Hivi mpaka leo kuna mtu anajifanya hawafahamu hao wanaoitwa "WASIOJULIKANA"? Mimi nafikiri ni sifa tu watu wameamua kuwapa. Ukweli ni kwamba wanajulikana kwa sababu ya tabia za kuogopa binadamu wenzetu kuliko aliyetuumba basi tumeamua wawe hawajulikani hata kama wanajulikana.
Katika jambo linaloniumiza kichwa sana ni binadamu kama wewe kucheza na uhai wako kama vile anacheza na mpira wa kitenisi. Yaani mtu unaweza kukatika mguu binadamu akakutengenezea mguu wa bandia. Ikawa huna nywele kichwani ukavaa wigi. Afya ikadorora au ukaumwa ukatumia dawa. Lakini uhai wa binadamu ukiondoka ndio basi hakuna kiumbe yoyote au kiumbe yoyote hapa duniani anaweza kukurudishia uhai wako. Hivi inakuwaje mtu anathubutu kuutishia uhai wenu au kukutoeni uhai, wa kwanza, wa pili, wa tatu, ... bado tupo tupo tu km vile kuku kachinjwa huyu kesho atachinjwa mwingine na bado tupo tupo.
Kwangu mimi watu hawa wakija kuna option 3 tu.
1. Waondoke na mimi nikiwa maiti, hapo waliponikuta hawawezi kuondoka na mimi nikiwa mzima hata siku moja.
2. Wabaki wao wakiwa maiti, au
3. Waondoke wao wakiwa wazima au wamejeruhiwa na kuniacha mimi mzima au nimejeruhiwa.
Nasema hivi kwa sababu sheria za polisi zipo wazi kabisa za ukamataji. Ukamataji usiofata taratibu kwa sasa ni kuendelea kuwalinda hao wanaitwa "WASIOJULIKANA". Hivi inakuwaje jeshi la polisi linashawishi watu kufuata sheria bila shuruti wakati wao ndio wa kwanza kutofuata taratibu zao wenyewe hasa za ukamataji. Hivi kweli unaniambia kuanzia sasa upo chini ya ulinzi nakuuliza kwa kosa gani unanijibu kosa utalijulia kituoni sasa umeja kunikamatia nini? Kama unasema kosa nitalijulia kituoni wewe umekuja kufanya nini si ungenipigia simu au kunipa taarifa nikaja huko kituoni halafu nikajua hilo kosa langu.
Unajua sisi binadamu wakati mwingine ni wajinga sana. Unakuta mtu anafurahia mwenzake kutekwa na kuuwawa au kuteswa kana kwamba yeye hatakufa. Wakati mwingine ni bora huyo anaepata mateso kwa kupigania haki yake kuliko wewe uwe kitandani unateseka kwa UKIMWI tu ambapo ungeweza kuuzuia kwa kutumia kondom ya bure. Pamoja na elimu yote iliyotolewa ya kujikinga na maradhi hayo bado kwa ujinga wa kutojitambua unauvaa lkn haraka kufurahia wenzako kupata mateso na kufa.
Pamoja na wengi kutoa sababu mbalimbali kwa nini watu wanatekwa. Fikra yangu mimi inaona kwamba hawa watu wanataka sisi tuwe hivi:-
1. Tuzoee hii hali ya watu kutekwa tuone ni kitu cha kawaida, wao waamue wakurudishe hai, majeruhi au umekufa. Ndio maana jeshi la polisi kila mara linasisitiza mtu akitekwa tusikimbilie kusema hivyo. Maanake ni kwamba mtu atekwe tukae kimya.
2. Tusijali na kuuthamini uhai wetu kama ambavyo hawauthamini. Yaani wanatuona sisi ni kuku tu wanaweza kutufanya kitoweo muda wowote pale wanapotaka.
3. Wanataka kutupangia nini cha kuongea na nini usiongee, nini cha kufanya na nini usifanye hata kama ni sheria. Yaani kwa kifupi wao ndio iwe sheria wanapanga wao kila kitu. Hivi hawajui zama za utumwa zimeshaisha?
4. Tusiwe na uthubutu na ujasiri wa kudai haki yako yoyote ile.
5. Kutia watu hofu kuelekea kwenye uchaguzi wa 2020 na nyinginezo. Kwa hili uwe mgombea au iwe umejitayarisha kwenda kumchagua mtu ambae wao hawamtaki.
Je wewe una tafakuri gani?