Tafakuri yangu ya Leo…..Historia ya mapinduzi ya zanzibar iandikwe upya!

Nova Kambota

Member
Nov 12, 2009
62
1
http://novadream.blog.com/index.php...toria-ya-mapinduzi-ya-zanzibar-iandikwe-upya/

Leo tunapoadhimisha kumbukumbu ya mapinduzi ya zanzibar ya tarehe 12 january 1964 kuna haja ya dhati kabisa kujihoji usahihi wa historia ya mapinduzi hayo kwa maana ya nani alihusika, nani alikuwa kiongozi wa mapinduzi hayo ili mwishowe tupate historia kamili ya visiwa hivyo vya karafuu kuliko hivi sasa ambapo historia ya mapinduzi hayo ina utata mkubwa ambao umepelekea kuandikwa vitabu mbalimbali na wanahistoria mbalimbali huku mjadala mkuu ukiwa ni nani hasa shujaa wa mapinduzi hayo kati ya professa Abdurlhaman Babu, Karume na John Okello.
Baadhi ya vitabu vya historia vinamtaja rais wa kwanza wa Zanzibar na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndiye hasa kinara wa mapinduzi hayo ya januari 12


Pia kuna baadhi ya vitabu vya wanahistoria wengine wanaodai kuwa mganda John Okello kuwa ndiye hasa aliyeongoza mapinduzi hayo huku mwenyewe wafuasi wake wakimpachika jina la Field Marshal Okello kutokana na ukakamavu wake, tena wanahistoria hawa wanatumia ushahidi wa picha iliyopigwa siku ya mapinduzi ambayo inamwonyesha Okello ndiye pekee aliyevaa kiaskari kuonyesha kuwa yeye ndiye kiongozi.


Lakini hiyo haitoshi kuonyesha kuwa kuna msuguano wa kihistoria kwenye visiwa hivyo ambavyo ni maarufu kwa zao la karafuu
kuna vitabu vinamtaja professor Abdurlhaman Mohamed Babu aliyekuwa kiongozi wa chama cha Umma party ndiye hasa kinara wa mapinduzi hayo

Lakini bora ingekuwa hivi tu ingevumilika lakini sasa mwaka 2010 tumeshuhudia kuchapwa kwa kitabu cha Kwaheri ukoloni kwa heri uhuru , huku kikituacha hoi wapenda historia wengi kwa jinsi mwandishi wa kitabu hiki Dr kassan alivyoweza kuibua hoja nzito za kihistoria ambazo bila shaka zimetuonyesha kwa kiasi gani tunahitaji historia sahihi ya visiwa hivyo ili tuwarithishe watoto na wajukuu zetu kuliko hivi sasa ambapo ni kama tunaficha ukweli au tunapotosha historia makusudi. Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Desutchwelle Dr Kassan alisisitiza kuwa kwa takribani nusu karne historia ya Zanzibar imepotoshwa kwa makusudi na watawala huku akisisitiza kuwa kitabu chake hiko ni kwaajili ya kuandika historia ya kweli ya visiwa hivyo akaenda mbali zaidi kwa kutaka jamii isimchukulie kama amekuja kufukua makaburi bali amekuja kuweka maua juu ya makaburi.
Haya ni baadhi tu ya mambo ya msingi kabisa yanayoonyesha kuna ulazima tena wa haraka wa kuandika upya historia ya mapinduzi ya zanzibar. Hivyo tunaposherehekea mapinduzi ya zanzibar siku ya leo ni muhimu pia tukakumbuka jukumu letu la kuwa na historia sahihi ya mapinduzi hayo ambayo itakuwa ni kumbukumbu muhimu kwa vizazi vijavyo.
Nova Kambota
Mzumbe university Morogoro
0717 709618 au 0766 730256
novakambota@gmail.com
novadream.blog.com

 
Back
Top Bottom