MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Ni dhambi kubwa sana kuuambia umma kua vyombo vyetu vya habari vinaweza kusababisha hali kama ya 1994, hii sio sawa! Tunatiana hofu bila sababu yeyote.
Hivi ni lini gazeti la Mtanzania, Tanzania Daima au Mwananchi limeandika kuhusu ukabila, udini, ukanda, rangi yetu au nafasi ya mtu kwenye jamii? Tusome tu historia ili tufahamu vyema UCHOCHEZI ulikuwa ukifanywa na vyombo vya habari huko Rwanda enzi hizo kabla ya Genocide.
Mwaka juzi huko Zanzibar tuliona na jinsi watu walivyobeba mabango kuwaponda wenzao kwa kuwabagua kwa rangi na kanda zao. Hao waliyafanya hayo wako wapi hivi sasa?
Tujaribu kuyachunga haya kwa u makini mkubwa ili kuilinda nchi yetu.