Mungu alimuumba Adam kisha akampulizia pumzi ya uhai.Kwa kweli maswali yako haya Askofu hapendi kuulizwa maana yanafikirisha sana ila pia hujazungumzia ile kauli ya alichounganisha Mungu pinadamu asitenganishe hio sentensi Askofu anaitumia sana kwenye kuelezea mada ya Ndoa kwamba mfungishaji wa ndoa wa kwanza alikua ni Mungu mwenyewe
Lakini pia Askofu ataenda na kukwambia Yesu alisema Mungu ni Upendo yaan unapendana na mwenzio ndio yupo katikati yenu kuudumisha Upendo, ataenda mbali zaidi kwamba pamoja na kwamba hakuwasamehe ila hakuwaacha alichofanya aliwaondoa kule kuliko na Malaika
Askofu ataenda mbali na kukwambia kabla ya mwili kwanza iliumbwa Roho, kwa hio ujue tofauti ya Mwili na Roho, Mungu anaishi Rohoni sio Mwilini, hayo ni maelezo ya Askofu sio mimi
Hivyo alianza kuumba mwili kisha ndio aka upa uhai ambaye ni roho.
Roho hukaa mwilini na siyo moyoni.
Inasema Mungu alisema na tumuumbe mtu kwa mfano wetu na wakamuumba Adam, kisha wakampulizia punzi wakampa uhai naamini mwili ni utupu bila pumzi ya Mungu.
Sijui Adam ni jina la ubatizo au ndio jina la asili ila twende hivyo hivyo.
Na ile pumzi ndiye roho na ndio uhai utwaliwao na kuucha mwili mauti yanapofika.