Tafakari ya leo; Hakuna mtu ambaye ni self made

Tafakari ya leo; Hakuna mtu ambaye ni self made

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,914
Reaction score
3,437
Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?

Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka ubora kwenye kile ambacho tunafanya.Kumbuka muda wa leo hautorudi tena, hivyo tumia muda wako vizuri rafiki.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu dhana ya SELF MADE, au KUJITENGENEZA MWENYEWE.
Wapo watu wamekuwa wanajiita SELF MADE MILLIONAIRE,
wengine SELF MADE BILLIONARE
na wengine SELF MADE ENTREPRENEUR
Japo hakuna mtu anaweza kumzuia mtu kujiita anavyotaka kujiita, kujiita SELF MADE SIYO KWELI.
Hakuna mtu yeyote ambaye ni self made, hakuna mtu yeyote ambaye amejitengeneza mwenyewe.
Hata kama umetoka kwenye hali ya chini kabisa, hukupewa chochote kifedha au kikazi, na umepambana mwenyewe mpaka kuwa tajiri, bado huwezi kujiita self made.

Kwa nini kujiita self made ni kujidanganya na kiwadanganya wengine?
Kwa sababu...
Kuna wakati ulikuwa huwezi kula mwenyewe, watu wakakulisha,
Kuna wakati ulikuwa huwezi kujisaidia mwenyewe watu wakakuwezesha kuondokana na uchafu wako,
Kuna wakati ulikuwa huwezi kuongea watu wakakufundisha kuongea,
Kuna wakati ulikuwa huna mteja yeyote, watu wakaja na kuwa wateja wako,
Chakula unachokula leo hukwenda shambani ukalima mwenyewe, ukavuna kisha ukaja kupika mwenyewe.
Nyumba unayoishi leo, hukuchukua mchanga, tofali na sementi wewe mwenyewe na kuijenga.
Usafiri unaotumia leo hukuutengeneza wewe mwenyewe.
Nchi unayoishi leo, hukuitengeneza wewe mwenyewe...

Sasa unaposema self made unamaanisha nini?
Kujiita self made ni ubinafsi na kusahau juhudi za wengine ambazo wameweka kwenye maisha yako.
Hata kama ulitupwa na kutekelezwa, bado wapo watu waliokusaidia kufika hapo ulipo sasa, usijisahaulishe.

Ufanye nini?
Wewe rafiki yangu, nakusihi sana usije kusimama mahali na kujiita wewe ni SELF MADE CHOCHOTE, hakuna kitu kama hicho.
Furahia mafanikio yako, lakini pia kumbuka kuna watu wengi wameweka juhudi zao kukufikisha hapo ulipo. Usiwabeze.

Nakutakia siku njema sana.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
www.makirita.info

N:B Karibu kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA tujifunze zaidi kila siku. Tuma ujumbe wenye neno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253.

Karibu sana.
 
Asante kwa ujumbe mzuri watu mada za kuelimisha kama hizi huwa wanazpita tu ndio maana wanaofanikiwa ni wachache mada zisizo na maana au faida ndio huwa znawachangiaji wengi waTz tubadilike
 
Go and read carefully, ukiwa hujalewa, what is SELF MADE Millionaires or Billionears..!!

Stop bringing your own false meaning...!! and you keep explaining that false meaning of yours..

Kwa hili nakupa.. XXX 00%
 
Go and read carefully, ukiwa hujalewa, what is SELF MADE Millionaires or Billionears..!!

Stop bringing your own false meaning...!! and you keep explaining that false meaning of yours..

Kwa hili nakupa.. XXX 00%
Nobody is self made, no matter what self made means, NOBODY.
 
Back
Top Bottom