TAFAKARI: Mwanaume akitaka lake hakuna wa kumzuia

BAFA

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
3,059
5,927
Wakuu nimeona nilete kisa hiki cha ukweli kwenu, kuna dingi mmoja anaishi magomeni mapipa, alikuwa na mapenzi sana na mke wake ila ikafika wakati akapata mchepuko, sasa kwa heshima ya mke wake, dingi wakati wa kuchepuka anaaga kwa mke wake anaenda jogging (walking) kuanzia saa 11 mpk saa 3 usiku anarejea nyumbani, kumbe muda ule alikuwa anaenda kuchepuka Nyumba ndogo.

Sasa mkewe akamshutukia baada kama mwezi hivi mke wake akaomba siku hio waanze jogging pamoja dingi akamkubalia basi bi mkubwa akajitaarisha jogging ikaanza wakaanza kutoka magomeni mpaka ubungo, bi mkubwa bado anaenda nae tu.

Dingi akakunja ubungo kulia mpaka mlimani city, bi mkubwa nae yumo dingi akaendelea kutoka mliman city mpaka ubungo tena kufika ubungo tena akaiingia njia ya kwenda kimara bi mkubwa kuona hivi akamwambia mumewe utaniua bure najua fika unamchepuko nilikuwa nakutext tu wacha nipande gari nirudi nyumbani
 
Back
Top Bottom