Tafadhalini sana, tusipende kuchukulia mfano Rwanda kuhusu UCHOCHEZI na Vyombo vyetu vya Habari

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Ni dhambi kubwa sana kuuambia umma kua vyombo vyetu vya habari vinaweza kusababisha hali kama ya 1994, hii sio sawa! Tunatiana hofu bila sababu yeyote.

Hivi ni lini gazeti la Mtanzania, Tanzania Daima au Mwananchi limeandika kuhusu ukabila, udini, ukanda, rangi yetu au nafasi ya mtu kwenye jamii? Tusome tu historia ili tufahamu vyema UCHOCHEZI ulikuwa ukifanywa na vyombo vya habari huko Rwanda enzi hizo kabla ya Genocide.

Mwaka juzi huko Zanzibar tuliona na jinsi watu walivyobeba mabango kuwaponda wenzao kwa kuwabagua kwa rangi na kanda zao. Hao waliyafanya hayo wako wapi hivi sasa?

Tujaribu kuyachunga haya kwa u makini mkubwa ili kuilinda nchi yetu.
 
Irrelevant example.....kamwe huwezi kulinganisha ya Rwanda na Tanzania hata Kenya na Tanzania.

Nilimsikia wakati akiongea hiyo habari jana. Alipomaliza nikapiga magoti nikasema 'Ee Mungu umsaidie rais wetu, umpe hekima ya kuongoza, kinywa chake ukitawale wewe ili maneno yanayotoka yawe matamu yasije yakawa ni kiberiti katika msitu mkavu'
 
Mtu asiyejua Saddam Hussein alikuwa Rais wa wapi wala asiyejisomea ili kufahamu wahanga wa matukio kama matetemeko walisaidiwaje na serikali zao kwenye nchi zingine hawezi kuwa na uwezo wa kujua ukweli wa jinsi mauaji ya kimbari yalivyotokea au jinsi yalivyochochewa.
Naamini anatumia muda mwingi zaidi kutafuta watu wa kuwalipizia visasi na kusikiliza majungu kuliko kufahamu world affairs. Hii ni aibu kubwa.
 
Na ndio maana tunapaswa kumwombea!
 
Kwa kusema ukweli ..., yeye aliyelalamikia UCHOCHEZI wa magazeti ndiye mbaguzi, mchochezi na dikteta . .

Katiba yetu inaruhusu watanzania kupata na kushirikishana habari, kutoa maoni, ili mradi hawavunji sheria . .
Kama kuna gazeti limefanya uchochezi kweli.., vyombo halali kikatiba vya kushughulikia kosa hilo vipo .. Kushughulikia watanzania wasema ukweli, kunyamzisha magazeti na vyombo vingine vya habari sio kazi tuliyomtuma pale Ikulu . .

Watanzania wakiona njaa, ni lazima waseme .., sio kwanza , eti .., wapate kibali cha kusema au kutoa maoni kutoka magogoni ..

Watanzania wakiona kiongozi wao ni mbaguzi, anatumbua watu kikanda, kiitikadi . . , au anatumia vyombo vya dola kukandamiza demokrasia . . , watanzania watasema . . !
Namna ya watanzania kufikisha maoni yao huko Ofisi Kuu ni kwa kupitia vyombo vya habari . . , na Bunge..
Kudhibiti vyombo hivi vya habari na Bunge ni kutudhibiti akili zetu, maono yetu sisi wananchi, ni kwenda kinyume na Katiba yetu . .

Sisi ktk JF . . , kama watu huru . . , tukemee mambo haya yanayoashiria kuibuka utawala wa KIIMLA hapa Tz. .
 
I don't know what's real anymore when it comes to his excellency.
 
anafanya maovu kupitia mgongo wa kitu fulani ili kuhalalisha ovu lake hicho ni kichaka cha kujifichia kuwatisha watu na mawazo yao nchi zote zinazokosolewa ziliingia kwenye machafuko? kiongoz wetu bwana nawaza ya kwamba anaijua siri ya ushind wake wa urais kama ulishinda ki halalai ya nini kuogopa kukosolewa?
 
Kwanza sidhani kama hata hao Wanyarwanda wanataka kusikia mtu wa taifa lingine akiropoka ropoka majukwaani kusemea ya kwao yaliyopita na kuwaachia maumivu! Kila kukicha tusiwe kama Rwanda!!! Huo ni udhaifu mkubwa kiuongozi.
Reality! A nice comment ever
 
Ni dhambi kubwa sana kuuambia umma kua vyombo vyetu vya habari vinaweza kusababisha hali kama ya 1994, hii sio sawa! Tunatiana hofu bila sababu yeyote.

Hivi ni lini gazeti la Mtanzania, Tanzania Daima au Mwananchi limeandika kuhusu ukabila, udini, ukanda, rangi yetu au nafasi ya mtu kwenye jamii? Tusome tu historia ili tufahamu vyema UCHOCHEZI ulikuwa ukifanywa na vyombo vya habari huko Rwanda enzi hizo kabla ya Genocide.

Mwaka juzi huko Zanzibar tuliona na jinsi watu walivyobeba mabango kuwaponda wenzao kwa kuwabagua kwa rangi na kanda zao. Hao waliyafanya hayo wako wapi hivi sasa?

Tujaribu kuyachunga haya kwa u makini mkubwa ili kuilinda nchi yetu.
Namuunga mkono Rais kwenye hili suala. Kuna magazeti yana mislead sana na kinachotisha zaidi ni uwepesi wa watanzania kuamini huo uwongo.
 
Kama Taifa tunatakiwa kutubu kwa kufanya hii dhambi..Pogba amekuwa ni janga linalotugharimu kwa kiasi kikubwa sana..matamko yake ni uchochezi kuliko hayo magazeti
 
Mtu asiyejua Saddam Hussein alikuwa Rais wa wapi wala asiyejisomea ili kufahamu wahanga wa matukio kama matetemeko walisaidiwaje na serikali zao kwenye nchi zingine hawezi kuwa na uwezo wa kujua ukweli wa jinsi mauaji ya kimbari yalivyotokea au jinsi yalivyochochewa.
Naamini anatumia muda mwingi zaidi kutafuta watu wa kuwalipizia visasi na kusikiliza majungu kuliko kufahamu world affairs. Hii ni aibu kubwa.
World affairs ni zipi mkuu!! Ndo Mara yangu ya kwanza kusikia hili neno
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom