa kuumiza wengine . tumia vipaji na mamlaka yako au kile ulichonacho kwa tahadhari na tafakari matokeo ya kila unachokifaanya.

3. Usiogope sana changamoto unaposimamia mambo ya msingi ambayo yatasaidia ustawi wa watanzania wenzako na jamii ya mwanadamu kwa ujumla. Kumbuka kuwa kifo ndio changamoto kubwa kupita zote inayomkabili mwanadamu lakini hakuna mtu ambaye ashawahi kunusurika kwa kukiogopa na kukikwepa. Kwa namna ya ajabu sana; kadiri unavyokimbia kifo ndivyo unavyoki attract kukukabili. Hivyo usihofie sana kufa bali hofia kufa ukiwa unadhulumu watu wengine au kufanya matendo ambayo hayana maana yoyote.

4. Ishi duniani kwa unyenyekevu kwani sisi binadamu ni viumbe dhaifu sana hata kama tumepata nguvu au mamlaka fulani duniani. Kulikuwa na watu waliokuwa na nguvu sana duniani wengine wakazitumia vizuri wengine wakazitumia vibaya ila leo wote wamelala chini.

5. Jitahidi kwa kadiri uwezavyo kushawishi “Inspire” watu kwenye vitu unavyoviamini na kuwasaidia watu kupata vitu vizuri ambavyo wanavitamani kwenye maisha yao kulingana na uwezo na nafasi yako. Ni kwa msingi huo watu watakufuata kwa hiari na kukuheshimu sana, ukiwa hai au umekufa.

Tukiyatafakari haya na kuyafanyia kazi, tutaweza kufikia Tanzania tuitakayo mapema.

Nimekukubali, tutazingatia
 
Inategemea tu kwamba mtu anaangalia kutokea kwenye angle gani. Hata Nelson Mandela, kuna baadhi ya watu humtizama na kumtaja kama gaidi. Huwa mambo ni mengi lakini bado hoja za msingi zinabaki pale pale.
nakubaliana nawe kuhusu hoja zake..mi namwamngalia kutokea engo ya mtu mweusi...
 
Maendeleo yaliyofikiwa duniani leo ambapo sisi ni wanufaika, hayakufikiwa kwa tamaa bali kwa kufikiri na kujitoa.
 
hili jiwe limelenga jiwe
 
Mkuu, shukuran sana kwa kunipa moyo, tuungane kuisaidia jamii yetu kuwa na mtizamo bora juu ya maisha na mafanikio kwa ujumla ili siku moja Tanzania iwe moja ya nchi bora zaidi duniani. Inawezekana na ipo siku tutafika tu ndugu yangu.
jiwe linaleta mafarakano nchini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom