Tafadhalini Ikulu, msidhalilishe Kanisa

Ndio wamekwenda kujitambulisha,hamtaki mnaacha, kama vipi wangebaki kwenye makanisa yao,...
 
Mdogo akisemewa; msemaji ataitwa muongo, mpika majungu au mchochezi. Mkubwa akisemewa; msemaji wake ataitwa Msemaji Mkuu, Katibu Mwenezi, au Afisa habari Mkuu!
 
Ndio wamekwenda kujitambulisha,hamtaki mnaacha, kama vipi wangebaki kwenye makanisa yao,...
Wewe ukimtembelea mdau mwenzako kwa kukaribishwa maana yake umeenda kujitambulisha? Hiyo lugha ya kujitambulisha inatumika kwa wageni, unapoenda ukweni kuposa au balozi anayekuja nchini kuiwakilisha nchi yake nchini sio kwa wenyeji.

Kama mnatetea uandishi huo wa kikanjanja, siku wakialikwa Ikulu viongozi wa vyama vya upinzani, mtasema wameenda kujitambulisha.

Vv
 
Acha kuweweseka , Maaskofu wakienda kujitambulisha kuna shida gani? Ukristo ni pamoja na kunyenyekea , unyenyekevu ndio ukristo wenyewe, ukristo hautafuti ukuu , bali kunyenyekea na kujishusha ili Mungu ainuliwe .
 
Kwani tanzanite La msiba limeandikaje
 
Maaskofu na wenyewe wamezid kujipeleka kwa mkulu
 
Acheni kukuza na kufanya mambo yawe makubwa nawakati ni swala la kueleweka tu. Walienda kumuona mkuu wa nchi na kujitambulisha kwasababu ni uongozi mpya wakaona si vibaya kwenda kumuona mkuu wa nchi kwa maswala ya kimwili waweze kuunganisha na maswala ya kiroho.

Watz punguzeni kukuza haya maswala jaman.
 
Unawezakuta raisi mwenyewe aliwaita ili atubu, YASIRI YATAKUWA WAZI ONEDAY. SUBILI
 
Unawezakuta raisi mwenyewe aliwaita ili atubu, YASIRI YATAKUWA WAZI ONEDAY. SUBILI
Soma neno la Mungu kibeseni acha kuweweseka , watumishi wa Mungu wanahitaji unyenyekevu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…