Tafakari: Mwanaume hupaswi kuwa na tabia ya kususa au kununa kwa mkeo, ni hatari sana

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Kama huna uwezo Wa kuoa bora uache!
Nanyi wanawake tambueni ya kwamba siyo kila mwanaume anayekutongoza ana uwezo wa kuoa!

Ile kauli ya kila mwanaume anayekusemesha unamuuliza utanioa au utanichezea, ni moja ya kauli zilizoanzishwa na mwanamke mjinga zaidi duniani!

Kumbuka mwanaume kwa mwanamke ni kichwa ndani ya nyumba, atakayefikiri badala yako, atakaye amua badala yako, atakayekupa heshima n.k

Chanzo cha matatizo mengi yakiwemo mauaji kwenye familia ni kununiana/kususa!
  • Mwanamke hajakuaga bahati mbaya akirudi unasusa kula.
  • Mwanamke kachelewa kupika unasusa.
  • Kasemeshwa njiani unaona basi unasusa.
  • Kapigiwa simu bahati mbaya umeona unaamua kususa!
KUSUSA, KUSUSA, KUSUSA!
Ni moja ya kosa kubwa sana ndani ya nyumba kwa mwanaume hupaswi kulijaribu kamwe!

KISA
Jamaa mmoja aligombana na mke wake akaamua kususa (akamnunia mkewe)

Mke wake alijaribu kujibebisha kwa mumewe lakini wapi, hadi mke alipoamua kumvalia kanga moja iliyoandikwa "Ukisusa wenzio wala"

Jamaa akamaindi zaidi akaenda kumuita rafiki yake ili aje amsaidie kumkanya mkewe; Waliporudi wakamkuta mke huyo kabadili kanga Imeandikwa " Umdhaniae rafiki ndiye adui yako"

Jamaa akachukia sana, akaona ataua mtu akaamua kusafiri wiki kadhaa na simu akazima kabisa, siku aliporudi akakuta mkewe kavaa kanga inasomeka " Kuliko kiozee ndani bora kumpa jilani" 😂😂

KUSUSA NI MOJA YA UJINGA WA KUTOJITAMBUA MWANAUME

Mwanaume hupaswi kususa wala kununa; Unachopaswa kufanya kama mwanaume ni kukanya FULL STOP! Halafu maisha yanaendelea!

Hupaswi kabisa kuchelewa kumkanya mkeo, maana ukichelewa siku ndo umkanye atakuuliza mbona siku zote nafanya hivyo husemi au umepata mwingine?!

Unaponuna na kususa ujiandae kuchapiwa

IMG_20191027_133615.jpg
 
Mwanamke nae akiona anasuswa ajitafakari si rahisi sisi kususa kilicho kitamu,hapa ni wali waliwa.
 
  • Mwanamke hajakuaga bahati mbaya akirudi unasusa kula,
  • mwanamke kachelewa kupika unasusa,
  • Kasemeshwa njiani unaona basi unasusa,
  • kapigiwa simu bahati mbaya umeona unaamua kususa!


Hawaaminiki
 
Mwanamke nae akiona anasuswa ajitafakari si rahisi sisi kususa kilicho kitamu,hapa ni wali waliwa.
wewe kichwa ndani ya nyumba; kichwa kipofu huathili hadi kiwiliwili kuliwa
 
Back
Top Bottom