Kwa kusema ukweli ..., yeye aliyelalamikia UCHOCHEZI wa magazeti ndiye mbaguzi, mchochezi na dikteta . .
Katiba yetu inaruhusu watanzania kupata na kushirikishana habari, kutoa maoni, ili mradi hawavunji sheria . .
Kama kuna gazeti limefanya uchochezi kweli.., vyombo halali kikatiba vya kushughulikia kosa hilo vipo .. Kushughulikia watanzania wasema ukweli, kunyamzisha magazeti na vyombo vingine vya habari sio kazi tuliyomtuma pale Ikulu . .
Watanzania wakiona njaa, ni lazima waseme .., sio kwanza , eti .., wapate kibali cha kusema au kutoa maoni kutoka magogoni ..
Watanzania wakiona kiongozi wao ni mbaguzi, anatumbua watu kikanda, kiitikadi . . , au anatumia vyombo vya dola kukandamiza demokrasia . . , watanzania watasema . . !
Namna ya watanzania kufikisha maoni yao huko Ofisi Kuu ni kwa kupitia vyombo vya habari . . , na Bunge..
Kudhibiti vyombo hivi vya habari na Bunge ni kutudhibiti akili zetu, maono yetu sisi wananchi, ni kwenda kinyume na Katiba yetu . .
Sisi ktk JF . . , kama watu huru . . , tukemee mambo haya yanayoashiria kuibuka utawala wa KIIMLA hapa Tz. .