Tafadhali Soma mrejesho huu

Aisee Jamaa amejieleza hadi raha.

Kama alivyosema MAMA hapo juu.
Je unawadhamini wa uhakika?
Nakuambia hivyo kwa maana moja kwamba,hata mtu unapoajiriwa kazini unajaza sehem ya wadhamini wako.
Mie mwenyewe kwenye Biashara yangu ya Bodaboda tu na Carry,nimejazisha watu mkataba serikali za mtaa yao na kila mmoja alikuja na Mdhamini mwenye mali isiyohamishika au dhamna yenye uwezo wa kulipa.
Maana miaka ya nyumba Kila dereva alisema amekabwa na chombo kimechukuliwa,siku ya tatu unapata habari kapiga issue mwenyewe kwa kupanga dili,sasa tangu yaingie mambo ya kujazishana mikataba kesi hizo hakuna tena.

Sasa muhim ni kudhibitisha kwamba una wadhamni wa uhakika,mie binafsi nimependa sana ulivyoanisha.
Ningekuwa sawa tungefanya biashara ya Bajaji,maana ndio sijaijaribu hiyo,hope ungenipa mwanga na huko nikajua changamoto zake.
Tuombeane mungu,nimeweka kumbukumbu zako kama hali ikiwa sawa nitakutafuta kama pia masharti na vigezo vitakuwepo.
 
Back
Top Bottom