Tafakuri yangu ya leo; Edward Lowassa sema neno moja tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakuri yangu ya leo; Edward Lowassa sema neno moja tu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KAMBOTA, Jun 11, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  View attachment 31806
  Na Nova Kambota

  Ingawaje mimi sijawahi kusoma maswala unajimu wala utabiri naomba leo nitabiri mambo matatu kuhusu maisha ya waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Bw Edward Ngoyai Lowassa, kwanza nashawishika kuwa Lowassa ametoka familia ya kichifu au wazazi wake walikuwa matajiri, pili Lowassa ni msiri sana na tatu Lowassa anaishi kwa ahadi kuliko nyakati.

  Kwa kawaida watoto wa kichifu au wa familia za kitajiri ni waoga tena wapo tayari hata kutoa fedha mradi wasikumbwe na dhoruba hata kwenye shule za bweni watoto wa kitajiri ni waoga kwelikweli, kwa jinsi Lowassa asivyopenda matatizo “ajali kazini” hapendi “kupambana jino kwa jino” yaelekea ni tatizo la kimalezi kuliko kisiasa, malezi ya Lowassa aliyolelewa katika familia yake ambayo ni ya kitajiri yamemfanya kuwa mwoga sasa amebaki kulalamika kuwa “anaonewa”.

  Chukulia sakata la Richmond ambalo lilimwondoa Lowassa kwenye kiti cha uwaziri mkuu, kamati ya bunge iliyoongozwa na Mwakyembe ilileta ushahidi mzito dhidi yake kwa kushindwa kusimamia mawaziri wake vizuri na Lowassa alipotoa ile hotuba yake ya …”nimetafakari sana , nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana kwa heshima ya chama changu…………………akaingizia na tuhuma kuwa kamati ya Mwakyembe imelidanganya bunge na akazidi kuongeza utata kwa madai kuwa tatizo ni uwaziri mkuu lakini yote haya yamebaki siri kubwa hayuko tayari kusema kinagaubaga na kutwambia kuwa tatizo lilikuwa uwaziri mkuu au kweli kamati ilidanganya bunge.

  Halafu yaelekea Lowassa ni mtu anayeishi kwa ahadi kuliko kusoma alama za nyakati , tangu mwaka 1995 iliwahi kuelezwa kuwa Kikwete na Lowassa ni maswahiba wakubwa tena ikaelezwa kuwa iwapo mmoja wapo ataukwaa urais basi mwingine angeteuliwa kuwa waziri mkuu na hili halikupita kwani kufuatia ushindi wa “sunami” wa kikwete wa mwaka 2005 Lowassa akateuliwa kuwa waziri mkuu tena nakumbuka ile hotuba ya Kikwete siku ya uteuzi wake mara baada ya bunge kupitisha jina lake “mtaani watu wanasema ooh Lowassa ni rafiki yangu ni kweli rafiki yangu ila namfahamu Lowassa ni mtendaji mahiri asiyetetereka” haya yalikuwa ni maneno yake Kikwete sasa yaelekea kuwa si hivyo tu bali pia Lowassa aliahidiwa ndiye atakayekuwa mrithi wa Kikwete 2015 lakini licha ya yote yaliyomkuta naona bado kalala kwenye usingizi wa “fofofo” anategemea ahadi badala ya kuenenda kadri ya alama za nyakati zinavyomtaka.

  Kama mwandishi mahiri wa habari za uchambuzi nchini maarufu kwa jina la Mwanakijiji alivyomshauri Lowassa kupitia makala yake iliyokuwa na kichwa cha “Edward Lowassa uchaguzi ni wako” , katika makala yake hiyo Mwanakijiji anamtaka Lowassa kurudi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa na mimi narudia tena kufanya siasa za chinichini kama anavyofanya Lowassa hivi sasa haimjengi chochote bali inabidi arudi rasmi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa tena atolee matamko mambo mazito bila woga, nashindwa kuelewa Lowassa anaogopa nini? kwa maana ushahidi wa nguvu na ushawishi wake unaonekana waziwazi mfano licha ya yeye kujiuzulu sambamba na Msabaha na Karamagi hawa wenzake wote “tupa kule” hawasikiki tena ila yeye bado anasikika kwenye vyombo vya habari (japo si kwa mema).

  Bado hatujasahau vuta nikuvute kati ya Mwakyembe na Lowassa kiasi kwamba Mwakyembe aliwahi kuwapa changamoto kina Lowassa ili kupima iwapo wanakubalika kweli basi yeye na wao waende kuhutubia pale sokoni kariakoo kisha waone wananchi watafanyeje? Kama kweli Lowassa anajiamini tulitegemea ajitutumue hata kujibu au kufanya chochote kuonyesha kuwa anakubalika lakini wapi! Lowassa alikaa kimya hii maana yake nini? na inatafsiri gani? nini hitimisho la mvutano huu wa Mwakyembe na Lowassa?

  Mvutano kati ya Samwel Sitta na Lowassa ulizua ya kuandikwa, kuna baadhi ya watu wakadai kuwa Lowassa aliposema kuwa …”tatizo ni uwaziri mkuu..” alikuwa akimaanisha mvutano wake na Sitta na hili likapewa uzito na kauli za Andrew Chenge “swahiba wa Lowassa” kuwa Sitta alitumia bunge kujeruhi wenzake kisiasa lakini licha ya yote haya Lowassa hakutia neno yeye kaka kimya, watu wanapotaka kufahamu uwaziri mkuu wake ulikuwa na uhusiano gani na Sitta? yeye “anajibu kisiasa badala ya kujibu ukweli” kuna nini hapa? Anamwogopa nani?

  CHADEMA katika moja ya mapambano yao dhidi ya ufisadi waliwahi kumhusisha Kikwete na ufisadi tena baadhi ya magazeti yakadai kuwa iweje waziri mkuu Lowassa ahusike na Richmond kisha Kikwete ambaye kimsingi ndiye bosi wa waziri mkuu asihusike? Haya ni maswali ya msingi ambayo Lowassa hakupaswa kukaa kimya alitakiwa atwambie iwapo Kikwete alihusika au la? Na sio kutwambia tu bali aseme kwa nukta na mantiki kiasi tukipima maneno yake tuone yana ukweli na yamejengwa kwa mtiririko wa “logic”.

  Sasa kuna operation ya kujivua gamba ambayo ilielezwa kuwa mmoja wa walengwa alikuwa ni Edward Lowassa lakini sasa operation hii imekuwa butu kwa maana nyingine imeshindwa na watu wanamlaumu Kikwete kwa kushindwa kuisimamia, wengine wanahoji ingekuwaje kama angeisimamia? Lowassa angeathirika kwa kiwango gani? na je kwa kutoisimamia Lowassa kanufaika kwa kiwango gani? na je Kikwete anamwogopa Lowassa? Au Lowassa bado ni swahiba wa Kikwete? Haya ni maswali ya msingi na hakuna mtu mwingine wa kuyajibu zaidi ya Lowassa hapaswi kukaa kimya.

  Lowassa anapaswa kuingia kwenye siasa za malumbano na minyukano bila kusita hata ikibidi kumjeruhi “swahiba” wake Kikwete potelea mbali ajali kazini hata ikibidi kulipua msuguano tena baina yake na Sitta na Mwakyembe sawa tu lakini ukweli pekee ndiyo utakaomweka huru Lowassa vinginevyo anajimaliza kisiasa kiasi kwamba hata kwenye historia ya taifa hili hatokumbukwa tena. Lowassa asiishie kusema pembeni kuwa yeye ni msafi anaonewa tu inabidi adhihirishe kauli yake kwa kuwataja wachafu pasipo kusita vinginevyo yeye ndiyo mchafu na anawasingizia wenzake kwa kusema wanamwonea.

  Lowassa inabidi ajiamini kwani yeye si ndo alikuwa injinia mkuu wa mtandao uliomwingiza Kikwete 2005 kwa maana nyingine maadui Lowassa aliwapata wakati akimtetea Kikwete sasa anaogopa nini? kwa maana nyingine maadui wake pia ni maadui wa Kikwete hivyo asiogope sana! Kwa maana nani ana nguvu za kumshinda kiongozi wa nchi? Na kwa upande mwingine Kikwete na chama chake anachokiongoza CCM wanapaswa kuweka hadharani uchafu wa Lowassa kuliko kuendelea na minong’ono, mzee Chiligati, Nape Nauye na Mukama wamkane waziwazi Lowassa na Kikwete avunje urafiki na Lowassa iwapo kweli anaamini Lowassa ni “mchafu tena anamharibia kwa wananchi”. Tunataka Mwakyembe, Sitta, Chenge na Rostam waseme ukweli kuliko kumung’unya maneno, tunataka ukweli “kindakindaki”

  Tumechoshwa na siasa za mipasho na vijembe , hatutaki kusikia upuuzi wa “hao mafisadi” tunataka tuambiwe fulani na fulani ni mafisadi, hatutaki kusikia “mimi ni msafi” bali sina kosa kwasababu moja mbili tatu, hatutaki upuuzi wa “ni lazima CCM ijivue gamba” bali tunataka kusikia “fulani na fulani wamekiuka kanuni za chama sasa tunawatimua na kuwafilisi mali zao” , haya ndiyo matakwa ya watanzania.

