Tafakari yangu ya pasaka

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Heri ya Pasaka WanaJF,

Kwa muda nimekuwa mfuatiliaji wa jukwaa hili bila kuchangia jambo lolote.Pamoja na ukweli huu leo imenibidi niandike mistari michache juu ya tafakari yangu wakati nikisherekea sikukuu ya pasaka.

Ndugu zangu, nchi yetu kwa sasa ina shida moja kubwa sana,USHABIKI WA KIPUMBAVU.Hatuko makini kwenye mambo yanayohitaji umakini.Wananchi waliowengi ikiwepo viongozi wanapenda kudandia na kushabikia mambo ya kipuuzi na kuacha yenye mantiki.Vibaka na matapeli wa kisiasa wanapewa nishani za kiushujaa kulinda status quo na kupuuza watu wenye fikra,maono na uzalendo juu ya taifa hili.Wanatumia fikra zilizoshindwa kutatua changamoto za nyakati.Watu wenye masiharamasihara,kejeli,wasio na chembe ya busara ndio watu wa maana na ndio madereva wa Taifa hili.

Wanasiasa waliowengi wa nchi hii wamejenga mipaka ya kifikra kulinda ufalme kwa kutumia maneno rahisi kwa mambo yanayohitaji tafukuru ya kina.Mchakato wa katiba ni moja ya kielelezo kikubwa cha udhaifu mkubwa wa kifikra.Uhalali na ushindi wowote wa kisiasa unatokana na nguvu ya hoja.

Inahitaji moyo wa uzalendo,ujasiri,uthubutu na ushawishi wa hali ya juu kubadilisha fikra za viongozi na wananchi kutambua mwelekeo wetu kama taifa bila kujali itikadi zetu za kiitikadi.

Nguvu yetu ni UMOJA na UTHUBUTU
Mbelwa Germano
 
Back
Top Bottom