Tafakuri ya Hekima

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,655
Tunapokua ni lazima ukuaji wetu uambatane na hekima na busara. Kwasababu binadamu sio ukuaji wa mwili tu bali pia ukuaji wake wa kiakli.

Ukuaji wa binadamu sio kurefuka tu au unene au kutoka utoto , ujana na uzee kwa mtizamo wa mwili pekee yake kama mti unavyokua.

Binadamu anahitaji maarifa kuongoza maisha yake. Ni kwa kukosa maarifa kwetu maisha yetu mara kwa mara tunayaweka hatarini.

Ni lazima tukue kiakili pia. Ni lazima tukue tukiwa na busara. Na tutafute kadiri ya uwezo wetu maarifa na busara ambayo itatufanya tuishi vyema.

Vitu viwili ambavyo nimejifunza ambavyo ni muhimu sana pengine kuliko hata dhahabu, Upendo na busara. Hivi vitu viwili ni muhimu sana kuvitafuta kadiri ya uwezo wetu.

Katika maisha yetu ya kila siku tunatakiwa kufanya maamuzi na tunahitaji busara kufanya maamuzi yenye hekima. Maamuzi yetu mara nyingi yanafunikwa na ubinafsi wetu na kushindwa kuangalia upande wa pili. Kushindwa kuangalia madhara ya maamuzi yetu hapo baadae na kuangalia faida ya hapo kwa hapo. Lakini hii sio njia ya mtu mwenye hekima.

Mara kibao tumetoa sadaka familia zetu kwa kutimiza haja zetu za kipindi kifupi na kuweka rehani stability za familia zetu na upendo wa familia zetu. Ambao ni chachu ya ustawi wa familia yeyote ile na umoja wake.

Hivyo hivyo katika ngazi ya utaifa wetu. Tunaiba, tunakula rushwa hatutii sheria za nchi. Miongoni mwetu katika taifa hili ni wachache sana wenye uwezo wa kujiita raia bora na watiifu kwa taifa lao. Ambao wanatenda yaliyo sahihi na kuwajibika kama ipasavyo.

Wengi wetu ni wabinafsi na mawazo yetu kuhusu utaifa wetu yanapita mara chache sana katika tafakuri zetu. Lakini tufahamu kwamba maendeleo yetu yanategemea kila mmoja wetu. Na kila mmoja wetu anapaswa kuchangia katika maendeleo na umoja wa taifa lake. Tunafikiria zaidi kuhusu ubinafsi wetu kuliko jamii zetu na taifa letu. Lakini tutambue kwamba tunategemea taifa kwa maendeleo yetu binafsi pamoja na ulinzi wetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom