Tafakari, jiamini na weka msimamo

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
New York iko masaa 3 mbele ya Calfornia...lakini hii haimaanishi Calfornia inaenda taratibu au labda New York iko mbio sana..Zote ziko sawa isipokuwa kila moja ina TIME ZONE yake

Kuna mtu yuko single sasa hivi. Kuna mtu ameolewa na kusubiri miaka 10 kabla ya kupata mtoto..wakati kuna mtu amepata mtoto ndani ya mwaka wa kwanza wa ndoa

Au, kuna mtu amemaliza degree akiwa na miaka 22, lakini akasubiri miaka 5 kabla ya kupata kazi, wakati kuna mwingine amemaliza degree akiwa na miaka 27 na akapata kazi mwaka huo huo

Kuna mtu kawa mkurugenzi akiwa na miaka 25 na kufariki akiwa na umri wa miaka 50 , wakati mwingine amepata ukurugenzi akiwa na miaka 50 na kuishi mpaka miaka 90

Kila mmoja anaishi kulinga na TIME ZONE yake

RAFIKI ZAKO, NDUGU ZAKO AU WADOGO ZAKO WANAWEZA KUONEKANA MBELE YAKO , AU WENGINE NYUMA YAKO
KILA MMOJA HAPA DUNIANI ANATEMBEA/KUISHI KWENYE BARABARA YAKE PEKE YAKE YA MUDA..MUNGU ANA MPANGO TOFAUTI KWA KILA BINADAMU..TOFAUTI NI MUDA TU..
Tazama , Obama anastaafu akiwa na miaka 55, Trump anaanza akiwa na 70.

USIMWONEE WIVU ,WALA KUMLAUMU MTU, KILA MMOJA NA TIMEZONE YAKE

ENDELEA KUJIAMINI, KILA KITU KITAKUWA SAWA.

HAUJAWAHI WALA HAUJACHELEWA..ISSUE NI TIME ZONE YAKO TU

USIUMIZWE SANA KICHWA KWAMBA ..MBONA MWENZANGU KAJENGA MIMI BADO, ANA GARI MIMI SINA, KAOLEWA MIMI BADO..KAOA MIMI BADO....N.K

CHAPA KAZI KWA BIDII,HUKU UKISUBIRIA MUDA WAKO..MCHE MUNGU UMTEGEMEE...KILA UFANYALO FANYA KWA IMANI.
Weakend njema
 
Sometimes huwa nawaza sana hatma ya maisha yangu kumbe sijachelewa ,Ngoja nikazane maana umri unakimbia kama rocket, pamoja na kwamba kila MTU ana TIMEZONE yake ila kisiwe kigezo cha kukaa tu bila kufanya kazi nakuanza kusubili mafanikio,tupambane vijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa kutukumbusha,.japo kibinadamu unaweza ona kama umechelewa mnooo kumbe ni suala la "muda"tuu,..muhimu ni kuishi kwa tumani na imani Mungu wetu hawai wala hachelewi hujibu kwa wakati,wakati wako ukifika umefika tuu na utaona na kushangaa goliati wako anavyoanguka kirahisi wakati pengine miaka nenda rudi ulikuwa unamshindwa...

Mungu akatupe mioyo ya imani na uvumilivu tukiamini IPO siku kama sio leo basi kesho Mungu ataifanya njia,tusiache kufanya kazi kwa bidii na kumcha yeye pekee katika Roho na kweli.
 
wa stendi they told me everybody's 15 minutes in a different time zone
And since i have it wacha nikae kwa kona patiently and wait for my regime.
I trust the process.
 
Kwani hamna mifano mingine ya kutoa mpaka kwenye vitabu vya dini?
Muandishi wa makala,pamoja sana..
 
Ahsante kwa kutukumbusha,.japo kibinadamu unaweza ona kama umechelewa mnooo kumbe ni suala la "muda"tuu,..muhimu ni kuishi kwa tumani na imani Mungu wetu hawai wala hachelewi hujibu kwa wakati,wakati wako ukifika umefika tuu na utaona na kushangaa goliati wako anavyoanguka kirahisi wakati pengine miaka nenda rudi ulikuwa unamshindwa...

Mungu akatupe mioyo ya imani na uvumilivu tukiamini IPO siku kama sio leo basi kesho Mungu ataifanya njia,tusiache kufanya kazi kwa bidii na kumcha yeye pekee katika Roho na kweli.
Amen
 
wa stendi . Umeongea vyema, ila kwa kuongezea kukaa kwenye 'zone' yako na kusubiri bila kuwa na malengo/mipango/ndoto utasubiri sana. Juhudi zako ndio mafanikio yako.
 
Back
Top Bottom