Thad
JF-Expert Member
- Mar 14, 2017
- 13,402
- 31,652
Kosea kujenga ila usikosee kuoa/kuolewa. Pengine maneno haya yanaonekana ni ya 'kiswahili' sana, lakini yana maana kubwa sana. Watu wengi wameharibikiwa kimaisha kwasababu tu walikosea kuoa/kuolewa. Ni vyema kujiuliza na kutafakari haya kabla ya kuoa/kuolewa ili upunguze hatari ya kujutia ndoa yako maisha yako yote:
a) Je, unahitaji baba/mama bora au unahitaji mume/mke bora? Kuna wanaume wameumbwa kuwa baba bora na wanawake ambao ni mama bora. Hawa ni wenzi ambao baada tu ya watoto kuzaliwa mapenzi yao huhamia kwa watoto wao na sio kwa wenza wao kama ilivyokuwa mwanzo. Kwao watoto ndio kipaumbele chao kuliko mke/mume.
Mke/mume bora, hawa vipaumbele vyao vya kwanza ni wenza wao,watoto baadae.
Watu wengi wamekuwa wakipata shida sana katika ndoa zao kwa kuwa wenzi wao hawawajali kama wanavyojali watoto wao. Ndoa za watu wenye haiba moja (wazazi bora au wenza bora) mara nyingi hudumu kwa amani.
b) Je, (mwanaume) huyo umpendaye ataweza kuwa msaidizi wako? (mwanamke) utaweza kuwa msaidizi wa mwanaume umpendaye? Mungu alimuumba Eva/Hawa ili awe msaidizi wa Adamu, vivo hivyo mwanaume unapotaka kuoa yakupasa uoe mwanamke atakaye kuwa msaidizi wa majukumu uliyonayo, hapa hatuangalii mwanamke atakayechangia pato la familia,hapana, tunaangalia yule atakayekuwa nawe bega kwa bega katika shughuli zako. Mfano, kama wewe ni daktari basi umpate mwanamke atakayekuwa tayari kuvumilia 'shift za night'. Vinginevyo mtaishia kwenye ugomvi kila kukicha. Mwanamke pia ni vyema ukaolewa na yule ambaye utaweza kumsaidia majukumu yake.Mfano,usiolewe na mchungaji wakati unaona huwezi kulibeba jukumu la mama mchungaji.
c) Je, unayetaka kumuoa anakupenda au wewe ndio unampenda? Wengi waliooa/kuolewa na wanaowapenda wao pasipo kupendwa huishia kujutia ndoa zao. Hivyo ni vyema kuoa/kuolewa na unayependana naye kuliko asiyekupenda kwa kujidanganya kuwa ipo siku atakupenda tu.
Nawatakia ndoa njema wote mnaotarajia kuoa/kuolewa

asante