TAFADHALI USIPITE BILA KUCHANGIA:MSAADA KUHUSU CVT

TAFADHALI USIPITE BILA KUCHANGIA:MSAADA KUHUSU CVT

inspectorbenja

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
635
Reaction score
705
Ndugu zangu,kama unajua kitu toa msaada wa kielimu kwa anayeomba msaada.Kukaa kimya kwako mwenzakl anapata hasara kubwa sana wakati ungemuelimisha angesaidika na Mungu wa mbinguni angekubariki.
Nina Suzuki Swift 2008,engine yake ni K12B,gearbox yake ni cvt,haina dip stick.
Sasa mara ya kwanza nimeuliza sana humu naweka transmission gani maana mi nililiwa sijui mambo haya ya cvt.Nikaweka atf ya suzuki badala ya cvy mwaka huu cvt belt imekatila nankusagika sagika.Sasa nimeorder used.
Kuanzia hapa nataka niwe makini sana.Manual ya gari online inanimislead.
Utafiti wangu unaonesha hizi gearbox zinatengenezwa na Jatco.
Sasa kimbembe maelezo yanakuwa mengi sana
1.Machaposho mengine yanasema weka Atlantis ni universal na haina shida.
2.Machapisho mengineyanafai kwa gari hii niweke Suzuki CVT Green 2
3.Machapisho mengine yanaelekeza niweke NS2 ambayo pia huwa inatumika kwenye nissan.
Kwa watalaam wa haya mambo tafadhali naomba usipite bila kucoment.
Naombeni kuelimishwa.
 
Kama hautaki mambo mengi, chukua hii picha nenda Kariakoo ukatafute.
IMG_8620.jpeg

Nadhani lita 5.5 hivi inakaa.
 
Ukikosa kabisa hakikisha fluid utakayoweka ina specs au imeandikwa “NS-3/J4 CVT Fluid”

IMG_8621.jpeg
 
CVT na DCT ni transmission nzuri ila za kifala sana ikisha swala la fluids.
 
Nasikia hata GP5 inatumia DCT...
Haijakuletea ufala wowote?
Kuna special fluid kwa ajili ya DCT?
GP5 inatumia DCT ndio. Kila 45-50,000 km unachange fluid. UKISAHAU UMEISHA.
 
Back
Top Bottom