  Mtu pekee ambaye anaweza kutufikisha huko ni Lowassa , Lowassa ni lazima azungumze yeye ni “kichocheo” katika hili, aseme neno moja tu ! na alisimamie pasipo uwoga “UKWELI” huu ndiyo utamweka huru, atwambie bila kificho tena waziwazi basi mlolongo utafata kila mtu atasema ukweli, Kikwete, Chenge, Sitta, Rostam na Mwakyembe wote watasema ukweli mtupu na iwapo kweli Lowassa atajitokeza hadharani na kusema pasipo kumung’unya basi uamuzi wake huo usipokelewe kama amekuja kufukua kaburi bali atazamwe kama amekuja kuweka shada la maua juu ya kaburi…..A Luta Continua!

  Nani bora anayeandika kwa taaluma yake au mimi nayeandika nachokiamini?
  Nova Kambota Mwanaharakati,
  Nipigie; 0717 709618 au +255717 709618
  Niandikie kwenda;novakambota@gmail.com
  kwa habari zaidi za uchambuzi nitembelee;www.novakambota.com
  Tanzania, East Africa,
  Jumamosi 11, Juni 2011.   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hauziki soko la taifa huyo? jaribu tena soko la monduli
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good tea. Ukosawa sie yetu macho ipo siku video itakuwa nzuri tu maana ukweli according to sofia lion ccm wote mafisadi, mwenye kumwaga mboga wengine watamwaga ugali karibu sana kimbota well said
   
 4. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  KAMBOTA, EL ni mzigo usiobebeka. Kuna gazeti liliandika habari za mwanae Freddy kuhamsiha mihela za kununulia nyumba London, labda wanajitayarishia makazi ya baadae.
  Hata afanyeje hatumtaki. Porokwa alitaka kumwaga mambo akapozwa na pesa za 'Alfa'
   
 5. Mvua Ya Kiangaz

  Mvua Ya Kiangaz JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Imani yangu na naamini........ufisadi nchi hii umeanza zamani sana japo mwalimu alijitahidi kupambana nao lakini mafisadi walimzidi kete wakamuondosha kipenzi chetu sokoine, hivyo basi lowasa si kielelezo cha ufisadi kwa kiwango chochote kile katika nchi yetu,maamuzi ya kuipigia debe richmond ni maamuzi ya kawaida tu ya utekelezaji wa majukumu yake kama waziri mkuu,jiulize kama richmond ingefanikiwa kwa kiwango kilekile ktk utekelezaji wa mkataba wake...lawama ingetoka wapi??????????


  Lowassa ni jembe na ndio maana kelele nyingi,tatizo la nchi yetu waandishi wetu ni mambumbumbu,akili zao finyu katika kuchambua mambo,wanajipendekeza kwa baadhi ya wanasiasa(mfano kuna wengine baada ya uchaguzi wa 2005 walipewa ulaji ikulu) hivyo wanashindwa kuwahabarisha wananchi juu ya ukweli wa mambo ktk swala husika,mathalani,lowassa fisadi:ufisadi wake ni upi? Ni kuipigia chapuo richmond??? Na je aliwajibika au kuwajibishwa? Kama ndio ufisadi huo wa kimaamuzi(kama anavyotuhumiwa)utaendelea miliele au nini hukumu yake?

  Pamoja na hayo,inamaana lowassa hakuna lolote ambalo anastahili japo kasifa kidogo? Kwani si lowassa huyu alievunja mkataba na city water watu wote tukamshangilia,hii inamaana kama city water wangeshinda tuzo icc kama dowans tungemgeuka???,je si lowassa huyu aliekaidi makubaliano ya misri na wakoloni juu ya matumizi ya maji ya ziwa victoria kwa kusaini na kusimamia mradi wa maji kutoka ziwa victoria hadi shinyanga???
  Nachelea kusema kuwa watanzania tumeathirika na siasa za maji machafu,ambapo ili kumshinda mwenye nguvu na ushawishi ni kumpaka matope tuuuu(ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya) kwa kutumia vijarida na magazeti ya upande mmoja.....................lowassa wewe ni jembe,tunatambua serikali ya awamu ya nne ilivyopwaya baada ya wewe kujiuzuru,usikae kimya,rudi chukua nafasi yako ktk jamii ili wenye maono na akili timamu (sio za kuazima) wakusemeee.

  Lowassa sema neno moja tuuuuuuuuuuuuuuuu kieleweke.
   
 6. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Nani wa kumfunga paka kengele!!!!!!!!!
   
 7. K

  KAMBOTA Senior Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  yapi hayo yatajiri? kwani kati ya JK na Lowassa nani anamwogopa mwenzake?
   
 8. K

  KAMBOTA Senior Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ajabu sana aisee! teh teh teh mitandao inazidi kubomoka tu nani aliwatuma kuunda mitandao?
   
 9. K

  KAMBOTA Senior Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaelekea movie ndo inazidi kuwa tamu ni vuta nikuvute kati ya kubwa la maadui na Staa wa filamu ila anyway lazima kubwa la maadui afe tu sasa sijui itakuwaje?
   
 10. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni upuuzi kumtetea mtu asiye na mvuto katika jamii baada ya kuchafuka,wanaomtaka aseme wanataka aseme nini,kwani hamuoni anavyoivuruga ccm ,mara leo vijana wanagombana arusha,mara pwani,nadhani inatosha tanzania si nchi ya mtu,ndio maana baada ya nyerere akaja mwinyi-mkapa na sasa kikwete then atakuja Rais wa supprise sio wa kujiandaa,ndio maana nchi inayumba kwa kuwa Rais aliyejiandaa kuingia madarakani na watu wake,watu wenye sifa wanaachwa wanachukuliwa wapambe
   
 11. K

  KAMBOTA Senior Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  unachekesha sana wewe ndugu yangu, yaelekea ndo kwanza umejiunga na CCM , sasa nani anaivuruga CCM? mwanzilishi wa mitandao ya 2005 au Lowassa? mvuto ndiyo nini hapa? mbona kuna mtu anaongoza nchi na hana mvuto kwa watanzania? acha ushabiki wewe embu toa hoja za msingi mkuu, au hujasoma gazeti kibaraka la chama chako CCM lililohoji tatizo ni Lowassa au urais 2015? na lile lingine lililouliza tatizo ni Lowassa au udhaifu wa JK?
   
 12. Mvua Ya Kiangaz

  Mvua Ya Kiangaz JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33

  Hivi umekuja lini mjini??? unajua unachokisema au ndo walewale fata mkumbo?????Kama unachangia mawazo ya wanamme toa hoja zenye mashiko na si mahaba ya chama,ushabiki wa kambi au gazeti la udaku wa siasa, fanya tafakuri na uchambuzi wa hoja sio kubuni vitu au kuamini kile unachoaminishwa na magazeti.............au unataka magazeti yakupelekechaka kama yalivyowafanya watanzania kwenye uchaguzi wa 2005??? au umesahau mlipochagua u-hendisamu wa mtu badala ya mtu???kitu gani kilichowafanya watz woooote mvutiwe na rais wenu kama sio magazeti.............................ENDELEA KUAMINISHWA AGENDA ZA WATU
   
 13. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  lazima afanye kazi ya ziada kurudi kwenye chati kwa sababu mtanzania wa kawaida kuja kumshawishi
  kwamba Rowasa ni msafi eti ni kashfa tu kazi ipo,angejisafisha siku ile ile ili ijulikane nani ni nani
  kwa sasbabu kamua kuuvaa mkenge aendelee kuvaa tu............,lakini siasa za bongo zinafurahisha.
   
 14. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,798
  Likes Received: 1,044
  Trophy Points: 280
  mkuu umejipanga!
   
 15. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,151
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Kinachojiri ni nani anacheza kete gani na wakati gani.Hadi sasa lowasa muda unamtupa mkono!Wanaogopana, lakini JK kashika mpini, EL, Kashika makali!
   
 16. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ndo faida ya kuwa na vijana ambao ni wasomi. Big up sana Novakambota kwa mada yako nzuri umenesha ni kiasi gani ulivyo mzalendo. MUNGU AKUBARIKI.
   
 17. Mizinga

  Mizinga Senior Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Big sana kaka. Unajua watz wengi ni masharo..... Sema mkuu.
   
 18. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe huoni kuwa JK anamuogopa EL!?, kama Richmond ilikuwa mzigo wa kuulizwa ni Sita na Kikwete kwani Sita ndiye hakuishauri serikali vizuri wakati akiwa boss wa TIC. Kumbuka kuwa Richmond haimuhusu EL kabisa kwani wakati inapewa mikataba yeye hakuwa anahusika= taarifa ya mwakyembe niyakupika.
   
Loading...